DPP: Sheikh Ponda anahusika na Al-Shabaab!

DPP: Sheikh Ponda anahusika na Al-Shabaab!

Status
Not open for further replies.
teh teh ndo tanzania na maajab
hahah. raha ya siku hizi ni vita kati ya waislam na wakiristo. sio kama tulivyozea kwamba waislam tu ndio wanaopigwa na Polisi wakiristo wanakaa pembeni kunywa soda na Kupongeza na kuwpongeza watawala. Style hii mpya inaweza ikajenga heshima ndani ya jamii yetu
 
waacheni waandamane, mbona swala la kuchinja mmewakubalia bila masharti.?
 
*asema anadaiwa kuhusika na al-shabaab, vurugu za zanzibar
*polisi yawaonya waislamu wanaotaka kuandamana kesho

mkurugenzi wa mashitaka nchini (dpp), eliezer feleshi, amesema hatumii madaraka yake vibaya kumnyima dhamana katibu wa jumuiya na taasisi za kiislamu tanzania, sheikh ponda issa ponda na mwenzake.

Amesema kwamba, amezuia dhamana dhidi ya sheikh ponda kutokana na taarifa, kwamba watuhumiwa hao wanahusishwa katika vurugu mbalimbali zilizotokea nchini na nje ya nchi.

Mawakili wanaomtetea sheikh ponda na mwenzake walikutana na dpp feleshi mwezi huu, kujadili ni kwa nini haondoi zuio la dhamana kwa wateja wao. Katika mazungumzo yao, dpp aliwaambia kwamba hatumii madaraka vibaya, bali kuna sababu za msingi.

Waliokutana na dpp ni wakili juma nassoro na yahaya njama, ambao jana waliiambia mahakama ya hakimu mkazi kisutu, kwamba wamezungumza na dpp ofisini kwake ili kupata sababu zilizomfanya uzuie dhamana ya sheikh ponda na mwenzake.

"dpp alituita tukajadili suala la dhamana ya akina ponda, alituambia kwamba, barua tuliyomwandikia kuomba aondoe zuio la dhamana haijamfikia, hivyo tumwandikie nyingine.

"alikataa kwamba, hatumii madaraka yake vibaya kwa kuzuia dhamana ya washitakiwa hao, isipokuwa alifanya hivyo kwa ajili ya usalama kutokana na taarifa zilizomfikia kutoka jeshi la polisi.

"katika maelezo yake, dpp hakueleza moja kwa moja sababu za kuzuia dhamana ya akina ponda, lakini alieleza viashiria kwamba, kuna taarifa za sheikh ponda kuhusishwa na vurugu zilizotokea markaz chang'ombe, dar es salaam, vurugu za zanzibar, vurugu zilizotokea kenya, tetesi za kuhusika na kuingia kwa kundi la al-shabaab nchini na pia kulikuwa na taarifa za kuhusika na mauaji ya sheikh mmoja kule mombasa, kenya na suala jingine ni malalamiko kwamba ponda siyo raia.

"alitueleza kwamba, kuwapo ndani kwa sheikh ponda siyo kwa maslahi ya nchi peke yake, bali hata kwa usalama wake, pia endapo kuna watu wanataka kumdhuru au la," aliongeza wakili njama. Alisema pamoja na kumpa barua hiyo dpp, kwa mara nyingine, hadi jana walikuwa hawajapata majibu kama maombi yao yamekubaliwa au la.

Dpp akizungumza na mtanzania kwa simu jana, alikiri kukutana na mawakili hao kujadili suala la dhamana ya sheikh ponda. Pamoja na hayo, alisema amepanga kukutana na wanazuoni wa dini ya kiislamu nchini februari 28, mwaka huu, kwa lengo la kujadili suala la dhamana ya washitakiwa hao. Katika uamuzi huo, alisema baraza la wanazuoni wa kiislamu liliwaandikia barua mawakili wa sheikh ponda wakiomba wakutane naye kuzungumzia hatima ya dhamana ya washtakiwa hao.

"barua waliyoandika nimeiona februari 11 na mimi nimepanga kukutana nao niwasikilize na tuelimishane pia, kwa sababu hii ni ofisi ya umma ambayo mtu yeyote yuko huru kufika."

kutokana na amri ya dpp kuzuia dhamana ya sheikh ponda, waislamu walifanya kongamano februari 3, mwaka huu maeneo ya mwembe yanga, temeke, wakihamasishana kufanya maandamano makubwa kesho kuelekea kwa dpp endapo washitakiwa hao hawatadhaminiwa.

