Kigoma Region Tanzania
JF-Expert Member
- May 25, 2021
- 230
- 611
Raia 2643 Kutoka kongo-DRC wameingia mkoni kwetu Kigoma kuomba hifadhi kutokana na machafuko ya vita yanayoendelea nchini kwao baina ya jeshi la nchi hiyo na waasi wa M23
#VisangavyaCongo
1-Msafiri Jampiele
-Kule kongo, hali kule ilikuwa tete sana, maana tangu mimi nizaliwe sijawahi kuona matendo kama yale ambayo tulikuwa tunafanyiwa sisi.
Maana watu walikuwa wanatoka porini, watu tusiowajua, kwenye usiku tu mnalala watu wanaingia, bahati mbaya unakuta wazazi wanafariki, bahati mbaya watoto wanafariki, yani wanauwa watu pasipokua na hatia.
Yaani vile vikapeleka vifo sana ndani ya nchi ya kongo, ile sehemu tuliyokuwa tunaikaa nchi ya Goma, vifo vikakua sana sana sana, watu wakaona hapana, tukizidi kukaa hapa au kuishi hapa, tutapata matatizo sana. Watu wakaamua hapana wacha tukimbilie Tanzania, ili angalau wenzetu wataweza kutupokea ili tupate makao mazuri.
Mimi nimeshuhudia rafiki yangu akiuwawa mbele ya macho yangu, ambaye tulikua naye, saa nne za usiku, maana tulikua tumetoka kuangalia TV sehemu fulani, kuangalia kufuatilia mambo ya mpira haya, muda wa kurudi ndo tukaona watu wanatupiga Taa usoni, wakatushika pale, vizuri mimi nikakimbia.
Nilipokimbia nikafichama sehemu fulani, yule ndugu yangu nikashuhudia jinsi wanavyomfanya pale, wanamfunga kwenye uso, wakampiga mapanga na mimi mwenyewe nikaona, nikashuhudia macho yangu nikifichama, wala hawakuniona, lakini nikashukuru MUNGU maana nikafika nyumbani salama.
#VisangavyaCongo
2-Stanley Goliati
Familia yangu, yani shikupata muda ya kufika nyumbani, baada ya kuambiwa na rafiki yangu kua, yaani ni mtoto ya rafiki yake ya bhabha ni mwanajeshi wa M-vingttrois, akaniambia kaka mzee kashakamatwa, mzee alishakamatwa,
Yaani baba yangu na mama yangu walikamatwa wakawafunga kamba kwenye kimti wakachukua Bidoo ya vide, unajuaa Bidoo, ambalo halina maji wakaweka juu wakachukua kibiriti wakachoma, wakafia hapo kwenye mti.
Mimi nikapigiwa simu niko shamba yaani sikupata na muda wa kusema kwamba niende tena nyumbani, ahh nilipatwa kwanza na uwoga, na hata bibi yangu, mke wangu na watoto sijui kwenye wako, kwa hiyo niliokoa nafsi yangu tu ndo nikaja huku hivi.