DPP kuridhia mashtaka dhidi ya vigogo kesi za TAKUKURU?

Hamna lolote longo longo tu hadi leo hawajafungwa MAFISADI. Subira yenye heri imekwisha changa la macho la kila siku.
 
UCHUNGUZI dhidi ya tuhuma za ufisadi dhidi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha katika Serikali ya awamu ya tatu, Basil Mramba, umechukua sura mpya, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), Eliezer Feleshi kukamilisha kazi yake.

Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa tayari jalada la uchunguzi huo limesharejeshwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa ajili ya kufanyika kazi zaidi.

Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa, Mramba anachunguzwa kutokana na tuhuma za ufisadi katika misamaha ya kodi ambayo ilitolewa kwa mabilioni ya shilingi kwa wafanyabiashara katika mazingira tata.

Feleshi alilithibitishia Mwananchi Jumapili katika mahojiano maalumu ofisini kwake, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuwa jalada la kesi hiyo lilifikishwa ofisini kwake na amemaliza kulifanyia kazi.

Alisema baada ya kumaliza kulifanyia kazi amewakabidhi Takukuru kwa ajili ya kulifanyia kazi zaidi.

"Tumelirudisha kwao ndiyo wanaojua ambacho wanaedelea nacho, kwa hiyo nini kinafanyika ni bora muwaulize wao," alisema Feleshi.

Alipoulizwa kama ofisi yake imetoa maelekezo ya kufunguliwa mashtaka au kulifanyia kazi zaidi jalada hilo, alisema kwa kawaida taratibu zao haziruhusu kueleza nini ofisi hiyo imeandika katika jalada la uchunguzi.

Feleshi aliongeza kwamba, Takukuru ambao ndiyo wanaochunguza tuhuma hizo ndiyo wenye mamlaka ya kueleza hatua iliyofikiwa.

Mkurugenzi huyo alifafanua kwamba, taratibu za kiutendaji haziruhusu kueleza nini ambacho ofisi hiyo imeandika kwenda kwa mhusika.

Alisema taratibu zote zinazofanyika ikiwamo kama ni mashtaka, mhusika pia anapaswa kupewa taarifa.

"Hakuna kitu kinafanyika kwa siri, hata mhusika (mtuhumiwa) lazima awe anapewa taarifa za mchakato," alisisitiza Feleshi.

Hata hivyo, uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini zaidi kwamba kuna mipango mbalimbali ya chini kwa chini, inayofanywa na serikali ya kutaka kuwafikisha mahakamani baadhi ya vigogo nchini kwa tuhuma za ufisadi.

Taarifa kutoka ndani ya serikali zinaeleza kwamba, majalada mbalimbali ya uchunguzi yameanza kupelekwa katika ofisi ya DPP.

Alipoulizwa taarifa za majalada ya baadhi ya vigogo wengine kuchunguzwa na kupelekwa ofisini hapo, alisema wingi wa majalada katika ofisi hiyo ni kitu cha kawaida.

Naibu Mkurugenzi wa Takukuru, Lilian Mashaka, alisema pamoja na taarifa hizo kuwa za kweli, hawezi kusema chochote kwa kuwa sio msemaji wa taasisi.

Alishauri gazeti hili kuwasiliana na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hosea, kwa maelezo ya kina kuhusiana na suala hilo.

Kauli ya Mashaka ilirudiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa taasisi hiyo, Alex Mfungo, aliyesema kuwa taasisi hiyo ina taratibu zake katika kutoa taarifa na kwamba mkurugenzi mkuu ndiye msemaji.

"Nyie mkitaka taarifa hizo njooni ofisini, mfuate utaratibu, sio kila mtu anasema kila kitu. Msemaji wa taasisi ni mmoja tu," alisema Mfungo.

Hata hivyo, Dk Hosea hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo, baada ya simu yake ya mkononi kuita mara kadhaa bila kupokelewa.

Kwa upande wake, Mramba alipotafutwa kwa njia ya simu jana kwa ajili ya kutoa ufafanuzi kuhusiana na suala hilo, alisema hawezi kuzungumzia mambo yaliyopo katika ofisi za watu wengine bila kufafanua zaidi.

Ikiwa mwanasiasa huyo atafikishwa mahakamani, itakuwa ni mara ya pili kwa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuwashtaki watendaji wake wa zamani ikianzia na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, anayeendelea kujitetea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. Profesa Mahalu anatuhumiwa kuiibia Serikali Sh 2 bilioni kutokana na kuongeza bei wakati wa mchakato wa ununuzi wa Jengo la Ubalozi wa Tanzania, mjini Rome.

