Pre GE2025 Dr. Asharose Migiro, Mary Nagu walifaa kugombea Urais kupitia CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mama anawatoa nnyaa si mchezo. Iko hivi, aliyepandishwa na Mungu kamwe hawezi kushushwa na mashetani........mkashifuni kwa kashfa zozote mzitakazo lakini milele atabaki mbele yenu kwa miaka 10000. Historia ameshaiandika na anaendelea kuiandika.
🤣🤣🤣🤣🙏🙏🙏🙏
 
Hivi huyu mama alitokea wapi mpaka akafika hapo alipo?

Amekuwa Waziri kwa miaka 10

Kabla ya hapo amefanya kazi UN kwa miaka zaidi ya 10

Wanamponda Mama humu hawajawai kupata cheo hata cha ujumbe wa mtaa.

Hawajawai kufanya kazi hata ya u teller wa bank.

Ila wanamkashifu Mama samia
 
Ninashangaa sana wanaomkazania na kumpa chepuo mgombea urais wa chama cha mapinduzi mpaka inafika wakati unajaribu kuhoji uwezo wa akili zao.Leo hii Tanzania imefikia hatua CCM hata wakimsimamisha mgombea mwenye changamoto ya akili, kisha mgombea mwenye akili, uwezo na stahiki zote za kuwa rais bora akasimamishwa kupitia CHAUMA au ADC, bado kuna watu watajitoa akili na kuandamana kumuunga mkono mgombea wa CCM.Siasa zimekuwa za kishabiki zaidi badala ya uhalisia! Jambo ambalo ni hatari kwa nchi, tofauti na nchi za demokrasia ya kweli kama Kenya na Marekani ambapo chama si muhimu kuliko mgombea mwenyewe!

Leo kama nchi ingehitaji kiongozi mwanamke,tukizungumza uwezo na tukiweka uchawa pembeni, Mgombea wa CCM hamfikii hata robo Dr. Asharose migiro au Dr. Mary Nagu kwa kila kitu, uwezo, akili na uongozi bora. Kama isingekuwa uzanzibari na uanamke wake, sidhani kama mgombea wa CCM angekuwepo kwenye rada za uongozi wa nchi hii!

Awamu zote za nyuma hakuna Rais aliyemwona anafaa kuwa hata mkuu wa mkoa? Achilia mbali uwaziri. Leo hii aongoze nchi? Si bure tumeshuhudia awamu mbovu na isiyokubalika kwa watanzania kuwahi kutokea katika historia ya Tanzania.

Tunapaswa kujadili na kuzingatia uimara wa mgombea husika badala ya chama cha kisiasa

Amekuwa Waziri kwa miaka 10

Kabla ya hapo amefanya kazi UN kwa miaka zaidi ya 10

Wanamponda Mama humu hawajawai kupata cheo hata cha ujumbe wa mtaa.

Hawajawai kufanya kazi hata ya u teller wa bank.

Ila wanamkashifu Mama samia
Swali ni alitokea wapi na siyo alipitia wapi,rudia kujibu Steve Nyerere a.k.a tivu ake
 
kabla ya kuwa Rais, Mama Samia Alitokea kwenye umakamu wa rais

Kabla ya kuwa Makamu wa Rais, Mama Samia alitokea kwenye cheo cha U waziri
 
Migiro alikuwa hoi U.K kama ambassador, sidhani kama wamemtoa; kwa sababu awamtaki.

Itakuwa kawaomba inatosha. Yaani ukikutana nae uwezi kuamini kama kashika nyadhifa nyeti za kimataifa na serikali ya Tanzania.

Migiro ni kama mama wa mtaani.. Mtaa wowote ndani ya Tanzania; she is humble (very, very humble); yaani hana majivuno hata chembe.
 
Ninashangaa sana wanaomkazania na kumpa chepuo mgombea urais wa chama cha mapinduzi mpaka inafika wakati unajaribu kuhoji uwezo wa akili zao.Leo hii Tanzania imefikia hatua CCM hata wakimsimamisha mgombea mwenye changamoto ya akili, kisha mgombea mwenye akili, uwezo na stahiki zote za kuwa rais bora akasimamishwa kupitia CHAUMA au ADC, bado kuna watu watajitoa akili na kuandamana kumuunga mkono mgombea wa CCM.

Siasa zimekuwa za kishabiki zaidi badala ya uhalisia! Jambo ambalo ni hatari kwa nchi, tofauti na nchi za demokrasia ya kweli kama Kenya na Marekani ambapo chama si muhimu kuliko mgombea mwenyewe!

Leo kama nchi ingehitaji kiongozi mwanamke,tukizungumza uwezo na tukiweka uchawa pembeni, Mgombea wa CCM hamfikii hata robo Dr. Asharose migiro au Dr. Mary Nagu kwa kila kitu, uwezo, akili na uongozi bora. Kama isingekuwa uzanzibari na uanamke wake, sidhani kama mgombea wa CCM angekuwepo kwenye rada za uongozi wa nchi hii!

