Tetesi: Dr. Dau kufikishwa mahakamani. Yasemekana kahojiwa TAKUKURU

Tetesi: Dr. Dau kufikishwa mahakamani. Yasemekana kahojiwa TAKUKURU

Status
Not open for further replies.
huyu anatakiwaq atandikwe lile kosa la kusafisha hela kwanza ili akae ndani tukiendelea kufichua madudu manake alifanya kufuru.
 
Kama maghufuli hatajitumbuwa kwa nyumba za serikali MV Dar es salaam na meli ya samaki nitamuona ni mnafiki sana msumeno ukate kote sio kuchagua na kama Mkapa na KIkwete sitawaona basi ajenge nchi kwa kutuletea miradi sitahiki sio sifa

Jitahidi kwanza ufahamu utaratibu wa mambo ulivyo, kama hujui kuuliza si vibaya.Kutoa 'conclusion' kwa kitu usichokifahamu wala kuwa na taarifa zake za kina ni uhayawani
 
Watu wamemuamini kabisa mleta uzi! watanzania ni mizigo kwakweli!
 
Huyo si alishapewa ubalozi? Bado hajapangiwa kituo na kuondoka?
 
hayo ndo majipu alisema kuyatumbua inabidi utumie akiri ya ziada.Subiri evidence nyingi ambazo zitapelekea hiyo kitu kutokea
Kumtenganisha Muhongo, chenge na escrow itakuwa ni uonevu kwa watakao tumbuliwa
 
Huyo si alishapewa ubalozi? Bado hajapangiwa kituo na kuondoka?
Jipu lake lilikuwa kubwa, ilihitaji hekima kulitumbua, amepata bahati ya kupigwa ganzi (ubalozi) ndio anatumbuliwa sasa.
 
Zito shoga huyu hana jipya.
VIVA AWAMU YA TANO....VIVA MAGUFULI....GOD BLESS YOU OUR BELOVE MAGUFULI!
 
Kweeeeeeeeeeli siamini hiki ninachokiona kwa dau! Hivi ukiwa mwizi kwanini ujifanye mfia Dini????? Haya tuoneshe aya sasa inayokuruhusu kukwapua hela za watz kama ulivyohodari wa kuquote!!!! Katika hili unaweza sema majambazi wana nafuuuu! Hivi pesa zote hizo zingeokoa maisha ya watz wangapi mahospitalini! Shaaaame on you! Nchi yetu inatia huruma jmn! Daaaa! Na bahati mbaya wadanganyika tumeumbiwa kuchukulia issue poa tu! Nimekasirika sana!

Nakukumbusha tu kuwa hukumu ni kazi ya mahakimu na majaji hapa duniani na kesho huko akhera ni yake Sub'hana Wataala.Tuwe na subira, kama atakuwa na kesi ya kujibu atapelekwa mahakani na kama huko atapatikana na kosa atatiwa hatiani. Tuchangie sawa, tukihukumu basi tujihukumu na sisi wenyewe kwani nafsi zetu zafahamu pasi shaka maasi mangapi tuliyoyatenda kuwadhulumu watanzania wengine. Tukijitoa hadharani kusema mabaya yetu itakuwa bora sana kwani itakuwa kweli tupu na pia tutakuwa tumeanzisha mwanzo mpya wa kusafisha nafsi zetu. Kabla hatujahukumu pasipo kufahamu ukweli kama tulivyozoea tuanze kujihukumu kwani ukweli wetu tunao mioyoni mwetu.
 
Yaani wezi wote wanaohujumu uchumi wa nchi hii ni wanaCCM....bila kuwaondoa Magamba madarakani, tusitarajie kufikia uchumi wa kati.
 
Haki zote zimehifadhiwa

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
Magufuli atakapoambiwa pesa zote hizo zilitumika kufanya kampeni iliyomweka madarakani atatulia tu. Kwa sasa bado wanamlia timing atawekwa sawa tu.
 
Meli ya 1979 kwa 7.9bn halafu unakaa kimya .....lazma nae atumbuliwe tu mda ukifika

Kwani wewe bei za meli unazifahamu? Hebu tuambie basi meli ile ina thamani gani na alitakiwa kununua meli ya mwaka gani kwa bei gani? Tusaidie muungwana wasije kusema unafanya majungu
 
Hatimaye DK. Ramadhan Dau, aliyekuwa mkurugenzi wa Shirila la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.