Pia kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa rasmi kwamba, serikali iko mbioni kuwashtaki watu wanaotajwa kuhusika katika wizi wa mabilioni ya fedha za umma, katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wale waliohusika kuipa zabuni kwa upendeleo Kampuni hewa ya kufua umeme wa dharura ya Richmond Development LLC.

Rais Kikwete alimuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, kuongoza timu ya wataalamu akisaidiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Saidi Mwema na Mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hosea kuchunguza na kuwashtaki watu ambao watabainika kuhusika na wizi wa Sh 133 bilioni kutoka katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika BoT.
 
Mwendesha Mashtaka akamilisha uchunguzi kuhusu Basil Mramba
Na Ramadhan Semtawa

UCHUNGUZI dhidi ya tuhuma za ufisadi dhidi ya aliyekuwa Waziri wa Fedha katika Serikali ya awamu ya tatu, Basil Mramba, umechukua sura mpya, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), Eliezer Feleshi kukamilisha kazi yake.

Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa tayari jalada la uchunguzi huo limesharejeshwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa ajili ya kufanyika kazi zaidi.

Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa, Mramba anachunguzwa kutokana na tuhuma za ufisadi katika misamaha ya kodi ambayo ilitolewa kwa mabilioni ya shilingi kwa wafanyabiashara katika mazingira tata.

Feleshi alilithibitishia Mwananchi Jumapili katika mahojiano maalumu ofisini kwake, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuwa jalada la kesi hiyo lilifikishwa ofisini kwake na amemaliza kulifanyia kazi.

Alisema baada ya kumaliza kulifanyia kazi amewakabidhi Takukuru kwa ajili ya kulifanyia kazi zaidi.

"Tumelirudisha kwao ndiyo wanaojua ambacho wanaedelea nacho, kwa hiyo nini kinafanyika ni bora muwaulize wao," alisema Feleshi.

Alipoulizwa kama ofisi yake imetoa maelekezo ya kufunguliwa mashtaka au kulifanyia kazi zaidi jalada hilo, alisema kwa kawaida taratibu zao haziruhusu kueleza nini ofisi hiyo imeandika katika jalada la uchunguzi.

Feleshi aliongeza kwamba, Takukuru ambao ndiyo wanaochunguza tuhuma hizo ndiyo wenye mamlaka ya kueleza hatua iliyofikiwa.

Mkurugenzi huyo alifafanua kwamba, taratibu za kiutendaji haziruhusu kueleza nini ambacho ofisi hiyo imeandika kwenda kwa mhusika.

Alisema taratibu zote zinazofanyika ikiwamo kama ni mashtaka, mhusika pia anapaswa kupewa taarifa.

"Hakuna kitu kinafanyika kwa siri, hata mhusika (mtuhumiwa) lazima awe anapewa taarifa za mchakato," alisisitiza Feleshi.

Hata hivyo, uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini zaidi kwamba kuna mipango mbalimbali ya chini kwa chini, inayofanywa na serikali ya kutaka kuwafikisha mahakamani baadhi ya vigogo nchini kwa tuhuma za ufisadi.

Taarifa kutoka ndani ya serikali zinaeleza kwamba, majalada mbalimbali ya uchunguzi yameanza kupelekwa katika ofisi ya DPP.

Alipoulizwa taarifa za majalada ya baadhi ya vigogo wengine kuchunguzwa na kupelekwa ofisini hapo, alisema wingi wa majalada katika ofisi hiyo ni kitu cha kawaida.

Naibu Mkurugenzi wa Takukuru, Lilian Mashaka, alisema pamoja na taarifa hizo kuwa za kweli, hawezi kusema chochote kwa kuwa sio msemaji wa taasisi.

Alishauri gazeti hili kuwasiliana na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hosea, kwa maelezo ya kina kuhusiana na suala hilo.

Kauli ya Mashaka ilirudiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa taasisi hiyo, Alex Mfungo, aliyesema kuwa taasisi hiyo ina taratibu zake katika kutoa taarifa na kwamba mkurugenzi mkuu ndiye msemaji.

"Nyie mkitaka taarifa hizo njooni ofisini, mfuate utaratibu, sio kila mtu anasema kila kitu. Msemaji wa taasisi ni mmoja tu," alisema Mfungo.

Hata hivyo, Dk Hosea hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo, baada ya simu yake ya mkononi kuita mara kadhaa bila kupokelewa.

Kwa upande wake, Mramba alipotafutwa kwa njia ya simu jana kwa ajili ya kutoa ufafanuzi kuhusiana na suala hilo, alisema hawezi kuzungumzia mambo yaliyopo katika ofisi za watu wengine bila kufafanua zaidi.