Awamu zote za nyuma hakuna Rais aliyemwona anafaa kuwa hata mkuu wa mkoa? Achilia mbali uwaziri. Leo hii aongoze nchi? Si bure tumeshuhudia awamu mbovu na isiyokubalika kwa watanzania kuwahi kutokea katika historia ya Tanzania.

Tunapaswa kujadili na kuzingatia uimara wa mgombea husika badala ya chama cha kisiasa
...'Bado kuna watu watajitoa akili'...
Hao wenye kujitoa akili ndiyo machawa wenyewe, ama walamba viatu.

Uchawa kwa Ccm imekuwa ni ajira, ni kada!

Na katika kila tukio huwa wamejipanga kipandikizi, bila kujali wadhifa ama cheo, elimu na wala haiba ya mtu.

Mtu yeyote kwangu mimi, awe Waziri ama kiongozi yeyote, katika hotuba yake nikimsikia tu kila baada ya maneno mawili anachomekea 'mama katoa ama kaleta fedha', 'nani kama mama', 'mama anaupiga mwingi' bila kiunganishi cha maana chenye mantiki kusapoti maneno hayo nk nk, kichwani mwangu humtoa maana moja kwa moja na kumdharau sana mtu huyo.

Nchi imekuwa na watu aina ya zombie wasioweza kuhoji chochote wanapojazwa taka taka za kila aina vichwani mwao na huzimeza bila ya tathimini na kuzichambua, hii inakera sana kwa kweli!

Ninawashukuru Chadema kwa kpumpitisha TAL kwa kishindo, mtu ambaye anaweza akachallenge siasa za kipuuzi za nchi hii.
 
Labda migor lakini siyo Nagu. Labda kwa vile nawfahamu wote waili kwa mude mrefu. Nilimfahamu Migiro tukiwa bado waajiriwa nwa UDSM tungali vijana na pia nilifahamu Nagu akiwa meneja wa kiwanda cha Mabegi Morogoro pia tungali vijana. Lakini kwa uwezo wa kuongoza independenly, bado nampa Migiro kuliko Nagu.
 
Leo kama nchi ingehitaji kiongozi mwanamke,tukizungumza uwezo na tukiweka uchawa pembeni, Mgombea wa CCM hamfikii hata robo Dr. Asharose migiro au Dr. Mary Nagu kwa kila kitu, uwezo, akili na uongozi bora. Kama isingekuwa uzanzibari na uanamke wake, sidhani kama mgombea wa CCM angekuwepo kwenye rada za uongozi wa nchi hii!
Nimeona niseme. Huenda, kama ulivyosema, hawafikii hao uliowataja kwa elimu kwani wao ni PHD holders, lakini uongozi hapa kwetu haupatikani kwa kuwa na PHD tu, bali kuna na vigezo vingine. Nikukumbshe tu hapa Tanzani miongoni mwa marais sita waliotawala, ni mmoj tu alikuwa na PHD. Jikumbushe.
Mama, nikukumbudshe, amepata nafasi hiyo kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri na haina uhusiano na Uzanzibari.
Awamu zote za nyuma hakuna Rais aliyemwona anafaa kuwa hata mkuu wa mkoa? Achilia mbali uwaziri. Leo hii aongoze nchi? Si bure tumeshuhudia awamu mbovu na isiyokubalika kwa watanzania kuwahi kutokea katika historia ya Tanzania.
Naona umeandika kijinga (ignorantly). Sikulaumu kwa kutojua kwani wewe ni mvivu wa kufikiri. Sasa nikukumbushe tu kwamba huyu mama alishawahi kuwa waziri katika JMT na SMZ. Mara ya mwisho alikuwa waziri katika ofisi ya makamu wa rais wa JMT.

Ama kuhusu kuwa hii ni awamu mbovu, huenda hujui tafsiri ya mbovu. Nakutonya tu kwamba huyu ndiye aliyemalizia ujenzi wa SGR na daraja lile la Kigongo - Busisi. Huwa unajivunia kwayo. Sitaki niseme mengi kwenye hili kwani kila kitu kinaonekana.
Tunapaswa kujadili na kuzingatia uimara wa mgombea husika badala ya chama cha kisiasa
Ni kweli unayoyasema, sasa tujadili kwa haki bila upendeleo wala chuki.
 
Shida ni elimu yetu na quality yake.

Kwanini udhani mtu mwenye PhD hasa ya social science anaulewa mpana kuliko mwenye bachelor.

Huu ni ushamba tu, hasa kwenye siasa.

Having a PhD doesn’t doesn’t mean shit, in politics.

Utaahira wetu

You study 18-24 modules as an undergraduate.

You study 6-7 modules in post graduate (nyingi umesoma as undergraduate) unless umefika hapo kwa degree tofauti na undergraduate ndio utakutana na new topics,

Unafanya thesis at PhD.