Katika kusisitiza maandamano hayo, shura ya maimam na jumuiya na taasisi za kiislamu tanzania, walimwandikia barua kamanda wa polisi, kanda maalum ya dar es salaam, suleiman kova, wakimtaarifu juu ya maandamano hayo.

"tunakutaarifu kwamba februari 15, mwaka 2013, kutakuwa na maandamano ya amani ya waumini wa kiislamu baada ya swala ya ijumaa kutoka misikiti mbalimbali kuelekea ofisi ya dpp.

"madhumuni ya maandamano hayo ni kutaka kujua sababu inayopelekea dpp kuzuia haki ya dhamana kwa viongozi wa dini ya kiislamu, akiwemo ponda, katika kesi ya kiwanja iliyopo mahakamani takribani miezi minne," ilisema sehemu ya taarifa hiyo kwa kamanda kova.

Sheikh ponda na salehe mukadam wako rumande tangu kesi hiyo ilipofikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu kwa mara ya kwanza, oktoba mwaka jana, kwa kuwa dpp aliwasilisha hati ya kuzuia dhamana zao.

Sheikh ponda na wenzake 49, wanakabiliwa na mashitaka matano, yakiwamo ya kuingia isivyo halali katika uwanja wa markaz chang'ombe na kujimilikisha uwanja huo ambao ni mali ya agritanza limited. Pia, wanakabiliwa na mashitaka ya kuwachochea wananchi hadi wakakusanyika katika uwanja huo, kuvunja na kuiba vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani zaidi ya sh milioni 59, mali ya agritanza limited.

Kesi hiyo inatarajiwa kutajwa leo katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu, mbele ya hakimu mkazi, victoria nongwa. Wakati huo huo, mwenyekiti wa baraza la habari la kiislamu tanzania, sheikh said mwaipopo, ametoa tamko kwa waumini wa dini ya kiislamu, akiwataka wasishiriki maandamano yaliyopangwa kufanyika kesho kupinga sheikh ponda kunyimwa dhamana. Sheikh mwaipopo liyasema hayo jana, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam.

"sisi sote tunajua kuwa, maandamano ni haki ya kila mwananchi, lakini lazima yaratibiwe na yakubalike na kutolewa kibali na polisi. Katika hili, sisi tumeshawasiliana na kamanda kova na amekanusha hilo," alisema mwaipopo.

"watakaoandamana wajue watazidi kumweka ponda katika mazingira mabaya, kwani hatatolewa kwa dhamana kirahisi kama wanavyotaka na hawataitendea haki serikali na waislamu kwa ujumla.

Naye mwenyekiti wa taasisi ya islamic peace foundation, sadiq godi, alisema wananchi wanatakiwa kujua ni kwanini ddp amefunga dhamana ya sheikh ponda.

Katika hatua nyingine, kaimu kamanda wa polisi, kanda maalum ya dar es salaam, ahmed msangi, aliiambia mtanzania kwa simu, kwamba waislamu wanaotaka kuandamana wanaligawa taifa.

"hawa waislamu wasitake kuligawa taifa kwa udini, huku wakiweka kisingizio cha kudai haki zao. Tunawaomba waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari wasiwaunge mkono kwa kuandika habari zao, badala yake tuungane kupinga vitendo hivyo.

"jeshi la polisi halitavumilia vitendo vyovyote vinavyoashiria uvunjifu wa amani, tumejipanga kudhibiti hali hiyo, maana tumesikia kwamba baada ya kutoka misikitini siku ya ijumaa, wataandamana kwenda kwa dpp, nawaambia wasijaribu," alisema.

"katika zuio hili kuna sababu tano zinazotufanya tusiruhusu maandamano hayo, ya kwanza ni hatuna polisi wa kutosha kulinda misikiti yote jijini dar es salaam na ya pili ni kwamba ofisi ya dpp iko katikati ya jiji.

"sababu ya tatu ni kwamba suala wanalolalamikia liko mahakamani, nne ni kwamba wapo wanazuoni walioomba kukutana na dpp na wamekubaliwa na sababu ya tano kuna taarifa za uvunjifu wa amani wakati wa maandamano hayo.