Ikiwa mwanasiasa huyo atafikishwa mahakamani, itakuwa ni mara ya pili kwa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuwashtaki watendaji wake wa zamani ikianzia na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, anayeendelea kujitetea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. Profesa Mahalu anatuhumiwa kuiibia Serikali Sh 2 bilioni kutokana na kuongeza bei wakati wa mchakato wa ununuzi wa Jengo la Ubalozi wa Tanzania, mjini Rome.

Pia kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa rasmi kwamba, serikali iko mbioni kuwashtaki watu wanaotajwa kuhusika katika wizi wa mabilioni ya fedha za umma, katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wale waliohusika kuipa zabuni kwa upendeleo Kampuni hewa ya kufua umeme wa dharura ya Richmond Development LLC.

Rais Kikwete alimuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, kuongoza timu ya wataalamu akisaidiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Saidi Mwema na Mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hosea kuchunguza na kuwashtaki watu ambao watabainika kuhusika na wizi wa Sh 133 bilioni kutoka katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika BoT
 
msiwe waabishi, wanaweza kumpeleka mahakamani kama vile mchezo wa kuigiza, ili kutengeneza move lingine kama lile la naila kiula, halafu baadaye atshinda kesi, kimchezo mchezo. mafisadi wana njia nyingi za kuhadaa. kama wanaweza kutengeneza filamu kama ya balali hili litawashinda?
 
Hurray! kwa mbali mwanga wa mapambazuko waanza kujitokeza taratibu na kuleta marumaini mapya kwa watanzania, wafikishwe maakamani tuone uzalendo wa majaji kwa mafisadi wanaomaliza nchi yetu.

Mkubwa hamna kitu hapo, kama watu waliweza kutoa kanya boya Richmond iweje washindwe kwa Mramba.

Huyu Banyamulenge (HOSEA) mwenye MWIZI, sasa wewe umeona wapi kesi ya Nyani ukampelekea Tumbili tena ya Mahindi.

Wakubwa hapo tumeliwa. Ila mimi wala sijakata tamaa hawa tutakomaa nao tuu.
 
Ama kweli watanzania bwana, hebu ni lini akili zetu zitakuwa na ufahamu? Eti Mramba anashitakiwa, kwa kosa gani jamani? Mramba ni mtu huru ndani ya nchi yake huru, haya mengine ni kelele za chura, tukitaka kumshitaki Mramba kwanza tuanze na .................................., kisha afuate.S..................... Na mwisho hawa mawaziri wengine.

Basi mshitakini muone cha moto, atatoa siri zote, mpaka mchanganyikiewe.
 
Kanyaga boya ili
Kikwete kushinda kwa 80% ni kutokana na pesa za BOT, ambazo mramba alikuwa waziri wa Fedha chini ya Fisadi mkuu Mkapa, hivyo huyu Kikwete hawezi lolote hapa kwani Mramba kashika mpini jamani
Tusahau haya, hata siku moja hakuna litakalotokea Tanzania, kuwapeleka Mafisadi Mahakamani, ni sawa na Bush kukaa meza moja na Osama jamani

BABA H
Nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani. Mimi ni mgumu sana kuamini vipi kesi ya nyani asikilize Ngedere, siamini vipi inawezekana Ngedere aamuru Nyani aliyemletea mahindi akamatwe, lazima kitakuwa ni kiini macho tu. Lakini pamoja na pessmism tuliyonayo tuendelee kusubiri, unaweza kushangaa kuwa inakuwa ni kiini macho kama cha Nalaila Kiula.
 
Kama kungekwua na dhamira ya kuwashitaki, kesi ingekuwa imeshamalizika na mwenye kuwa Segerea angekuwa anakaribia kumaliza kifungo. CHANGA LA MACHO HILO
 
Changa la Macho lingine hilooooooooo... Nimewahi kusema tena kuwa tutapiga kelele weee ila hakuna kitakachofanyika hapa Tanzania.. Ila ni vizuri tujifurahishe tuu huku JF ili kupunguza machungu But nothing will be done in Tanzania regarding MAFISADI. Wana pesa nyingi sana ambazo hata PM wetu anaziogopa, wana mitandao mikubwa sana. Naomba niulize na mwenye data aniambie. Mramba ameweka watu wake wengi sana pale Hazina kila mtu anajua na mkitaka hata majina nitawapatia. Kuna watu wa sehemu fulani waliandikisha majina yao ili wapatiwe kazi serekalini, kama utani vile 2005 aliwaingiza watu kama 4 ninaofahamu mimi waliojiandikisha kwenye hiyo orodha, unafikiri hao watu wataweza kumgeuka leo hii? Hapa tunapigishana kelele tuu.

