Dr. Cheni aeleza sababu za kutojihusisha tena na filamu nchini

Dr. Cheni aeleza sababu za kutojihusisha tena na filamu nchini

YAANI WATU WOTE WANGENISIKILIZA TUNGEANZA KAMPENI YA MAKUSUDI YA KUWAANGAMIZA WASANII WOTE WALIOCHAGUA CCM KWA KUSUSIA KILA WANACHOFANYA. NDIYO MAANA NDOMO SIMPENDI KABISA INGAWA ANATOKA KASULU KWETU.
Ndomo mpende tu yeye pale alikua anafanya bashara ndio maana hukumona akizunguka sijui mama ongea namwao..yeye alipiga show akasepa zake
 
wasanii wa bongo movie wana organization yao inaitwa Tollywood ina kaz gani? Me kwa mtazamo wang ni wao kutokua organized ndo maana movie zna zagaa mtaani wakae chini wajipange wa angalie mfumo sahihi wa kusambaza kaz zao
Wanaibiana chupi ndio maana tollywood chaliii
 
kinachoiangamiza Bongo Muvi sio suala la mauzo pekee...wajiulize mbona hata umaarufu wa Wasanii wa Muvi umekwisha kwa muda mrefu sasa...Hakuna wasanii wapya wanaoibuka, zaidi ya kubaki na wale wale wa tangu miaka zaidi ya kumi iliyopita ukilinganisha na wenzao wa Bongo flavour, Majina ni yale yale JB, Ray, Aunty, Wolper, Rose Ndauka, Uwoya n.k.

Na kama hizo kazi zingekuwa zinasambaa kwa njia ya uharamia kama anavyojaribu 'kutujaza' Dr Cheni basi bado tungeona Wasanii wengi wapya wanaibuka na umaarufu wa Bongo muvi ungebakia kama sio kuongezeka...labda ambacho mngekosa ni pesa tu.

Hata Wasanii wa Bongo flavour hawauzi CD, lakini kwa nyimbo zao kuchezwa hovyo na kuchomwa hovyo mitaani ndio tunashuhudia kuibuka kwa Wasanii wapya kila siku.

Kilichoiua bongo Muvi ni ubinafsi ulioendekezwa na hao hao wanaojiita 'Waanzilishi' wa Bongo muvi....wao baada tu ya kuona Watanzania wamewapokea vizuri wao wakajifungia kwenye chumba chao kama Wasanii na kuamini kwamba sasa ndio wakati wa kuchuma mihela..walisahau kabisa kwamba sanaa ya filamu ni matokeo ya team work, kwa maana ya Wapiga picha, Waandishi, Waongozaji n.k ndio maana mlishuhudia kina Ray wakijipa majukumu yote ya kuandaa filamu, muandishi yeye, Cameraman yeye, Muigizaji yeye, na wenzake walifuata mkumbo huo huo.....Wao waliamini kuwa Wasanii wangeweza kusafiri kivyao na kufaidi mihela ya Watanzania milele.

Wana kazi kubwa ya kurudisha imani ya Watanzania tena kwani sio kazi rahisi sana...kuna usemi maarufu kuwa 'bahati huwa haiji mara mbili' ila upo uwezekano wa kurudi tena iwapo tu watakaa chini na kutaka kujifunza Filamu ni nini..

.....Sanaa ya Filamu/burudani huwa haifi, bali husinzia au kuwa kwenye coma hata kwa miaka mia moja iwapo kutakosekana ubunifu na uelewa, mpaka hapo watakapojitokeza watu sahihi wa kuirudishia uhai.
Umenena vyema
 
Bongo muvi tulieni, tena kaeni kimya kabisaaaaaaa.

Mlishachagua maslahi yenu Oct, 25--2015
Safi sana....watulieeeee kama wanachinjwa

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Tumia akili angalau kidogo basii!!!!
Serikali iliyoko madarakani haipendwi.
Koment zinatoa mwanga huo.
Wachangiaji humu hamna lolote la kushauri, mmekwama kama walivyokwama Wasanii hao...kubwa mnalofanya ni kukimbilia siasa...na hizo ndio shahada za Watanzania, mnapoona kichwani hakuna ufumbuzi mnageukia siasa.

Yaani kwa kuwa tu siasa inaruhusu kuongea chochote basi ndio Watanzania tumeamua kujikita huko kama njia ya mkato kwa kila jambo, utakuta Watu mitaani mnageuza mifereji ya maji kuwa ndio sehemu za kutupa uchafu mnaozalisha majumbani, mkiulizwa manakimbilia siasa...kana kwamba mkiugua kipindipindu siasa itakuja mbio na kuwanusuru.
 
Ndo tuseme basi hutotoa filamu tena maana hadi serikali ije iweke mambo sawa sio leo wala kesho
 
Hebu tuache mboyoyo...kuna uhusiano gani kati ya kudorora soko na kushiriki kampeni za chama?

Basi na mhusianishe mafanikio ya Diamond na kampeni...maana naye si alishiriki?

Nadhani mmekosa tu cha kushauri na sasa mnatafuta njia ya mkato.

Hao Wasanii waliounga mkono upinzani ni wangapi sasa wanakula matunda ya mafanikio kutokana na kufanya hivyo?
foaming
 
Wachangiaji humu hamna lolote la kushauri, mmekwama kama walivyokwama Wasanii hao...kubwa mnalofanya ni kukimbilia siasa...na hizo ndio shahada za Watanzania, mnapoona kichwani hakuna ufumbuzi mnageukia siasa.

Yaani kwa kuwa tu siasa inaruhusu kuongea chochote basi ndio Watanzania tumeamua kujikita huko kama njia ya mkato kwa kila jambo, utakuta Watu mitaani mnageuza mifereji ya maji kuwa ndio sehemu za kutupa uchafu mnaozalisha majumbani, mkiulizwa manakimbilia siasa...kana kwamba mkiugua kipindipindu siasa itakuja mbio na kuwanusuru.
foaming
 
Back
Top Bottom