Uchaguzi 2020 Dr. Bashiru: Kama Membe anasema tatizo ni Urais agombee kwa chama chochote tukutane uwanjani

Habari Jf!
Kuna nini kwani kimetokea mbona kila kona nasikia Membe Membe???

Inamaana ss CHADEMA mshampata shujaa wenu naye ni Benard Membe ,maana kila nikipita katika kurasa za Jf naona jina la Membe limepambwa vizuri kwa mbwembwe nyingi na akibatizwa majina makubwa kama mwanaharakati,mwanadiplomasia wengine washampa cheo cha ukamanda.

Ila mm nawaambia wapinzani neno moja tu kwamba Membe hafai hata kwa kurumangia,nimalizie tu na kwa kusema kidagaa kilichomponza Ndobe ndio kitakachomponza kambare.

Wapo wanaongoja tamko rasmi la Membe kwamba atafanya nn baada ya kufukuzwa CCM ,wengine washaanza kumtamani Benard Membe ili kujihimarisha kuelekea uchaguzi mkuu .

Fanyeni mipango yenu yote ila CCM itatawala mpaka miaka 100 ijayo hakuna wakuiangusha na waakikishia,upinzani ulishakufa .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…