Tusubirie tuone labda kweli Watanzania wameamka
 
Mkuu isaya heshima mbele
sasa haya mambo ya dash dash mbona hapa hakuna
hapa ni kumwaga vitu

kwani ni kazi kubwa hapo kusena tuanze na MKAPA kusha tufuate na SUMAYE??
 
CCM ipo kimyaaaaaaaaa inatafuta uongo wa kutupatia....
 
hamna kitu hapa! itachukuwa miezi kadhaa hadi ripoti ya tukukuru itoke.....na ikifikishwa mahakani tutaambiwa ushahidi hautoshi!
sitaki kusema, lakini sina imani na serikali yetu
 
munakumbuka hii stori hizi?

http://www.raiamwema.co.tz/08/03/26/index.php

http://www.thisday.co.tz/News/3951.html

kuna mambo mawili yanawezekana katika hili suala

1. PCCB hawakuleta facts za kutosha kwa DPP na hivyo facts zaidi zahitajika ili ku-justfy ufunguliwaji wa mashtaka

2. Kulindana, i.e involves a chain of other prominent figures
 
Count down ya Ripoti ya EPA...............
 
Hii system inasound kama office ya mganga wa kienyeji bwana, kama DA ameshamaliza kuandaa file kilichotakiwa ni kumburuza mramba mahakamani. I can't wait kusikia Mramba VS United Republic of Tanzania, na kitakachonivutia zaidi ni kusikia kwamba Mramba ahukumiwa miaka 30 jela.
 
Vigogo mafisadi waitisha serikali

Waandishi Wetu Julai 16, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Kesi zao zakwama kufunguliwa

WATUHUMIWA wakubwa wa rushwa na ufisadi, wanaelezwa kupumua baada ya kufanikiwa kuwatisha viongozi na watendaji wa juu wa Serikali ili kesi dhidi yao zisitishwe, Raia Mwema imebaini.

Habari za ndani ya Serikali zinaeleza kwamba uchunguzi wa kesi kadhaa uliokuwa katika hatua za mwisho na hata zile kesi ambazo zimekamilika 'zimegonga mwamba' na watendaji huenda sasa 'wakageuziwa kibao'.

Kwa mujibu wa habari hizo, taarifa zilizovuja na kuwafikia wahusika zilipenyezwa kutoka ndani ya vyombo vya Serikali na hivyo kuwafanya watuhumiwa hao kuanza kupambana kuhakikisha wanajihami kwa nguvu zote.

"Kesi zote kubwa sasa zimegonga mwamba baada ya watendaji na viongozi wa juu wa Serikali kutishwa na watuhumiwa ambao baadhi wana mahusiano nao kikazi ama waliwahi kufanya kazi pamoja," anaeleza ofisa mmoja wa ngazi ya kati serikalini.

Na mwanasheria mmoja mwandamizi ameiambia Raia Mwema wiki hii kwamba, kwa sasa inabidi Serikali iwe makini maana watuhumiwa wameungana kuhakikisha 'wanajibu mapigo' kwa yeyote ambaye anashiriki 'kuwaangamiza'.

Imeelezwa kwamba hata zile kesi kubwa 10 ambazo Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea, aliwahi kutamba kwamba ziko katika hatua nzuri, nazo hazitoweza kufikishwa mahakamani na wahusika sasa wanapumua.

Kwa mujibu wa habari hizo, watuhumiwa hao wamefanikiwa kuvivuruga hata vyombo vya dola kwa kuwagawa na kuwachafua watendaji wa vyombo hivyo na sasa wameahidi kutumia nguvu zao zote kupandikiza watu wao ndani ya vyombo hivyo, kimoja kikiwa ni TAKUKURU.

"Hivi sasa wanajitapa kwamba wataweka watu wao TAKUKURU na kwenye vyombo vingine ambavyo wanaamini kwamba kuna watendaji ambao wana nia ya kuwashughulikia, wakidai kwamba watendaji hao wametumwa kuwamaliza," anasema ofisa mwingine ndani ya Serikali aliye karibu na masuala ya kesi hizo.

Hosea alipata kunukuliwa akitangaza hadharani kwamba ofisi yake inachunguza kesi 10 kubwa za ufisadi, akisema kesi tano kati ya hizo ziko katika hatua za mwisho za kufunguliwa mashitaka akiungwa mkono na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ambaye alitaja hata kesi ambazo amekwisha kuzitolea kibali cha kufikishwa mahakamani.

Hata hivyo, hadi sasa hakuna hata kesi moja iliyofunguliwa mahakamani na baadhi ya watuhumiwa wamediriki kutamka hadharani kwamba hakuna mwenye 'ubavu' wa kuwafikisha mahakamani.