"kutokana na sababu hizi, hatuko tayari kuruhusu maandamano yafanyike na nazidi kuwaambia wasithubutu kuandamana," alisema msangi.

kama dibagula alifungwa kwa kusema yesu si mungu aliachiwa kwa maandamano. Nadahani dpp hawajui waislam vizuri. Kama anashindikizwa na mapadri na maaskofu kumtesa ponda. Asitake kuliangamiza taifa letu kwa udini wake mtu mmoja. Mara utasikia hata yule wa geita ponda alienda kumuua yeye. Kwani liondoka mahabusu usiku kenda geita. Kama kashindwa bush kuua uislam sidhani dpp anaeweza kuungamiza uislam tz
 
KAtika utawala wa Mkapa huyu Ponda alikuwa anaishi wapi? Je alifuata taratibu za kutoka hapa nchini? wakati anarudi je, alifuata pia taratibu za kuingia nchini?? Hapo tutajua kama ni raia au la!
 
Hii mihimili ya Dola laiti ingekuwa huru na yenye kuwajibika sina shaka isingetoa kuwepo nafasi za mambo waliyofanya akina Ponda na wenzake.

Ok maadam hii ni nchi ya vimemo na matamko DPP aendelee mpaka kimemo kingine kitakapompa mwongozo.
 
kama dibagula alifungwa kwa kusema yesu si mungu aliachiwa kwa maandamano. Nadahani dpp hawajui waislam vizuri. Kama anashindikizwa na mapadri na maaskofu kumtesa ponda. Asitake kuliangamiza taifa letu kwa udini wake mtu mmoja. Mara utasikia hata yule wa geita ponda alienda kumuua yeye. Kwani liondoka mahabusu usiku kenda geita. Kama kashindwa bush kuua uislam sidhani dpp anaeweza kuungamiza uislam tz

PAdri na Askofu yupi ndo mtendaji wa Serikali? je, Kikwete, Bilali, Shein, Authman, Kofa, Mwema ndo mapadri wa nyumbani kwako?? Acha ujinga wewe andika kwa busara!!
 
Tulisha andika sana kujihusisha huyu Bw na Alshabab na mimi binafsi naendelea kusisitiza kuwa migogoro ya kidini inaanzia katika mahubiri yanayolenga kukosoa dini nyingine. Mihadhara hii ipigwe marufuku, nashangaa mmeshupalia kuwa vurugu za kidini chanzo ni vyama vya kisiasa. Kule Buseresere kuna ofisi gani ya chama imechomwa moto???


Busara itumike kupiga marufuku mihadhara ya kukashifu dini nyingine.


KUSEMA YESU SIO MUNGU NDIO KASHFA? Hahaha. kashindwa farau kuungamiza uislam. liweze kanisa hap tz? si mnatafuta ya GEITA TU
 
ndiyo tunavyofundishwa kwenye mihadhara yetu....... Kitendo cha kigaidi cha kuvunja makanisa na kuiba hakikubaliki. Kitendo cha kutaka watuchinjie hata vitimoto vyetu sababu wao wamefundishwa na imamu zako kuchinja binafsi sikubaliani nacho. Gaidi hukaa jela nyie muandamane milele sheria itachukua mkondo wake
style ya geita baada ya miaka 10 ccm watajua kwamba kuwaona wakiristo ndio watawala hapa tz itaondoka. Haki na umoja unaweza ukajengwa
 
Hii mihimili ya Dola laiti ingekuwa huru na yenye kuwajibika sina shaka isingetoa kuwepo nafasi za mambo waliyofanya akina Ponda na wenzake.

Ok maadam hii ni nchi ya vimemo na matamko DPP aendelee mpaka kimemo kingine kitakapompa mwongozo.
Mungozo ni maadamano Ijumaa na ikibi ihamie J2 hata yeye asiende kanisani kusali na kuongea na mapadri juu ya kuwadhibiti waislam kwa kisingizo cha sheria
 
Mimi niliwaambia hapa kwamba waislam watacheza sana lakini ikitokea kawekwa lupango basi kazi inakuwa kubwa kutoka mkabisha .Haya sasa yuko huyu mjinga .Mwacheni kwanza akae akitoka atakuwa katia akili

Wewe mpuzi acha Upogo. waislam hawakuanza kuteswa leo. ukisoma Historia ya Bilali kalazwa juani huku akipigwa mawe. unashangaa Sheikh Ponda kuteswa na wakiristo na wanafiki. ukisoma historia ya uislam wala hushangai kuona waislam wakiteswa.nawshangaa waislam waliopewa vyeo wanajishau na kuungana na wakiristo kuwaangamiza waislam wenzao.
 
Hakuna MUNGU anaeamasisha vurugu ni shetani tu ndiyo kazi yake, Kama kweli wasilamu wanamwabudu mungu wa kweli wa tuonyeshe kwa utulivu na upendo.

