DPW Special Thread: Uzi maalumu kuhusu kampuni ya DP World

DPW Special Thread: Uzi maalumu kuhusu kampuni ya DP World

"...asili mia kubwa..." ngapi?

Unasema umechunguza, tena sana; lakini hata mifano miwili tu huna?

Wewe unadhani kutumia takwimu ni anasa?
Kuanza kutaja watu kwa kuwashutumu ni hatia zaidi, kama huamini na wewe fanya uchunguzi,
Ila siwezi kuwataja humu
 
Sijui kwanini huyu bibi ushungi kaamua kuuza nchi yetu (siyo yake) kuhuni hivi.
Angekuwepo Nyerere sijui kama mtu huyu andedumu kwenye kiti kwa masaa mengine yanayoitimiza siku moja. Yungemkuta ameshapigwa pini na ameandika barua kuachana na mambo ya kuongoza nchi.
Sasa nyerere si ndie aliuza Tanganyika kbisaaaa? Au Unakusudia nyerere gani?
 
Japo tunayasema yasiyo sahihi mitandaoni dhidi ya Watawala na tuliowachagua wakapuuza, wajue kwamba tunaishi nao mitaani. Kwa karne hii ya TAHEMA, wakikosa madaraka yao ya kisiasa, watatukuta mitaani kama Wahenga walivyonena mpanda ngazi hushuka au aliye juu mngoje chini. Siyo dua la kuku kwani kuna ushahidi wa waliokuwa na madaraka tunao mitaani tunaona maisha yao, labda wachache wansolindwa na Katiba.

Hatujasahau wala hatusahau
[emoji830]︎ ubadhirifu wa mali ya umma, ulioripotiwa na CAG;
[emoji830]︎ matumizi ya hovyo ya kodi zetu, misaada na mikopo;
[emoji830]︎ usimamizi dhaifu wa rasimali za Taifa;
[emoji830]︎ urasimu na uzembe katika maofisi ya umma;
[emoji830]︎ na kadhalika

Tunachohitaji ni Wanasiasa tuliowapa dhamana ya madaraka na mamlaka, kikatiba, kutimiza wajibu wao kama ulivyoanianishwa kwenye Katiba, na siyo kuyatumia kwa maslahi yao binafsi.

Wenye madaraka na mamlaka ya kikatiba, wakumbuke kuwa japo wengine, kwa Katiba ya sasa wanaendelea kulindwa, kana kwamba bado wako madaraka, ninaamini Katiba mpya itawaondolea tupambane nao mitaani kunako huduma hafifu za jamii, miundombinu isiyoridhisha, mlolongo wa tozo, na kero lukuki za maendeleo.

KAZI IENDELEE na Kuupiga mwingi
Well said
 
Sasa nyerere si ndie aliuza Tanganyika kbisaaaa? Au Unakusudia nyerere gani?
Mtazamo wa kuangalia dini ya mtu ni ujinga unaowagharimu huku Pwani hadi leo, ukija huku mikoani hamna huo ujinga wenzetu wananeemeka kwa ujinga wetu kwa kutuibia, wewe unajadili dini zao, haya Nyerere kafa sasa dini yake inakusaidia nini, tuhoji kile kilichoibwa kwa wakati huu, tumia akili zaidi kuliko hisia.
 
Mtazamo wa kuangalia dini ya mtu ni ujinga ulioanzia huko Pwani na bado unaowagharu hadi leo ukija huku mikoani hamna huo ujinga wenzetu wananeemeka kwa kutuibia wewe unajadili dini zao sasa dini ya mtu inakusaidia nini wewe badala ya kuhoji kile kilichoibwa kwa wakati huu.
Duh, sio mchezo bwashee, wapi nimetaja dini?
Kudadeki kweli mumepagawa,
Hivi..... nyerere hakuiuza tanganyika?
Au ulikua hujazaliwa?
 
Duh, sio mchezo bwashee, wapi nimetaja dini?
Kudadeki kweli mumepagawa,
Hivi..... nyerere hakuiuza tanganyika?
Au ulikua hujazaliwa?
Lakini ni viongozi walewale wa ccm wanaendelea kutuibia, maana nyie uvccm mpo humu mnalipwa fedha za walipa kodi mlizoiba na kutugombanisha kututoa kwenye hii issue ya msingi ya bandari, tumewashtukia.
 
