Dr. Bashiru, CCM ilipasuka 2015, hutaweza kuiunganisha kwa kukumbatia wasaliti

Dr. Bashiru, CCM ilipasuka 2015, hutaweza kuiunganisha kwa kukumbatia wasaliti

Mkuu Johnthebaptist fafanua vizuri hiyo kanuni naona inaleta figure kubwa nadhani hiyo figure ni ya hela..!
Vipi zote hizo wanachangia nini hao ndugu..!!!
Hahahaaa....... Wanachangia chama mkuu!
 
Katika mazingira ya sasa Chadema wamepoteza ushawishi kwa wananchi kwa sababu kile kilichowapa umaarufu ndio hicho kinachompa umaarufu Rais Magufuli namaanisha vita dhidi ya rushwa na ufisadi.

Tena Dr Magufuli ameenda mbali zaidi kwa kuweka ulinzi wa rasilimali zetu na kuwapa mrejesho wa keki ya taifa wananchi wanyonge!
Kama ni hivyo kinachomfanya kila akiona jukwaa la Chadema ahisi moshi wa Ruangwa unamjia ni nini ? aache kutumia polisi aone moto
 
Hahahaaa....... Wanachangia chama mkuu!
Asante kwa ufafanuzi Mkuu...

Sasa wawaache huru wanaoamua kubwaga Manyanga, we unachangia 30m..! hata jengo la HQ la chama hulioni miaka nenda rudi.. kukosea ni Mara moja wenye akili wameshtuka..!

MTU akiamua kurudi wamwache awe huru kuamua bila kuweka visingizio vya oh Mara kanunuliwa..!!!
 
Bado sijajua hasa mwaka ambao Bashiru Ally aliingia kwenye siasa , lakini baada ya kumfuatilia kwa undani nimegundua kwamba huyu ni miongoni mwa WANASIASA WACHANGA SANA ambaye hana uwezo wa kuongoza CCM ya sasa , ameshindwa kujua kama ile CCM iliyofufuliwa na Kinana imekufa na kusambaratika kabisa.

Mwaka 2014 kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ndipo hasa kifo cha CCM kilipoasisisiwa, ukiua chama katika ngazi ya matawi ufahamu kwamba unaua chama chote hadi juu. Kwa mfano, Mtaa wa Keko Magurumbasi A kulikuwa na kiongozi wa CCM aliyeitwa Fundi , huyu aliondolewa kwenye kinyang'anyiro cha serikali za mitaa kwa mizengwe, akahamia CHADEMA.

Hakugombea chochote lakini alitumika kusambaratisha kabisa CCM Kata ya Keko, ambapo katika mitaa mitano CCM iliambulia mmoja tu tena kwa wizi. Nafahamu kwamba lengo la Bashiru Ally kuagiza marudio ya uchaguzi ni kujaribu kuondoa makovu yaliyosababishwa na uonevu lakini amesahau kwamba CCM Makao Makuu ndio chanzo cha uchafu wote huu wa kuondoa michakato halali ya kura za maoni na kukumbatia Wasaliti " walionunuliwa " ama kusaliti kwa hiyari.

CCM makao makuu imesimamia kikamilifu uvunjwaji wa katiba ya chama chao ya kupiga marufuku kura za maoni ili kuwapitisha tena Wasaliti ikiwa ni masharti ya mikataba ya ununuzi, ambapo Mwenyekiti wao Mh Magufuli alichukua nafasi ya Yesu na kuonekana akiwaambia wahamiaji kwamba " Njooni kwangu msumbukao na mizigo ya dhambi nami nitawapumzisha " Astaghafillulah ! wala hakuna mtu yeyote ndani ya ccm aliyelikemea hili , walishangilia na kupiga makofi mengi .

Sasa leo wanaCCM halali waliopigania chama chao kikamilifu wakati Bashiru akiwa UDSM, wakati wanaCCCM wanapambana kuinua chama wakishirikiana na Migiro na Kinana Bashiru hakuwepo wala wasaliti wake anaotaka kuwabeba hawakuwepo.

Nakuhakikishia Bashiru kwamba ukitaka kuimalizia CCM endelea kuwabeba wasaliti wako.

Itaendelea ...
Ahahahah! Yaani kama vile Nugaz awe mtaalam wa kuichambua Simba!
 
Chadema ya Mashinji ina jukwaa?!......mnazidiwa hata na yule mzushi wa ujiji!
Tangu Slaa aondoke kimyaaaaa...!!!

Walikosea sana yule alikuwa lulu lakini ndo hivyo hawakuitumia vizuri..
wakamweka pembeni, sasa yuko nyumbani na miaka ya mbeleni Slaa akiamua kugombea Urais ndani ya wataanza kumtamani tena..!!
 
Pamoja na uchanga wake ameimega Chadema kwa kuchukua wabunge zaidi ya 10 na madiwani zaidi ya 100, amejiwekea historia ndani ya chama!
Amewachukuaje? Kwa mapenzi yao au kwa ushawishi wa fedha? Polepole mwenyewe huyo huyo aliwahi kukuri kwa kinywa chake na rekodi zipo kuwa uchaguzi ukiwa wa huru na haki hakika CCM ijiandae kuachia madaraka.

Ukitaka kulijua hilo juzi meko alizushiwa umauti cha ajabu watu walijawa na furaha isiyokuwa na kifani. Watu waliokuwa wanafurahia ni wengi kuliko waliokuwa wanahuzunika. Hujiulizi tu?

Ninyi kinachowabeba ni jeshi la polisi na tume. Vinginevyo sasa hivi mngekuwa TLP!
 
Tangu Slaa aondoke kimyaaaaa...!!!

Walikosea sana yule alikuwa lulu lakini ndo hivyo hawakuitumia vizuri..
wakamweka pembeni, sasa yuko nyumbani na miaka ya mbeleni Slaa akiamua kugombea Urais ndani ya wataanza kumtamani tena..!!
FB_IMG_1570952637609.jpg

unataka na sisi tushike bunduki ?
 
Amewachukuaje? Kwa mapenzi yao au kwa ushawishi wa fedha? Polepole mwenyewe huyo huyo aliwahi kukuri kwa kinywa chake na rekodi zipo kuwa uchaguzi ukiwa wa huru na haki hakika CCM ijiandae kuachia madaraka.

Ukitaka kulijua hilo juzi meko alizushiwa umauti cha ajabu watu walijawa na furaha isiyokuwa na kifani. Watu waliokuwa wanafurahia ni wengi kuliko waliokuwa wanahuzunika. Hujiulizi tu?

Ninyi kinachowabeba ni jeshi la polisi na tume. Vinginevyo sasa hivi mngekuwa TLP!
Si kwamba hajui bali anajisahaulisha ili aendelee kulipwa elfu 7
 
Katika mazingira ya sasa Chadema wamepoteza ushawishi kwa wananchi kwa sababu kile kilichowapa umaarufu ndio hicho kinachompa umaarufu Rais Magufuli namaanisha vita dhidi ya rushwa na ufisadi.

Tena Dr Magufuli ameenda mbali zaidi kwa kuweka ulinzi wa rasilimali zetu na kuwapa mrejesho wa keki ya taifa wananchi wanyonge!
Ni fisadi gani yuko ndani mpaka sasa? Huna tofauti na msiba
 
Back
Top Bottom