Mungu hakusema ukibiwa mali yako UMPONGEZE mwizi. MOU wanayo. Vatikana wanamiliki. hata masheikh waandelee kuwanyanayasa? DPP acha udini tenda haki.
 
Huwa naelimisha kama hivi.Nawe saidia katika hili mkuu.Kadhalika watanzania wengi mtu hujikuta akiwa muislam kwa kuwa kazaliwa katika familia ya kiislam na kuwa mkiristo kwa sababu hiyo hiyo. kwa sababu hiyo wengi wamejikuta na dini zao kwa bahati nasibu tu kama mtu anavyojikuta mwanaume au mwanamke. Kadhalika hata tukisema tugombane mwisho wa siku tutaishia tu kuishi kwa chuki badala ya upendo na dini hizi zitaendelea kuwepo.sasa kwa nini tusiamue tu kuendelea kuishi kama mpare anavyoishi na mchaga(Wana taniana tu lakini kirafiki zaidi na hakuna mwenye ugomvi na mwenzake!)

Tatizo kuna watu wanataka tugombane kwa sababu zao binafsi. Hapa ninapoishi jirani zangu ni waislam. Na maisha yetu yapo hivi; wakati wa kristmas huwa napika na familia yake inakuja kwangu, tunatandika mkeka, tunakula. Idd vile vile. Nikinunua kuku nampa anachinja, nabariki kwa imani yangu, tunashare. Ila nikiamini kuwa siyo ibada, ni utaratibu ili tuishi.
Hizi imani tumeanishwa tu. Na ni nadra sana mimi nikiwa naye tunajadili habari za dini, ni maisha ya kawaida tu.
 
kama dibagula alifungwa kwa kusema yesu si mungu aliachiwa kwa maandamano. Nadahani dpp hawajui waislam vizuri. Kama anashindikizwa na mapadri na maaskofu kumtesa ponda. Asitake kuliangamiza taifa letu kwa udini wake mtu mmoja. Mara utasikia hata yule wa geita ponda alienda kumuua yeye. Kwani liondoka mahabusu usiku kenda geita. Kama kashindwa bush kuua uislam sidhani dpp anaeweza kuungamiza uislam tz

Tena huyu DPP inatakiwa awe mfano maana anaanza kutubore.
 
Naamini wakithubutu kuandamana askari watatosha kuwadhibiti misikiti yote. Lakini wakiandamana kwa amani askari wa kuwalinda hawatoshi.

Mkuu... ukweli ulioje! unajua tatizo la hawa watawala wetu wanatoa majibu ya uongo na kitoto kwenye maswali muhimu. Sasa hii inawafanya hata kesho wanaposema ukweli wasiaminiwe. Kuna tatizo gani kusema ukweli?
 
DPP kigugumizi cha nini,hii ndiyo shida ya kufanya kazi za kitaalamu kwa shinikizo toka kwa wanasiasa. Hapa inapigwa danadana baadaye tutasikia huyu gaidi kaachiwa na ataendelea na uchochezi wake.
unamwita mwenzako gaidi kwa kuaje?mbona unakua mpofu wa kufikiri?
 
Nchi yetu inapaswa kuwa na rekodi za kila mtu na shughuli zake katika database ili kufahamu nani mwema na nani si mwema!!
 
daa hii nchi bwana,mtu akidai haki yake tuu,mara gaidi,mara al shabab,sijui mara si raia,hivi shekh ponda yupo hapa tokea lini?kwanini asikamatwe kitambo wakati wanamjua huyu sio raia?apewe haki yake ya dhamana,asinyimwe kisa muislam,mwenzako akinyolewa wewe tia maji,wakristo mnafurahia mashekh wanavyoswekwa rumande,kunyimwa haki zao na mengine,jua nanyi mpo hapa hapa,mlishabikia ray alivyotoa taraka tatu,mkaja juu alivyotoa sister merry
 
Hua najitahidi kufafanua ila bado hamjajua,na dhambi mnayo isapoti itawarudia japo siombei iwe hivyo maana namimi itaniathiri,hivi mashitaka aliyo somewa ponda ndio haya aliyo yasema DPP?kwakua ni mwisilamu mnasapoti uvunjifu wakatiba! Mimi ni mwana harakati naamini nyeupe naiwe nyeupe hata kama haitoninufaisha
 
Seems like when it comes to Ponda, Is guilty till proven innocent? Wataalam wa sheria (na si wataalam wa hisia tafadhali) tuondoeni gizani, vitabu vinasemaje?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom