, anatarajiwa kufikishwa mahakamani
wakati wowote kutoka sasa. Anaandika
Pendo Omary…(endelea).
Dk. Dau anatuhumiwa kuingiza NSSF hasara
ya mabilioni ya shilingi, kutokana mikataba
ya kinyonyaji. Amekuwa katika shirika hilo
kwa miaka 15.
Taarifa kutoka serikalini na taasisi nyingine
zinazoshughulikia uchunguzi zinasema, Dk.
Dau ambaye aliong’olewa NSSF 15 Februari
mwaka huu, atafikishwa kwa mahakamani,
kujibu tuhuma za ufisadi zilizoibuliwa ndani
ya shirika hilo.
Tuhuma nyingine ni matumizi mabaya ya
madaraka, uzembe na ukiukwaji wa taratibu
katika miradi ya uwekezaji na vitega uchumi
mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Miongoni mwa miradi hiyo, ni ujenzi wa
daraja la Kigamboni; hoteli ya kitalii jijini
Mwanza, mradi wa ujenzi wa majengo katika
mji mpya wa Kigamboni, uwekezaji kwenye
jengo la biashara la Mzizima na mgodi wa
mkaa wa mawe wa Kiwira, mkoani Mbeya