DPW Special Thread: Uzi maalumu kuhusu kampuni ya DP World

DPW Special Thread: Uzi maalumu kuhusu kampuni ya DP World

Hujanielewa., soma unielewe nimesema wenye asili ya Tanganyika. Unaposema Tanzania kuna wenye asili ya Tanganyika na asili ya Zanzibar. Kama kweli unafuatilia hii mambo niambie wenye asili ya Zanzibar kama wanalalamika kuhusiana na hii kitu. Unamjua Jussa ni nani, katamka kwa mdomo wake kuwa huo mkataba hautuhusu Wazanzibar watajijuwa Watanganyika wenyewe maana yake nin. Think big maseee..,

Jussa ameongea ukweli kutoka moyoni, so acha kushabikia maovu yanyuma
 
Inashangaza sana ila ndio ukweli kwa sasa.

Nyuzi nyingi zimeanzishwa kuhusu DP World, kuna wanaounga mkono na kuna wanaopinga.

Cha ajabu nimechunguza sana na kuona kuwa asilimia kubwa ya wanaopinga au kuanzisha uzi za kupinga ni new member JF, kwanini?
Huo sio utafiti ni makisio

Tafiti inatakiwa uje na numbers

Wapya asilimia x
Existing asilimia x
 
Halafu mkuu kwa nini mpaka bandari za maziwa makuu nazo ziwemo., au ndiyo yale ya kipindi kile bandari ya bagamoyo kusiwepo na bandari pinzani kwa miaka ....., TRA asikusanye Maputo kwa miaka ...., maana swala la mikataba ni sensitive sana sema tu watawala hawana umakini.
Sa100 hasomi
 
Inawezekana na ndio maana kuna watu naona wamemute
Huo ndio ukweli mzee pale bandarini yupo Anuari wa TRH huyo muhindi ana gari zaidi ya 3000 unadhani akija muarabu ata survive? TICS wamempasia adani ila michezo ni ile ie sema watanzania wengi hatujui yanayoendelea pale bandarini.
 
Mimi wananikera mno kuingiza udini, ukabila na utaifa, yani mtu anaonyesha kabisa chuki kwa watu flani,, hoji suala la mkataba na sio kuingiza udini mara oh huyu mama mzanzibari mara hao wadubai ni ndugu zake, kwani akipewa mwarabu kuna shida gani!! Au mlitaka apewe mzungu, mchina au mhindi ndio mridhike!!
 
Inashangaza sana ila ndio ukweli kwa sasa.

Nyuzi nyingi zimeanzishwa kuhusu DP World, kuna wanaounga mkono na kuna wanaopinga.

Cha ajabu nimechunguza sana na kuona kuwa asilimia kubwa ya wanaopinga au kuanzisha uzi za kupinga ni new member JF, kwanini?
Kwani ulitakaje.
 
Inashangaza sana ila ndio ukweli kwa sasa.

Nyuzi nyingi zimeanzishwa kuhusu DP World, kuna wanaounga mkono na kuna wanaopinga.

Cha ajabu nimechunguza sana na kuona kuwa asilimia kubwa ya wanaopinga au kuanzisha uzi za kupinga ni new member JF, kwanini?
Wafanyakazi wa bandari na sukuma gang
 
wapo kazini. watu wanalipwa kalaga bao wenye akili tushajua nani yupo nyuma yao. mh Rais usiyumbishwe piga kazi watanzania watakuja kukushukuru badae.
Hujajibu hoja

Kwanini ni New members wenye kutumia Id za kujificha?


Ukweli ni Maccm(ktk lugha ya Lisu) Yana mgeuka Maza hivyo yanajipa majina yasijulikane unaweza kukuta yakuna Kasimu muokoaji ktk ndege iliyozama Bukoba ambaye yupo katibu na Maza yupo humu na Id feki
 
Hujajibu hoja

Kwanini ni New members wenye kutumia Id za kujificha?


Ukweli ni Maccm(ktk lugha ya Lisu) Yana mgeuka Maza hivyo yanajipa majina yasijulikane unaweza kukuta yakuna Kasimu muokoaji ktk ndege iliyozama Bukoba ambaye yupo katibu na Maza yupo humu na Id feki
Very smart
 
Very smart
Ukweli wengi akili zetu hazi stuki haraka

Fikiri kama Maza baada ya kupata Uraisi aliweka wazi kuwa walikuwa Wana buruzwa na Jiwe

Itashindi kanaje Majaliwa muokoaji kujificha Kwa Id feki humu na kumsema Maza yupo hovyo?!!!?!!

Tabia za Maccm za hovyo Sana Manafiki kupitiliza yote ni Pangu Pakavu Tia Mchuzi
 
Inashangaza sana ila ndio ukweli kwa sasa.

Nyuzi nyingi zimeanzishwa kuhusu DP World, kuna wanaounga mkono na kuna wanaopinga.

