DPP awafutia Tundu Lissu na Wahariri wa Gazeti la Mawio kesi ya Uchochezi

DPP awafutia Tundu Lissu na Wahariri wa Gazeti la Mawio kesi ya Uchochezi

Rejea toka maktaba za online:

KESI NAMBA 208 / 2016


Alichosema Hakimu Thomas Simba kesi ya Tundu Lissu

IJUMAA , 6TH NOV , 2020
NA MWANDISHI WETU
Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba, ameahirisha kesi inayomkabili Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu na wenzake ya kuchapisha habari ya uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti kwa kile alichokieleza kuwa anaimani tarehe nyingine



TUNDU%20LISSUE.jpg

Tundu Lissu
itakayopangwa mshtakiwa atafika Mahakamani hapo.
Hakimu Simba amesema kuwa kama mshtakiwa atashindwa kufika Mahakamani hapo tarehe iliyopangwa basi hatua nyingine na kisheria zitafuatwa na kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 3 mwaka huu.

Mbali na Lissu, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya jinai namba 208/2016 ni Mhariri wa Gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

Inadaiwa Januari 12 hadi 14, 2016 jijini Dar es Salaam, washtakiwa Jabir, Mkina na Lissu, waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar.’

Katika shtaka la pili wanadaiwa Januari 14, 2016 walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.
 
Naona leo lisu meno njenje baada ya ofisi ya DPP kufuta kesi yake na mwenzane wa gazeti la mawio Jabri Idrisa

Sasa lisu yuko huru kuna nchi imetoa msamaha hadi kwa wazandiki kama lisu

USSR
Screenshot_20210922-111100.jpg
 
Mama anaondoa makando kando ya mwendazake..ili aupige mwingi zaidi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Kijasusi na hata Kidiplomasia njia pekee ya Kummaliza Adui yako ni Kujishusha Kwake, Kujinyenyekeza, kuwa nae Karibu sana, Kumpenda Kinafiki, Kumsoma vyema na Kiustadi kisha unammaliza vizuri na kinidhamu kabisa huku Mhusika akiwa haamini lakini pia anafurahia huko Kumalizwa Kwake.
 
Hujui chochote kuhusu ujasusi wala diplomasia, unajipa umuhimu usiokuwa nao kama teja wa unga.
Kijasusi na hata Kidiplomasia njia pekee ya Kummaliza Adui yako ni Kujishusha Kwake, Kujinyenyekeza, kuwa nae Karibu sana, Kumpenda Kinafiki, Kumsoma vyema na Kiustadi kisha unammaliza vizuri na kinidhamu kabisa huku Mhusika akiwa haamini lakini pia anafurahia huko Kumalizwa Kwake.
 
Back
Top Bottom