Sheria kali na hukumu za maana zitolewe kwa wahusika wote, sio viongozi wa NSSF tu bali hata wale azimio wauza viwanja na kampuni yao ifungwe mara moja ku operate Tanzania. Pia hawa watu inabidi mali zao na account zao zote zikamatwe,ziuzwe na kufidia pesa zote zilizopotea, kama sheria hizi hazipo basi ni wakati muafa wa serikali kupeleka pendekezo bungeni haraka lakini tayari wakiwa wameshakamata mali na account zote za ndani na nje za haya mafisadi. Kutowachukulia hatua kwa haraka na kuwapa dhamana na kuwafunga vifungo vya miaka mitano sijiu sita ndo kunawasabisha hawa watu waendelee kuwa wezi, tutoeni adhabu ili watu tuweze kujifunza na tuwe na hofu ya wizi. Serikali pia iangalie jinsi ya kuwapunguzia wakurugenzi wote mamlaka ya kuidhinisha pesa. Hii ni aibu sana, hata tukiangalia makampuni binafsi hakuna wakurugenzi,ceo,general managers walio na maamuzi ya pesa kwenye project ya 1.3 trioni, wekeni limitations ili kupunguza kasi ya wizi.