Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hurray! kwa mbali mwanga wa mapambazuko waanza kujitokeza taratibu na kuleta marumaini mapya kwa watanzania, wafikishwe maakamani tuone uzalendo wa majaji kwa mafisadi wanaomaliza nchi yetu.
Asante sana ndugu
Ni watanzania wachache tunaoweza kuona mbali kaka, naomba mungu awafumbulie wote wajue haya mambo
Hii serikali inatudanganya na kwa sababu ishajua kuwa sisi ni wepesi wa kudanganywa na hatuwezi kuoji na niwepesi wa kusahau
Hivyo wanachofanya ni kuja na uongo kila kukicha ili kutusahaulisha yale ya nyumba.
Maskini sie wadanganyika sijui tutaendelea kuwa namna hii mpaka lini
Ama kweli watanzania bwana, hebu ni lini akili zetu zitakuwa na ufahamu? Eti Mramba anashitakiwa, kwa kosa gani jamani? Mramba ni mtu huru ndani ya nchi yake huru, haya mengine ni kelele za chura, tukitaka kumshitaki Mramba kwanza tuanze na .................................., kisha afuate.S..................... Na mwisho hawa mawaziri wengine.
Basi mshitakini muone cha moto, atatoa siri zote, mpaka mchanganyikiewe.
Mawaziri kushitakiwa kwa tuhuma za ufisadi
Mwandishi Wetu
Machi 26, 2008
SERIKALI inakamilisha taratibu za kuwashitaki mawaziri wa zamani wawili wanaotuhumiwa kwa ufisadi, Raia Mwema imefahamishwa.
Habari za uhakika zilizopatikana na kuthibitishwa na maofisa waandamizi wa Serikali zinaeleza kwamba mawaziri hao (majina tunayo) walihojiwa na vyombo vya dola kwa mara kadhaa na sasa mchakato wa kuwashitaki uko katika hatua za mwisho.
Wote wawili walipata kuongoza Wizara ya Fedha, chini ya utawala wa Rais Benjamin Mkapa na mmoja aliteuliwa katika serikali mpya ya Rais Jakaya Kikwete kabla ya kuachwa katika mabadiliko yaliyofanyika hivi karibuni.
Mhe. Pesambili Mramba
Kwa mujibu wa habari hizo, mmoja amekuwa akichunguzwa kufanya maamuzi kadhaa yenye utata, ikiwamo kutoa misamaha ya kodi ambayo kisheria hakuwa na mamlaka nayo akiwa anatuhumiwa kuvuka mipaka ya mamlaka yake katika kutoa misamaha.
Mwingine anaelezwa kuchunguzwa kuhusika na maamuzi kadhaa akiwa Waziri katika Wizara ya Fedha na Wizara ya Nishati na Madini, lakini haikuweza kufahamika mara moja ni eneo gani hasa ambalo mwanasiasa huyo mstaafu amechunguzwa.
Mawaziri wote wawili wanatajwa sana kuwa karibu na Mkapa katika masuala kadhaa ya kiutendaji na hata katika masuala kadhaa binafsi na inaelezwa kwamba baadhi ya mambo yaliyochunguzwa yanaweza kumgusa moja kwa moja Rais huyo mstaafu.
Mkapa anatajwa kuhusika moja kwa moja na mradi mkubwa wa mkaa wa mawe wa Kiwira, akiwa na maslahi binafsi katika kampuni ya Tanpower Resources, ambayo iliuziwa hisa za kampuni ya Kiwira Coal Mines Limited iliyokuwa ikimilikiwa na serikali kabla ya ubinafsishaji.
Mhe. Daniel Yona
Pamoja na Mkapa kutajwa katika maeneo mengi, bado kumekuwa na maelezo ya kutaka "aachwe apumzike", huku baadhi wakitumia kinga ya kikatiba ambayo rais mstaafu anakuwa nayo pamoja na kupingwa na baadhi ya wanasheria.
Haikuweza kufahamika mara moja mawaziri hao walichunguzwa katika maeneo gani mengine zaidi lakini kuna uhakika kwamba uchunguzi huo uligusa pia misamaha ya kodi iliyofanywa katika kipindi mawaziri hao wakiwa madarakani.
Miongoni mwa mambo ambayo yaliguswa ni mkataba kati ya Serikali na wakaguzi wa Alex Stewarts waliokuwa wakifanya ukaguzi wa mapato katika sekta ya madini.
Eneo jingine tata ambalo linatajwa kuguswa ni mkataba wa Serikali na kampuni ya Tanzania International ContainerTerminal (TICTS) wa kukodisha eneo la bandari ya Dar es Salaam, mkataba ambao hadi sasa umekuwa ukipigiwa kelele na wadau mbalimbali wa sekta ya bandari.