Cha ajabu nimechunguza sana na kuona kuwa asilimia kubwa ya wanaopinga au kuanzisha uzi za kupinga ni new member JF, kwanini?
Hawakuwa member na wanataka kutumia hii forum kueleza dukuduku lao
 
Halafu mkuu kwa nini mpaka bandari za maziwa makuu nazo ziwemo., au ndiyo yale ya kipindi kile bandari ya bagamoyo kusiwepo na bandari pinzani kwa miaka ....., TRA asikusanye Maputo kwa miaka ...., maana swala la mikataba ni sensitive sana sema tu watawala hawana umakini.
Sio kwamba hawako makini,na wala hawajui consequences zake.
Kuna namna fulani wanapofushwa maksudi na wawekezaji.
 
Inashangaza sana ila ndio ukweli kwa sasa.

Nyuzi nyingi zimeanzishwa kuhusu DP World, kuna wanaounga mkono na kuna wanaopinga.

Cha ajabu nimechunguza sana na kuona kuwa asilimia kubwa ya wanaopinga au kuanzisha uzi za kupinga ni new member JF, kwanini?
Pye.... wewe ukitaka hao member wawepo tangu mwanzo wa jf :
1. Je DP-WORLD ilishakuwa imekuja Tanzania?
2. Kwa uelewa wako mdogo unadhani wale member wa zamani ndio wenye haki ya kuleta na kujadili hoja tuu!
3. Next time unapoanzisha mada tumia akili boya wewe!
 
MKATABA WA BANDARI NI WA KIUHAINI,UMEVUNJA KATIBA YA NCHI NA UTAKWENDA KUVUNJA SHERIA ZA NCHI -MWANASHERIA DR NSHALA RUGEMELEZA.

"Mkataba uliosainiwa ni "Binding Agreement" hakuna namna ya kujitoa,kuna propaganda zinasema eti tungoje HGA,this is nonsense,itategemea vipi HGA wakati IGA unasema hauna namna ya kujitoa na ukitaka kujitoa uende katika mahakamani za kimataifa,angalia ibara ya 10,18 na 27 ya mkataba huo ndio utagundua waliosaini mkataba huo walikuwa na dhamira ya kuuza nchi" Mwanasheria Rugemeleza.

Yote yanayofanywa sasa na Serikali ni propaganda kiwaaminisha watu walichofanya ni sahihi,na kilikuwa na nia njema,sasa hatuwezi kuruhusu nia njema kuuza rasilimali zetu-Mwanasheria Rugemeleza.

"Namshukuru Daktari Slaa kwa kulisemea hili,nawashukuru wote waliosimama kuhesabiwa kulisemea jambo hili la kuuzwa kwa rasilimali zetu,nilitegemea Bunge lingeweza kumuwajibisha Rais,kwa maana hakuna aliye juu ya sheria,lakini haikuwa hivyo" Mwanasheria Rugemeleza.

"Mtu mwenye hulka ya wizi lazima atatuibia,mtu mwenye uwezo mdogo wa akili haiwezekani leo ageuke mwenye busara" Mwanasheria Rugemeleza.

"Mkataba uliosainiwa kwa kuuangalia tu kama hauna majeraha ya akili na akili yako iko sawasawa utagundua ule ni mkataba batili,ule ni mkataba haramu,ule ni mkataba usio weza kutetewa na mkataba wenyewe umejivika madaraka kuwa juu ya sheria ya nchi katika ibara ya 27" Mwanasheria Rugemeleza.

"Mkataba uliosainiwa kwa kuuangalia tu kama hauna majeraha ya akili na akili yako iko sawasawa utagundua ule ni mkataba batili,ule ni mkataba haramu,ule ni mkataba usio weza kutetewa ni mkataba unaovunja katiba yetu ya nchi moja kwa moja na mkataba wenyewe umejivika madaraka kuwa juu ya sheria ya nchi katika ibara ya 27" Mwanasheria Rugemeleza.

"Mkataba uliosainiwa unajiweka juu ya sheria ya nchi, mkataba unajiweka juu ya katiba ya nchi,unagandisha sheria za kodi,halafu niliwasikia watu kama kina Tulia wakifokea fokea watu,mtoto mdogo unafokea fokea watu,nilichogundua hajui sheria za mikataba ya kimataifa" Mwanasheria Rugemeleza.

"Mkataba utaisha siku shughuli za bandari zitakapokwisha, mkataba hausemi manufaa ya uwekezaji huo,ni lipi andiko limeandika manufaa ya uwekezaji huo na kusema tunamuhitaji mwekezaji huyu, mkataba utatumia sheria za kodi za siku iliyosainiwa,hautalipa tozo,halafu Mbarawa anatueleza mkataba huu una manufaa,ni yapi hayo manufaa ikiwa mkataba utakuwa juu ya sheria zote za nchi yetu?" Mwanasheria Rugemeleza.

