Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tena linaonekana ni toto la mwisho kwa mama yake.Ni jambo la ajambu sana kwa mwanaume kama wewe kumpiga majungu mtoto wa kike kama gwajima
Ni hivi tunapokwenda kwenye nyumba za ibada viongozi wa dini wanapotoa sermon.Yaani watanzania tuna shida kubwa sana, tumefika mahali yunaamini kuwa mtanzania mmoja akiwa Waziri wa afya anaweza kutatua changamoto za Wizara ya afya. Kwanini tunakuwa na mawazo duni hivo, changamoto za Wizara ya afya zitatatuliwa na wana jamii wanapokuwa free kuhoji na vyombo vyetu vya habari vinapokiwa huru na kuandika habari zankoutafiti watu wenye uelewa kufanya utafiti na kupendekeza nini kifanyike kuboresha Wizara. Hivi hiyo Wizara si ndiyo ililazimishwa kusema uwongo kuhusu covid 19 hadi watu wadilifu wakafukuzwa.
Matatizo ya Wizara yatatatuliwa tutakoomdokana wa jamii ya wanafiki watu wakitaka kujipendekeza waongo na waoga walio katika sehemu mbali mbali za kazi. Kuendelea kukuombatia wanafiki, waongo, waoga na watu wakujipendekeza hakiwezi kutatua tatizo lolote sana sana tutaendelea kupiga sound kwenye mikutano na vyombo vya habari kumbe hakuna chochote.
Hivi wakisema madawa katika mahospitali na vituo vya afya yanapatikana kwa asilimia 78 huwa mkiugua na kwenda huko Hospital mnathibitisha hizo takwimu. Hii Wizara haihitaji kelele na matatizo ya Wizara yanatakiwa kutatuliwa na ma Katibu wakuu maana ndiyo wataalam wa hizo Wizara na hata nafasi zao ni za utendaji.
Hao mawaziri ni wapiga Siasa tu hakuna jipya wanaloweza kufanya wote tunawafahamu wanapenda kiki ili aliyewageua ajuwe wanafanya kazi.
Huyo mama ni mpiga mayowe kama alivyokuwa Kanga Lugole. Muda utasemaNi hivi tunapokwenda kwenye nyumba za ibada viongozi wa dini wanapotoa sermon.
Kuna makundi yafuatayo yatamuelewa zaidi anatokea wapi na maneno yake; kuna wanaosoma vitabu vya dini, wale waliojifunza dini wakati wadogo na wacha mungu sana.
Wengine dini ambayo aijatukaa sana sana tunaokota okota wakati sermon inaendelea.
Ndio kama baadhi ya watu wanavyomuona huyo mama kwa wale wenye kuelewa management ya afya awamuoni kama mtu anaepayuka isipokuwa as part systematic control kutokana anachoongelea kuna wasaa anazingumzia aspect za ‘empowering services users’, managing Human Resources, managing financial resources, facilitating changes, managing quality and health promotion.
Kwa ivyo kama una elewa afya unaweza kuona value yake and apparently wizara ina policies and guidelines nzuri tu tayari juu ya hayo mambo nimejifunza hayo kupitia kwake kwa sababu anajua namna ya utekelezaji wake unavyotakiwa kuwa na akifika ana mbinu za kukaguwa.
Usione kwenye video zingine anafika sehemu na ananyanyua godoro na kufungua cover ukadhani mwehu kuna regulations pia mpaka za quality za mahala wagonjwa wanapotakiwa kulala.
Hali kadhalika kwa wale wasiolewa management ya afya wanaweza muona anapayuka tu, bila ya kuelewa kwanini.
Kwa mtu yeyote ambae anadhani ipo siku atatumia hospitali za serikali kwenye chi ambayo kuna gap kubwa kwenye utolewaji wa kiwango cha huduma kati ya walionacho na wasionacho (and the probabilities of coming out alive) basi huyu mama ni mkombozi nina imani atafanikiwa kuweka standardisation ya huduma katika hiyo wizara.
Afanyi ivyo kutafuta sifa bali kwa maslahi mapana ya watumiaji wa huduma.
