DR Congo yaishutumu Rwanda kuisapoti M23 baada ya kutokea mashambulizi makali

DR Congo yaishutumu Rwanda kuisapoti M23 baada ya kutokea mashambulizi makali

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeishutumu Rwanda kwa kukisaidia Kikundi cha M23 baada ya Jeshi la DR Congo kushambuliana na kikundi hicho katika mashambulizi makali Mashariki mwa Taifa hilo yaliyotokea Mei 26, 2022.

Mashambulizi hayo yaliyotokea Kaskazini mwa Mji wa Kivu karibu na mpakani. Rwanda imekanusha tuhuma hizo ikiwa pia siyo mara yao ya kwanza kushutumiwa na kisha kukanisha kuhusika.

"Waasi wa M23 wanaungwa mkono na kupata msaada kutoka Rwanda," anasema Msemaji wa Serikali ya DRC, Patrick Muyaya.

Pia soma: Mapambano makali kati ya jeshi la DRC dhidi ya kundi la M23 yaanza tena

Chanzo: Daily Monitor
 
Na wao wangetengeneza kakikundi cha kwenda Rwanda

Sikilizia now Rwanda yuko msumbiji jamaa anatabia ya kutengeneza waasi ambao wako well trained hivo intelligence yetu ikae makini sana upande wa mtwara na msumbiji maana tunaweza kuachiwa msala ambao hatutousahau na silaha zikawa zinapelekwa kwa walinda amani wa rwanda huku nyingine wanapewa waasi watusulubu
 
Wanaijua Tz hao M23,
Unakumbuka kipindi kile MONUSCO Walipojumuisha jeshi la JWTZ,Kikundi kilipotezana..

Wanamtest Mama,soon atajumuisha,Maana mama na jk lao moja,pk akae mkao mzuri,JWEE Si wa mchezomchezi...
 
Yupo msumbiji akipigana kwa niaba ya ufaransa,maana marekani na uingereza wamempelekea wanamgambo asichimbe futa Cabo Delgado...dizaini ziara ya maza ufaransa miongoni mwake ilikua tz kuombwa kuungana na rwanda kule msumbiji
 
Wanaijua Tz hao M23,
Unakumbuka kipindi kile MONUSCO Walipojumuisha jeshi la JWTZ,Kikundi kilipotezana..

Wanamtest Mama,soon atajumuisha,Maana mama na jk lao moja,pk akae mkao mzuri,JWEE Si wa mchezomchezi...
Wiki 2 zilizopita Kagame alituma ujumbe maalumu kupitia waziri wake wa mambo ya nje ikulu ya magogoni kukutana na Rais Samia nadhani agenda mojawapo ilikua ni hilo suala la M23.
 
Rwanda ni kanchi kadogo sawa na mkoa wa Dodoma, lakini kana watu 12m+, eastern Congo kuna banyamulenge wengi sana (watutsi waliolowea) ambao hutamani kuimega congo ili iongeze ardhi kwa Rwanda. kuna siku eastern Congo itakuja kujitenga na kuwa part of Rwanda kama ilivyo kwa majimbo yaliyo mpakani mwa urusi kujimega toka ukraine. siku zoote hata iweje, hiyo ni sera ya Rwanda hawatakuja kuiacha hadi wafanikiwe kwasababu ina maslahi mapana kwa nchi. Dawa yao ni kupeleka JWTZ, na samia aachane na kagame, tuwe karibu na burundi na wakati huohuo m7 anaendelea kumbana paka abaki peke yake.

sasaivi dr congo imejiunga na East AFrica community, hivyo DR Congo wakiwa pamoja sana na Burundi, Tanzania, Kenya na kwa mbaali Uganda, Rwanda atabaki peke yake na ataona hamna namna ila kuwa na adabu tu. Tanzania tungekuwa ni nchi kubwa kidunia kama zilivyo hizo zinazopigana huko, tulikuwa na sababu ya msingi sana kwenda kuweka base yetu Congo, na Congo wangekubali kwasababu wanatukubali sana. sema ndio hivyo, nchi yenyewe hata bajeti ya jeshi ni ya 3rd world country.
 
Hata mi naona kama akili zimeanza kuwarudia kwa hatua hii walio chukua
Hahah Congo walijitoa ufahamu wakarusha makombora mawili ndani ya mipaka ya Rwanda,nao wakarudishiwa makombora 20 ndani ya Goma halafu wakasema hawajui makombora yalikotokea.

Imebidi haraka haraka Congo itume kamati ya mambo Yao ya usalama kwenda Kigali kujadili Nini kilichotokea.Afu Muda huo PK Wala hayuko Rwanda Yuko huko Davis kwny mkutano na wenye dunia yao(World Economic Forum).
 
Wiki 2 zilizopita Kagame alituma ujumbe maalumu kupitia waziri wake wa mambo ya nje ikulu ya magogoni kukutana na Rais Samia nadhani agenda mojawapo ilikua ni hilo suala la M23.
Kagame alituma ujumbe wake kuja kumkaribisha mama huko Kigali kwny CHOGM,na Waziri huyo wa mambo ya Nje ameenda pia Nchi nyingine kukaribisha marais wa nchi hizo.
 
Yaani linchi lote lile linasumbuliwa na Rwanda kila siku?!!! Waungane na Uganda na Burundi wamtwange Rwanda mpaka awe majivu, shenzi zake huyu PK!
 
Hahah Congo walijitoa ufahamu wakarusha makombora mawili ndani ya mipaka ya Rwanda,nao wakarudishiwa makombora 20 ndani ya Goma halafu wakasema hawajui makombora yalikotokea.

Imebidi haraka haraka Congo itume kamati ya mambo Yao ya usalama kwenda Kigali kujadili Nini kilichotokea.Afu Muda huo PK Wala hayuko Rwanda Yuko huko Davis kwny mkutano na wenye dunia yao(World Economic Forum).
Kwann Rwanda wamefanya utoto namna hiyo..Foristance makombora hayo wangehis yametoka tanzania au Kenya je wangepiga hiyo mikombora 20 kuja bongo pasi na kujaribu kujua whats wrong??
 
Rwanda haijaanza leo kushutumiwa na muda mwengine mpaka wanajeshi wake wanaonekana huko katika genge la waasi, Nchi zote hizi zipo katika Umoja wa Afrika Mashariki, je Wakuu wa Umoja huo wamechukua hatua gani au ni umoja usio na maana?
 
Back
Top Bottom