Like what’s so special after a bachelor especially kwa social science and business studies.

PhD is nothing special ni kupoteza muda tu if you ask, only useful kwa academic ambao wanataka kufundisha. For a politician ni ujinga mtupu.
 
Ninashangaa sana wanaomkazania na kumpa chepuo mgombea urais wa chama cha mapinduzi mpaka inafika wakati unajaribu kuhoji uwezo wa akili zao.Leo hii Tanzania imefikia hatua CCM hata wakimsimamisha mgombea mwenye changamoto ya akili, kisha mgombea mwenye akili, uwezo na stahiki zote za kuwa rais bora akasimamishwa kupitia CHAUMA au ADC, bado kuna watu watajitoa akili na kuandamana kumuunga mkono mgombea wa CCM.

Siasa zimekuwa za kishabiki zaidi badala ya uhalisia! Jambo ambalo ni hatari kwa nchi, tofauti na nchi za demokrasia ya kweli kama Kenya na Marekani ambapo chama si muhimu kuliko mgombea mwenyewe!

Leo kama nchi ingehitaji kiongozi mwanamke,tukizungumza uwezo na tukiweka uchawa pembeni, Mgombea wa CCM hamfikii hata robo Dr. Asharose migiro au Dr. Mary Nagu kwa kila kitu, uwezo, akili na uongozi bora. Kama isingekuwa uzanzibari na uanamke wake, sidhani kama mgombea wa CCM angekuwepo kwenye rada za uongozi wa nchi hii!

Awamu zote za nyuma hakuna Rais aliyemwona anafaa kuwa hata mkuu wa mkoa? Achilia mbali uwaziri. Leo hii aongoze nchi? Si bure tumeshuhudia awamu mbovu na isiyokubalika kwa watanzania kuwahi kutokea katika historia ya Tanzania.

Tunapaswa kujadili na kuzingatia uimara wa mgombea husika badala ya chama cha kisiasa
Acha chuki zako, Dr. Samia Suluhu Hassan ana akili kubwa sana!
Eti Marais wa nyuma hawakumpa nafasi!
Rais Samia amepata kushika nafasi nyingi zikiwemo Uwaziri.Wewe ndiye ulikuwa ukimteua?!
 
Kwanini udhani mtu mwenye PhD hasa ya social science anaulewa mpana kuliko mwenye bachelor.
Mkuu sijadhani; nilikuwa nachangia uzi uliojenga hoja ya kwamba kuna degree holders ambao wangepaswa kuwa marais tofauti na mama, hivyo mama yeye hakustahiki ila kaupata urais kwa Uzanzibari wake.

Sijajadili ubora wa elimu.
 
Huwezi kukuta mahala popote naandika ujinga huo wa maneno unayotaka kuniwekea.

I dare you tafuta quote yoyote ya ubaguzi kutoka kwangu iwe ya udini, Kabila, sexism au ubaguzi wa nchi jirani.

Keep your nonsense to yourself.
 
Ninashangaa sana wanaomkazania na kumpa chepuo mgombea urais wa chama cha mapinduzi mpaka inafika wakati unajaribu kuhoji uwezo wa akili zao.Leo hii Tanzania imefikia hatua CCM hata wakimsimamisha mgombea mwenye changamoto ya akili, kisha mgombea mwenye akili, uwezo na stahiki zote za kuwa rais bora akasimamishwa kupitia CHAUMA au ADC, bado kuna watu watajitoa akili na kuandamana kumuunga mkono mgombea wa CCM.

Siasa zimekuwa za kishabiki zaidi badala ya uhalisia! Jambo ambalo ni hatari kwa nchi, tofauti na nchi za demokrasia ya kweli kama Kenya na Marekani ambapo chama si muhimu kuliko mgombea mwenyewe!

Leo kama nchi ingehitaji kiongozi mwanamke,tukizungumza uwezo na tukiweka uchawa pembeni, Mgombea wa CCM hamfikii hata robo Dr. Asharose migiro au Dr. Mary Nagu kwa kila kitu, uwezo, akili na uongozi bora. Kama isingekuwa uzanzibari na uanamke wake, sidhani kama mgombea wa CCM angekuwepo kwenye rada za uongozi wa nchi hii!

Awamu zote za nyuma hakuna Rais aliyemwona anafaa kuwa hata mkuu wa mkoa? Achilia mbali uwaziri. Leo hii aongoze nchi? Si bure tumeshuhudia awamu mbovu na isiyokubalika kwa watanzania kuwahi kutokea katika historia ya Tanzania.

Tunapaswa kujadili na kuzingatia uimara wa mgombea husika badala ya chama cha kisiasa
Huyo mary nagu amefanya kitu gani cha maana kwenye nchi hii au Asha rose migiro japo alikuwa naibu katibu mkuu umoja wa mataifa amefanya nini cha maana?
 
Back
Top Bottom