"Viongozi matumbo wamefanya maamuzi ya vizazi vijavyo bila kuzingatia usawa,Wajukuu wetu watakuwa wanaiangalia bandari kama wanavyomuangalia Mama Mkwe na wasifanye lolote, Mkataba wa Rio unasema kufanya maamuzi juu ya vizazi vijavyo kwa kuzingatia usawa, Mkataba unasema utaisha siku,Mwenyezi Mungu akisema Dunia imefika mwisho,tutatawaliwa na Dubai hadi siku Dunia ikifika mwisho"Mwanasheria Rugemeleza.

"Viongozi awa ndio tunawapisha barabarani kwenye misafara yao,Rais aliapa kuilinda na kuitetea katiba,je alichofanya ndicho!!?? sicho,amepoteza uhalali wa kuwa Kiongozi wetu" Mwanasheria Rugemeleza

"Kitendo cha bunge kupitisha mkataba ule ni aibu,ni dharau kwa nchi,awa watu wameisaliti nchi yetu,wote waliosaini na kupitisha ule mkataba majina yao yaandikwe msaliti,mhaini,tuwakemee watu awa kwa hasira maana wameisaliti nchi yetu" Mwanasheria Rugemeleza.

"Na kuhusu suala la Katiba Mpya,nashauri tukae tuchague watu wa kwenda kutuandikia katiba yetu lakini sio awa waliopo" Mwanasheria Rugemeleza

"Ibara ya 14 kuhusu fidia (Prompty and adequate compassition) utalipa fidia ya hasara ya Sasa na ya mbeleni iliyopotea inapingana na ibara ya 24(2) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayosema alipwe fidia inayostahili,inapingana na ibara ya 4 na ibara ya 2 la Umoja wa mataifa ya International investment law inayosemwa alipwe fidia inayostahili,Mimi PhD yangu ni ya International investment law na nimesomea Havard,na Mimi sio Mwanasheria uchwara,huu mkataba umeiuza nchi na kukiuka katiba ya nchi yetu" Mwanasheria Rugemeleza

"Mkataba uliosainiwa ni "Binding Agreement" hakuna namna ya kujitoa,kuna propaganda zinasema eti tungoje HGA,this is nonsense,itategemea vipi HGA wakati IGA unasema hauna namna ya kujitoa na ukitaka kujitoa uende katika mahakamani za kimataifa,angalia ibara ya 10,18 na 30 ya mkataba huo ndio utagundua waliosaini mkataba huo walikuwa na dhamira ya kuuza nchi" Mwanasheria Rugemeleza.

"Spika alikuwa anakuja kwetu kama mwanafunzi wa kujifunza intern kuulizia haya mambo ya International investment law,Leo anajifanya yeye anajua sana,hii ni kejeli,dharau na jeuri,hii inatuonesha sisi Watanzania hatujawafundisha viongozi wetu kutuheshimu,zile kanuni za Tanu wao hawajazisoma,kwa hiyo sisi wanatufanya watwana wao,ndio maana licha ya ibara 27 kusema Tanzania itawajibika kwa Dubai,wao wanakata mayenu wanasema mkataba huu uko sawa sawa"Mwanasheria Rugemeleza.

"Ukiangalia ibara ya 28 uhaini mkubwa umefanyika dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mkataba huu wa bandari na hili nalisema bila kumung'unya maneno haya yamefanywa na Kiongozi namba moja,bunge na wote waliosaini" Mwanasheria Rugemeleza

"Viongozi wetu hawana uhalali wa kuendelea kukaa madarakani,wenzetu waislamu kama umemtendea baya lazima akuoneshe alivyochukia, Watanzania lazima tuoneshe tulivyochukia,hapa lazima tuvue gloves,kama kupigwa basi zipigwe kavu kavu kuonyesha jinsi tulivyochukia" Mwanasheria Rugemeleza.
"Mimi sio mtoto mdogo tena,nimepata miaka yangu yote ya kuishi na nimepata akili nyingi juu ya sheria za nchi na kimataifa,namshukuru Mungu,Sasa siwezi kuruhusu mtoto wangu au mjukuu wangu aishi katika ujinga namna hii,huu ni mkataba haramu,danyanyifu,mkataba wa kuuza nchi, mkataba uliovunja katiba"Mwanasheria Rugemeleza.

"Mkataba huu umevuja kwa namna ya ajabu sana,je mikataba mingapi haijavuja na kuna madudu kama,uliposainiwa mkataba huu ilisainiwa mikataba mingine mingi hapo Dubai,kwa hili lililotokea tutawaamini vipi awa viongozi wetu,wamepoteza uhalali wa kuaminiwa na Wananchi"Mwanasheria Rugemeleza.
Duuh 🙄
Mtetezi wa mkataba wa DPW FaizaFoxy njoo ujibu huku
 
Back
Top Bottom