Dk. Dau anatuhumiwa kuingiza NSSF hasara ya mabilioni ya shilingi, kutokana mikataba ya kinyonyaji. Amekuwa katika shirika hilo kwa miaka 15.

Taarifa kutoka serikalini na taasisi nyingine zinazoshughulikia uchunguzi zinasema, Dk. Dau ambaye aliong’olewa NSSF 15 Februari mwaka huu, atafikishwa kwa mahakamani, kujibu tuhuma za ufisadi zilizoibuliwa ndani ya shirika hilo.

Tuhuma nyingine ni matumizi mabaya ya madaraka, uzembe na ukiukwaji wa taratibu katika miradi ya uwekezaji na vitega uchumi mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Miongoni mwa miradi hiyo, ni ujenzi wa daraja la Kigamboni; hoteli ya kitalii jijini Mwanza, mradi wa ujenzi wa majengo katika mji mpya wa Kigamboni, uwekezaji kwenye jengo la biashara la Mzizima na mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira, mkoani Mbeya.

Wakati huo huo kuna taarifa kuwa wakurugenzi wakuu wa NSSF akiwemo Magori nao wamehojiwa na TAKUKURU kutokana na tuhuma za ubadhirifu na rushwa.

Magori ambaye ni Director wa Operations anatuhumiwa kuwa alipokea mabilioni toka kwa makampuni ya madini huko Geita wakati Eunice anatuhumiwa kupokea pesa toka makampuni lukuki ya matangazo, pia sakata la staff uniforms na kahusishwa na kampuni ya MARIEDO BOUTIQUE.

Eunice pia anatuhumiwa kupokea rushwa kwa ajili ya kufanikisha kuwapatia kazi watu walioomba kazi NSSF.

Stay tuned, kesho Alhamis gazeti la MSETO linaanika kila
kitu.

Source: Mwanahalisi
 
jamaa akipelekwa mahakamani ,ndugu zetu katika imani watakuja juu sana eti kuna mfumo kristu
 
Hatimaye DK. Ramadhan Dau, aliyekuwa mkurugenzi wa Shirila la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kutoka sasa.

Dk. Dau anatuhumiwa kuingiza NSSF hasara ya mabilioni ya shilingi, kutokana mikataba ya kinyonyaji. Amekuwa katika shirika hilo kwa miaka 15.

Taarifa kutoka serikalini na taasisi nyingine zinazoshughulikia uchunguzi zinasema, Dk. Dau ambaye aliong’olewa NSSF 15 Februari mwaka huu, atafikishwa kwa mahakamani, kujibu tuhuma za ufisadi zilizoibuliwa ndani ya shirika hilo.

Tuhuma nyingine ni matumizi mabaya ya madaraka, uzembe na ukiukwaji wa taratibu katika miradi ya uwekezaji na vitega uchumi mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Miongoni mwa miradi hiyo, ni ujenzi wa daraja la Kigamboni; hoteli ya kitalii jijini Mwanza, mradi wa ujenzi wa majengo katika mji mpya wa Kigamboni, uwekezaji kwenye jengo la biashara la Mzizima na mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira, mkoani Mbeya.

Stay tuned, kesho Alhamis gazeti la MSETO linaanika kila kitu

Source: Mwanahalisi
Mkuu rekebisha "tittle to include Ambassador"
 
Mkuu rekebisha "tittle to include Ambassador"
Ha ha ha, hakuna hio option mkuu, ni mpaka Mods wenyewe wafanye.

Na kwa habari nyeti kama hizi huwa hawakubali, wanatoa macho muda wote kwenye sredi kama hizi
 
IMG_5308.jpg

Habari imepikwa na hawa wawili ambao ni mtu na hawara wake

MAGORI na CHIUME wote ni wafanyakazi wa NSSF
 
jamaa akipelekwa mahakamani ,ndugu zetu katika imani watakuja juu sana eti kuna mfumo kristu
Preemptive strategy iliyotumika ndani ya siku hizi mbili tatu hakuna mtu atakaye kuja juu.

Magufuli ni kichwa ingine ile, hakuna anayeweza kucheza na sharubu zake kama walivyokuwa wanamchezea Mkwerre.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom