johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Dr. Anthony Diallo amesema ni makosa makubwa na hatari sana kuwaachia wanasiasa watengeneze katiba ya nchi.
Diallo amesema wanasiasa ni wabinafsi hivyo lazima wajipendelee ndio maana katiba ni lazima itengenezwe na wananchi wakisaidiwa na Wataalamu kama ilivyofanyika nchini Kenya.
Diallo yuko mubashara Star tv akihojiwa na Aloyce Nyanda.
=======
Dkt. Anthony Diallo: Mimi sio mtaalam sana wa masuala ya katiba lakini naamini kitu kimoja, katiba huwa ni ya watu, ni ya wananchi wa nchi ile. Katiba haiwezi kuwa ya chama, kosa moja tulilofanya wakati ule mwaka 2014 kwamba vyama ndio vilivyotaka kutengeneza katiba, sio katiba ya wananchi.
Kama mlifuatilia utaratibu uliotumika Kenya, wataalam walichukuliwa wakapelekwa kwenye eneo fulani linaitwa Bomas wakachakata wataalam wa Sheria.
Walipomaliza ikapitiwa tena na wataalam wengine, baada yakupitiwa wakapata draft, ile draft ikapelekwa kwa wananchi kwa kura za maoni, haikwenda bungeni straight.
Sisi hapa unasikia wanaopiga kelele wanasiasa, hakuna nchi ambayo katiba yake hata hii ambayo tunaitumia leo ya 77 ilikuwa revised lakini original katiba ni ya Lancaster ya mwaka 60 ambayo ndio ilitengenezwa tukisaidiwa na wataalam wa kiingereza kwa ajili ya uhuru wa Tanganyika.
Katiba wanasiasa tunafanya makosa kujiingiza, ukijiingiza mwanansiasa kwenye katiba, katiba ile itakuwa biased tu, si ntataka kujipendelea.
Pili, nchi za kiafrika tunafanya makosa sana kuona Katiba ndio tatizo, tatizo lipo kwa watu. Mnafanya makosa, mnaweka Rais ambae atakuja kuvuruga hiyo katiba, kwani katiba ya leo inaruhusu mtu anawekwa Magereza bila kupelekwa mahakamani? Yalifanyika, tatizo letu ni mtu wala sio katiba