Mna mwangia sana kwa ivyo sitoshangaa akitumiliwa husda ya jicho nayo inanguvu.Huyo mama ni mpiga mayowe kama alivyokuwa Kanga Lugole. Muda utasema
Huyo siyo MSUKUMA Wasukuma hawako hivyoWasukuma wana tabu sana
FoolishNi jambo la ajambu sana kwa mwanaume kama wewe kumpiga majungu mtoto wa kike kama gwajima
Mkuu, ulinielewa vibaya!! nimezungumuza hili bila chuki na unafiki kabisaa!! Mi nilimanisha wingi Kama wingi!!Mawaziri wameteuliwa Kwa kuzingatia Mikoa yao! Kanda ya ziwa ina Mikoa mingapi? Kama ni zaidi ya mmoja basi tulia dawa ikuingie acha udaku! Au ulikimbia hesabu?
Queen Esther
Dr Gwajima anajitahidi kuboresha mfumo wa afya ili wapate wateja wengi kwenye Universal Health Carea Insurance. (Moja ya manifesto za Lissu na Chadema).
Tatizo lililopo ni mfumo mbovu wa utawala. Kama katiba inapindishwa, daktari anaefanya makosa akiwa ni ndugu wa rais atawajibishwa?
Nape alipofuata utaratibu na akatumbuliwa baada ya Makonda kuvamia Clouds ilikuwa Corona ? kutetea watu hawa unapaswa kwanza kuwa mwehu , endelea na imani yako , bali utambue kwamba Watanzania siyo Wajinga
Pole MkuuIla jamaa unabore sana
Mkuu habari za hapo GeitaWe fake kweli. Unatafuta tu mahali lazima umtaje Rais. Ungeenda kumsadia babu Fake Original Lissuu. Mbebaa maono ya wazungu.
Akitumia utaratibu ilio wazi kama Daily briefing,safety meetings,vikao vya ndani zitambana kupika majungu.Yawezekana alikuwa anatamani ukubwa sasa kapewa hadi uwaziri wa wizara hiyo hiyo.Kazi kwake kwani Magufuli na umma unasubiri matokeo.Raisi Magufuli alishaweka wazi hataki selfie, we all know behind selfies everything else is bullshit...kuita makamera man, malipo, usafiri vipaza sauti, lunch & all that, hizi sinema zimeshapitwa na wakati, watu tunasoma report siku hizi hatutaki sinema...huyu mama arudi kwenye ubora wake...daily briefing, vikao vya ndani kama ni kufokeana huko huko ndani, mkifukuzana tusijue...wananchi wa kawaida tuone matokeo, hatutaki maigizo for God's sake
Hivi ni mke wa gwajima?Binafsi Siamini kama Wizara ya Afya, ambayo kwa maoni yangu ni Wizara nyeti kabisa inahitaji kuwa na Waziri, ama viongozi wenye makeke, ama makelele yasiyo na tija.
Kwanza uzoefu unatuonesha viongozi wenye makeke/ makelele wala hawadumu katika nafasi zao maana huwa hawana Ufanisi wowote zaidi ya kuzurura huku na huko wakipiga makelele na kutofanikisha lolote... mfano, Paul Makonda, Kigwangallah, Humphrey Polepole, Kangi Lugola na juzi Magu amemtaja Jafo kuwa Anazunguka tu lkn hakuna Ufanisi wowote katika mizunguko yake hiyo na makelele yake.
Sasa ametoka Lugola kaingia Mmama mmoja ana makeke kweli, Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya na Mnyiramba wa Shelui, Singida. Naye anatembea na Ilani ya CCM na scarf ya bendera ya Tanzania kama Lugola na kama Mwigulu...makelele yaleyale, makeke yaleyale, mikogo ileile.
Namwona hafiki Mbali, kama wapo wa Karibu yake wamwambie atulize wenge afanye kazi kwa Utulivu na Maarifa
Asije kusema hatukusema, ana mdomo sana yan chaaa[emoji1784]
Wana mzigo wa ushamba wanatembea nao kichwani!!Wasukuma wana tabu sana
eti namtabiria, kabet tuone Kama unaweza kutabiriNimemsikiliza nikacheka sana ! hivi ni kabila gani huyo mama ?
Namtabiria muda mfupi sana .