Dr. Diallo: Katiba inatengenezwa na Wananchi siyo Wanasiasa, 2014 tuliikosa katiba mpya kwa ubinafsi wa wanasiasa CCM ikiwemo!

Kitu ambacho Diallo anashindwa kuelewa ni kuwa katiba mbovu hutumika vibaya na katiba nzuri na madhubuti inatoa dira ya maendeleo ya nchi na inambana kiongozi ye yote kutumia madaraka yake vibaya!
 
Mahojiano kati ya Mhe Anthony Diallo Mwenyejiti wa CCM Mkoa wa Mwanza na Mtozi Alloyce Nyanda


Mjadala umeleta hisia na ushahidi mpya kuhusu utawala wa JPM
1.Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Biashara yetu ya Star Tv ,RFA iliharibika -Diallo

2.Sie hatukulipwa na CCM , waliolipwa ni Crew iliyokuwa inatembea na vifaa kama majukwaa , walipewa hela ya kula na kubeba vifaa , ukitazama katiba vitabu vyetu kuna hela chama hadi leo haijakipa-Diallo Mwenyekiti wa CCM

3.Mgombea wetu wa wakati ule alisema atatusaidia na alisema hadharani tena mara mbili pale
Kirumba na furahisha lakini tuliambulia misukosuko

4.Awamu ya 5 iliharibu sana protocal ya Chama , viongozi wa chama walikuwa wanawekwa mstari wa nyuma kabisa gari zinakuwa mwisho hata kama ukifika unakuta mtu amekata utepe-Anthony Diallo mwenyekiti wa CCm

5. Kuna kisa kimoja kiongozi wa CCM mkoa wakati flani tumeenda kumpokea Rais alipigiwa kiwako akadondondoka ,awamu ya Tano ilikuwa inazuia viongozi wa CCM hata kuingia uwanja wa ndege wanaelezwa kubaki nje -Antony Diallo Mwenyekiti wa CCm


6.Kuna siku nimemwambia waziri mkuu , hivi unajisikia raha gani kuzungukwa na mabunduki maana umezungukwa na mabunduki kama ishiri sie tumekuchagua ila unatuogopa ki vipi? -Antony Diallo

7.Swala hapa siyo katiba swala ni kuchagua watu makini ,unawezaje kuchagua kiongozi katika nafasi kubwa ya uongozi huku ana rekodi ya mirembe? Tuwe makini kuchagua viongozi-Anthony Diallo

8. Kama nchi tumepitia katika kiza kifupi ,tumepitishwa katika Black spot apo Nyuma , Sasa angalau watu wanaraha furaha imerejea-Dkt Anthony Diallo

9. Hata mimi Nimeshgulikiwa kidogo wakaniacha ila nimepata Msukosuko- Anthony Diallo


10. katiba siyi ya Vyama ni ya wananchi kosa tulilofanya ni kugeuza katiba kuwa vyama na kuacha wananchi hata katika lile bunge walitawala wananchi-Dk Anthony Diallo

11. Katiba siyo Tatizo , tatizo lipo Kwa watu mnachagua Rais ambae hataki kufata katiba mtanfanya nini? Kwani katiba ya sasa ilikuwa inaruhusu mtu kuwekwa ndani bila utaratibu? Lakini yamefanyika-Anthony Mwandu Diallo

12. Rais samia nimefanya nae kazi ni Rais makini na jasiri ni muumini wa utawala wa bora-Anthony Diallo

13.CCM tulijua haitashinda mwaka 2015 na wananchi wamegeuka wiki mbili tu baada ya kuamua hata kuunda makundi ya vijana kwenye maeneo mbali mbali waweke Star Tv ilibidi itumike nguvu

15.Kuna mambo hatukuweza kuyasema kwa sababu mfumi uliharibika kabisa. Tuliamua Kunyamaza tuliamua ku place safe mode ili kesho uendelee kuishi na watoto wako.

Jamani Mzigo upo Youtube . Nendeni jamani Diallo amesukumiwa maswali mazito na mtangazaji wa Star Tv Mtozi Alloyce Nyanda kama si boss wake ila Diallo kashangaza. Kawa mkweli na muwazi
 
Hiyo namba 13 ilikuwa inapofika wakati wa taarifa ya habari kuna vijana walikuwa wanatumwa kwenye mabaa kuhakikisha channel ya Star tv ndiyo inayoonyeshwa badala ya channel zingine!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…