"Mwaka huu (2008) kufikia Julai tutakuwa tumekamilisha kesi tano za kwanza… hizi ni kesi za rushwa kubwa kubwa. Na tabia ya kesi za rushwa kubwa ni kwamba inakuwa na madhara makubwa kwa uchumi wa nchi, wahusika huwa ni watu wakubwa, kiasi cha rushwa kinachohusishwa ni kikubwa, eneo la uchunguzi wake huvuka mipaka ya ndani na nchi za nje, zinahusisha maandiko mengi, zinahitaji kiasi kikubwa kwa uchunguzi na huvuta hisia za jamii," alinukuliwa Hosea akisema.

Habari zilizochapishwa na vyombo vya habari zimezitaja kesi kumi zinazochunguzwa kuwa kuwa ni pamoja na ile inayohusu mradi wa mgodi wa dhahabu uliopo Kahama wa Buzwagi, kampuni tata za Meremeta, Tangold, Deep Green na Mwananchi Gold ambazo zilichota fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kesi nyingine zilizotajwa ni pamoja na ile inayohusu kampuni ya ukaguzi wa madini ya Alex Stewarts, tuhuma zinazohusu ujenzi wa majengo pacha ya BoT, mradi wa mkaa wa mawe wa Kiwira, utata katika miradi ya umeme wa dharura na ununuzi wa rada ya kijeshi kutoa kampuni ya BAe Systems ya Uingereza.

Aidha ilipata kuripotiwa kwamba wanasiasa waliopata kushika nafasi za uwaziri wa fedha, walitarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni, taarifa zilizothibitishwa na maelezo ya DPP, Elieza Feleshi aliyenukuliwa akithibitisha kutoa kibali cha mashitaka kuhusiana na mmoja wa wanasiasa, hao lakini hadi sasa hakuna kesi iliyokwisha kufunguliwa mahakamani.

Miongoni mwa kesi zinazotajwa kuwa na ushahidi wa kutosha ni pamoja na ile inayoihusu kampuni ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation ya Washington DC, Marekani iliyopewa kazi ya kukagua mahesabu ya makampuni ya uchimbaji dhahabu.

Mbunge wa Karatu (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa, amewahi kunukuliwa akisema kwamba chini ya mkataba wake na Serikali, kampuni hiyo inalipwa asilimia 1.9 katika ya asilimia 3 za mrahaba inaolipwa Serikali ya Tanzania na makampuni ya madini ya dhahabu.

Dk. Slaa alisema kufuatana na barua ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu, katika mwaka wa fedha 2005/06, Alex Stewart (Assayers) walilipwa shilingi 14,175,753,189.46 kama malipo ya ukaguzi wa mahesabu ya makampuni ya dhahabu, ijapokuwa "hakuna ripoti za ukaguzi zilizowasilishwa na wakaguzi hawa kuhusu ukaguzi uliofanywa katika mwaka 2005/06."

Akimnukuu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Dk. Slaa alisema, "hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kwamba wakaguzi hawa wa dhahabu walipatikana kwa kufuata utaratibu wa zabuni ya ushindani."

"Kuna taarifa za kuwapo kwa rushwa na/au ufisadi kuhusiana na mkataba kati ya Serikali na Alex Stewart Assayers. Barua pepe iliyoandikwa na Erwin Flores ambaye ni Makamu wa Rais Mtendaji wa kampuni hiyo ya Novemba 14, 2006 inamtaja mtu mmoja mwenye wadhifa wa Waziri katika serikali ya Jamhuri ya Muungano na kuwa yeye pamoja na wenzake ambao hawakutajwa wana asilimia 12.5 za hisa kwenye kampuni hiyo na kuwa analipwa na kampuni hiyo," alisema Dk. Slaa.

Sehemu kubwa ye kesi hizo, ni mambo yaliyofanyika katika kipindi cha mwisho cha utawala wa awamu ya tatu ambayo ilijitambulisha kwa maofisa waandamizi serikalini kufanya kazi bila kujali kana kwamba walikuwa wakitarajia kuhama nchi.

Matukio kadhaa ya uhalifu kabambe miaka hiyo ya mwisho wa awamu ya tatu yanaonyesha mtiririko wa wizi wa kughushi, rushwa kabambe na maamuzi yasiyozingatia sheria, kanuni na taratibu za utendaji kazi serikalini.
 
Last edited by a moderator:
Serikali yenye vyombo vya dola inatishwa na mafisadi na kufyata mkia!!!! Kweli hapa kuna jambo kubwa sana lililojificha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…