Mimi sijui nani kamdanganya, Kati ya watu wanaocheza karata zao vibaya ni Membe, kwanza hawezi kumshinda Magufuli,kama Magufuli alimshinda akiwa hana connections 2015 leo utaweza?,achana na sifa za kudanganywa eti wewe ni shushu mara ohh ni mwana diplomasia nguli watu wanakuingiza chaka mbaya, Tz kwa sasa kuna millions ya wana diplomasia tena wako kitaa tu hawana kazi, jifunze unyenyekevu na kuwa mvumilivu na utafaulu katika ndoto yako ya urais, kikwete alivumilia baada ya kushindwa na mkapa ,akawa mpole wakati ukafika akafanikisha , angekuwa jeuri asingeweza kutimiza ndoto yake, bado una nafasi kubwa kwa miaka ijayo.
Upinzani, mikikimikiki ya upinzani membe hutaweza, upinzani bongo unataka moyo,yaani unatakiwa uwe tayari , na uwe ngangari vya kutosha, yaani ulivyo mayai mayai itakuwa ngumu kwako , sikukatishi tamaa lakini huu ndo ukweli.