Na kalamu Maria Sarungi-Tsehai

Port of Dar - TPA and Benki ya Dunia
Nawarudisha mwaka 2017/18 Benki ya Dunia ilikubali na kuingia mkataba wa mkopo wa maendeleo na serikali wa kuimarisha Bandari ya Dar es Salaam chini ya mradi unaoitwa Dar es Salaam Maritime Gateway Project ambapo dola za kimarekani (USD) milioni 400 ilitolewa kuimarisha miundombunu halisi (phyiscal) na dola milioni 21 kwa ajili ya kuimarisha taasisi na kusaidia kutekeleza mradi Mamlaka ya kutekeleza mradi huu ni TPA - pesa ilienda huko Mradi unaisha 30 June 2024 (mwakani) Kwa kifupi sisi wananchi tutalipa deni hili sehemu kubwa ya milioni 421 iliyotolewa na Benki ya Dunia na kuwekezwa ktk kuimarisha bandari Sasa tuchambue ripoti nini kimefanyika, na kwa nini DP World imetajwa katika ripoti hii?
Katika muhtasari wa Dar es Salaam Maritime Gateway Project report iliyotolewa February 2023 (mwaka huu) inaonyesha kuwa utekelezaji umezidi kuzorota na RISK ya mradi umeongezeka na kuwa SUBSTANTIAL yaani kuna hatari mradi kutotimiza malengo Inaelezwa kuwa mradi huu ulioidhinishwa 2017 na kuanza kutekelezwa 2018 ina mikataba 7 ikiwemo mashirika 5 ya consulting. Utekelezaji bado siyo mzuri na lengo la kuONGEZA UFANISI wa ports and terminals zote zinazoendeshwa na TPA, na kuijengea uwezo kuwa MENEJA na DEVELOPER (mwendelezaji) wa ports zingine huku ikiendelea kutathmini uwekezaji binafsi (tulikuwa bado hatujafikia hiyo hatua)
Katika ripoti ya World Bank ghafla DP World imeibuka Sasa ngoja niwaeleweshe Sehemu ya mkopo na msaada wa $421 milioni kuna pesa ya kujenga mfumo wa IT wa bandari kupitia TPA. Ripoti ya Benki ya Feb 2023 walisema hakuna maendeleo ILA TPA imesema imeingia makubaliano (MoU) na DP World kujenga mfumo huu wa IT ELEWENI: DP World watalipwa kutoka pesa hizi za mkopo wa Benki ya Dunia kusaidia “mifumo isomane” hawawekezi Pili kwa mujibu wa serikali walisema ile MoU ya TPA na DPW ni kuhusu mfumo wa IT (tunaambiwa ilisainiwa Feb 2022) Imekuwaje consultancy ya DPW ya IT imegeuzwa kuwa IGA na tunatoa bandari zetu kwa kusema eti DPW watatusaidia mifumo isomane alafu tunawapa uendeshaji wa bandari ambao UMESHAKAMILIKA kwa uwekezaji mkubwa wa mradi huu? Hii dili ilianza kama CONSULTANCY na kugeuzwa UPORAJI.

Pesa za mkopo wa World Bank zimetumika (na kukamilika) kupanua na kuimarisha Gati 1-7 na kujenga gati mpya Gerezani kupanua mlango wa bandari hadi Gati 11 kuboresha na kuunganisha na reli Kupanua na kuimarisha Gati 8-11 Kuna RORO terminal ilijengwa na kukamilishwa Sasa tuangalie wanachodai DP World kufanya kwa mujibu wa IGA Cha kwanza kikubwa eti kujenga, kuendesha na kusimamia RoRo terminal na Gati 1-4 na gati 5-7 Yaani pesa zote zimewekezwa za walipa kodi kupitia mradi wa sasa wa WB alafu wao wanakuja kuendesha na kusimamia? Wanawekeza nini?? Ndiyo maana mkataba haujawekwa thamani ya uwekezaji wao kumbe wanadandia mradi unaoelekea kukamilika waje wajisifu! Nyieeeeeeeeee! Mnaotetea mkataba huu mnajua kuwa mnatumika kutetea ulaji wa genge ndogo!?
 
Hawa Dp World Kwa makelele yote haya Bado Wana Nia tu kufanya kazi hapa Nchini.
Basi kuna Jambo.
 
Mtazamo wa kuangalia dini ya mtu ni ujinga unaowagharimu huku Pwani hadi leo, ukija huku mikoani hamna huo ujinga wenzetu wananeemeka kwa ujinga wetu kwa kutuibia, wewe unajadili dini zao, haya Nyerere kafa sasa dini yake inakusaidia nini, tuhoji kile kilichoibwa kwa wakati huu, tumia akili zaidi kuliko hisia.
Nyie ndo wapumbavu namba moja huwezi kukuta ubaguzi huku pwani, mnapewa hospitality nzuri ila nyie wachafu ndo mna ubaguzi mara huyu mzanzibar.

Taja sehemu zenye watu wakarimu angalia hata mnavyouana kwa kuwa na chuki na washamba sana .
 
Nyie ndo wapumbavu namba moja huwezi kukuta ubaguzi huku pwani, mnapewa hospitality nzuri ila nyie wachafu ndo mna ubaguzi mara huyu mzanzibar.

Taja sehemu zenye watu wakarimu angalia hata mnavyouana kwa kuwa na chuki na washamba sana .
So do you agree with he sale of the Port?.
 
So do you agree with he sale of the Port?.
Unakuwa na ujinga wapi uliona bandari zinakauzwa .

je unajua Dp world wanafanya kazi vip na TPA nao vip?

Unajua palishakuwa na TICTS kablq je unajua?

Ujinga👉unapiga kelel unaongozwa na mzanzibar tena mwanamke na anaendelea kuongoz na hakuna kitu utafanya wala hao Chadema😅😅
 
Unakuwa na ujinga wapi uliona bandari zinakauzwa .

je unajua Dp world wanafanya kazi vip na TPA nao vip?

Unajua palishakuwa na TICTS kablq je unajua?

Ujinga👉unapiga kelel unaongozwa na mzanzibar tena mwanamke na anaendelea kuongoz na hakuna kitu utafanya wala hao Chadema😅😅
You force us to believe what is not.
 
Kuanza kutaja watu kwa kuwashutumu ni hatia zaidi, kama huamini na wewe fanya uchunguzi,
Ila siwezi kuwataja humu
Wewe huelewi 'moto' ya JF;" where we dare talk openly"?

Tena jambo lenyewe linaloihusu JF na wanachama wake?

Wewe mkuu, utaniwia radhi nikikuita "mwongo"; kwa sababu ndivyo ulivyo katika swala hili.
 
Wasema kweli?

Basi tutatumia hivyo vipande vipande vilivyokwishajadiliwa humu kwa pamoja; badala ya "Makubaliano" yenyewe.

Mkuu 'tpaul' wazo lako hili zuri mbona JF hawalipi umuhimu stahiki na kufanya ulivyopendekeza?
Si kweli mkuu. Nenda kule juu kwenye uzi mkataba tayari umeishawekwa ujisomee mkuu.
 
Back
Top Bottom