RAIS Mstaafu Mkapa
Hata hivyo, mawaziri wote wawili walikuwa ama na mahusiano ya karibu na Mkapa kikazi na hata kibinafsi mambo ambayo yanazidi kuonyesha ni jinsi gani Serikali italazimika kumtaja ama kumgusa rais huyo mstaafu katika uchunguzi na hatimaye mashitaka.
Ikiwa wanasiasa hao watafikishwa mahakamani, itakuwa ni mara ya pili kwa Serikali ya Kikwete kuwashitaki watendaji wake wa zamani ikianzia na aliyekuwa Balozi wa Tanzania Italia, Profesa Costa Mahalu, anayeendelea kujitetea katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, akituhumiwa kuiibia Serikali Sh bilioni 2 kutokana na ununuzi wa jengo la ubalozi, Rome.
Hata hivyo, kiu kubwa ya Watanzania kwa sasa iko kwa watu wanaotajwa kuhusika katika upotevu wa mabilioni ya fedha za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wale waliohusika na mradi tata wa umeme wa dharura wa Richmond Development LLC.
Pamoja na Rais Kikwete kuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, kuongoza timu ya wataalamu akisaidiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Saidi Mwema na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa (Takukuru), Edward Hosea, kulikuwa na kazi iliyokwisha kuanza kufanywa na vyombo hivyo ndani ya BoT na maeneo mengine nyeti kiuchumi.
Revealed: What Mramba is accused of
-Probe zeros in on suspect tax deal with gold audit firm
-His comment: ''I don't know what you�re talking about''
THISDAY REPORTER
Dar es Salaam
FORMER finance minister Basil Mramba is being investigated for dubious tax exemptions given to US company Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation, which was awarded a controversial gold auditing contract by the third phase government in 2003, it has been revealed.
Mramba, who has already been questioned by investigators from the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB), has declined to make any comment about the allegations, telling THISDAY: ''I have no comment...I don't know what you are talking about.''
Latest findings by THISDAY have confirmed that the PCCB investigation against the veteran Rombo Member of Parliament, who is now in line for formal prosecution, has centred on the tax exemptions issue in relation to Alex Stewart (Assayers).
The US firm signed a two-year renewable contract with the Bank of Tanzania (BoT) on June 14, 2003, to audit production and exports from the country's booming gold mining industry. The contract was renewed for another two years in 2005.
Under the deal, Alex Stewart Assayers was paid by the government a staggering 70bn/- during the duration of the contract, equivalent to two-thirds of the country's total royalty turnover from gold exports.
Although Alex Stewart Assayers was able to uncover much cheating by most of the major gold mining companies in the country through under-declaration of profits and other means, the terms of the company's contract with the government have remained a subject of heavy criticism in various circles, including the National Assembly.
According to our sources, the investigation is zeroing in on a number of controversial tax exemptions that Mramba may have offered to the US company, contrary to government regulations.
There have also been allegations that various individuals related to either Mramba himself or former BoT governor Dr Daudi Ballali were employed by Alex Stewart Assayers in highly suspicious circumstances.
Investigations by THISDAY have already established that the office of the Director of Public Prosecutions (DPP) has given the PCCB a formal go-ahead to file criminal charges against Mramba.
The Director of Public Prosecutions, Eliezer Feleshi, confirmed that his office had processed the PCCB file on Mramba, but declined comment when asked if his office had issued its consent for prosecution.
However, well-placed sources confirmed that the DPP's office had indeed given the formal consent paving the way for PCCB to prosecute the former minister.
''We expect formal charges to be brought against Mramba at the Kisutu Resident Magistrate's Court in Dar es Salaam...it is now just a matter of time,''a source familiar with the issue told THISDAY.
The 68-year-old Mramba served as finance minister for five years from 2000 to 2005, in the second and final term of the third phase government under ex-president Benjamin Mkapa.
Before being appointed finance minister, Mramba served as minister for industries and trade in the Mkapa administration from 1995 to 2000.
From 2006, he served as minister for infrastructure development in the fourth phase government of President Jakaya Kikwete, later being reappointed minister in charge of industry, trade and marketing, before eventually being dropped after the dissolution and re-composition of the cabinet in February this year.
..................Alisema baada ya kumaliza kulifanyia kazi amewakabidhi Takukuru kwa ajili ya kulifanyia kazi zaidi.
"Tumelirudisha kwao ndiyo wanaojua ambacho wanaendelea nacho, kwa hiyo nini kinafanyika ni bora muwaulize wao," alisema Feleshi................