Dr. Dorothy Gwajima na makeke kama Kangi Lugola

Dr. Dorothy Gwajima na makeke kama Kangi Lugola

Binafsi Siamini kama Wizara ya Afya, ambayo kwa maoni yangu ni Wizara nyeti kabisa inahitaji kuwa na Waziri, ama viongozi wenye makeke, ama makelele yasiyo na tija.

Kwanza uzoefu unatuonesha viongozi wenye makeke/ makelele wala hawadumu katika nafasi zao maana huwa hawana Ufanisi wowote zaidi ya kuzurura huku na huko wakipiga makelele na kutofanikisha lolote... mfano, Paul Makonda, Kigwangallah, Humphrey Polepole, Kangi Lugola na juzi Magu amemtaja Jafo kuwa Anazunguka tu lkn hakuna Ufanisi wowote katika mizunguko yake hiyo na makelele yake.

Sasa ametoka Lugola kaingia Mmama mmoja ana makeke kweli, Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya na Mnyiramba wa Shelui, Singida. Naye anatembea na Ilani ya CCM na scarf ya bendera ya Tanzania kama Lugola na kama Mwigulu...makelele yaleyale, makeke yaleyale, mikogo ileile.

Namwona hafiki Mbali, kama wapo wa Karibu yake wamwambie atulize wenge afanye kazi kwa Utulivu na Maarifa

Asije kusema hatukusema, ana mdomo sana yan chaaa🤧
Ondoa Jina la Paul Makonda hapo!!

Kweli ana kelele nyingi, lakini Kwa upande wa ubunifu, jamaa Yuko fiti kinoma, Aliweza kuwatengenezea mazingira ya kutibiwa bure watoto wenye matatizo ya moyo, walemavu kupata miguu bandia bule, tayari alikuwa ameanza kuandaa utaratibu wa matibabu bule ya wenye mabusha, wanawake kupata haki za kisheria bule n.k, hizo hazikuwa kazi za kawaida za mkuu wa mkoa pekee

Jamaa anagundu tu, lakini Yuko fiti kuliko hata wewe kazi yako kuandika mabaya tu ya watu huku ukifunika wema wao
 
Hapana najua iko siku nitaumwa sitaki nipate services mbovu au daktari aje kunifanyia majaribio mwili wangu, kwa ivyo mtu ambae anajaribu kurekebisha mambo lazima awe rafiki yangu.

Marehemu baba yangu kaondoka kwa type 2 diabetes wakati anafanyiwa operation ya kukatwa kidole cha mguu (it should have been a normal operation procedure).

Kuna watu nawajua wamepoteza ndugu zao kwenye kujifungua mimba ambazo azikuwa na complications zozote isipokuwa uzembe tu wa midwives.

Tanzania mpaka leo jamii ailewi usonji ni nini na wala hakuna promotions campaigns to raise awareness nor minimal intervention to assist families. Watu wanalea watoto wao especially those with serious autism conditions na kila aina ya accusation kutoka kwa jamii sijui waliwatoa kafara etc with social ignorance on the condition. Who is responsible for tackling misconception and provide family support? aileweki so far, mara mkuu wa wilaya sijui nani ndio anatakiwa aje na solution all to do with the ministry incompetence.

In short hiyo wizara ilikuwa ovyo.

Ndio maana nina passion nayo kwa sababu najua iko siku nitafika kutumia huduma zao sasa sitaki maisha yangu yawe bahati nasibu na mtu anaekuja kunituba do he/she cares about my wellbeing or not, I like certainty in my life.

Kwa ivyo anapotokea mtu mwenye uelekeo wa kubadili jinsi watu wanavyofanya kazi through systematic approaches. Mafanikio ya initiatives zake ni kwa faida zangu na naona hiyo kazi anaiwezi lazima niwe upande wake ata angekuwa dada yake wa kuzaliwa Magufuli.

Muhimu kwangu ni maslahi yangu ya mbeleni maana iko siku nitafika tu hospitali nikifika nataka nipewe huduma bora.

Yaani watanzania tuna shida kubwa sana, tumefika mahali yunaamini kuwa mtanzania mmoja akiwa Waziri wa afya anaweza kutatua changamoto za Wizara ya afya. Kwanini tunakuwa na mawazo duni hivo, changamoto za Wizara ya afya zitatatuliwa na wana jamii wanapokuwa free kuhoji na vyombo vyetu vya habari vinapokiwa huru na kuandika habari zankoutafiti watu wenye uelewa kufanya utafiti na kupendekeza nini kifanyike kuboresha Wizara. Hivi hiyo Wizara si ndiyo ililazimishwa kusema uwongo kuhusu covid 19 hadi watu wadilifu wakafukuzwa.

Matatizo ya Wizara yatatatuliwa tutakoomdokana wa jamii ya wanafiki watu wakitaka kujipendekeza waongo na waoga walio katika sehemu mbali mbali za kazi. Kuendelea kukuombatia wanafiki, waongo, waoga na watu wakujipendekeza hakiwezi kutatua tatizo lolote sana sana tutaendelea kupiga sound kwenye mikutano na vyombo vya habari kumbe hakuna chochote.

Hivi wakisema madawa katika mahospitali na vituo vya afya yanapatikana kwa asilimia 78 huwa mkiugua na kwenda huko Hospital mnathibitisha hizo takwimu. Hii Wizara haihitaji kelele na matatizo ya Wizara yanatakiwa kutatuliwa na ma Katibu wakuu maana ndiyo wataalam wa hizo Wizara na hata nafasi zao ni za utendaji.

Hao mawaziri ni wapiga Siasa tu hakuna jipya wanaloweza kufanya wote tunawafahamu wanapenda kiki ili aliyewageua ajuwe wanafanya kazi.
 
Safi san kuna dr mmoja aliulizea dawa zinapatikana kwa asilimia ngapi akasema 92.5% kimbembe kilpokija aonyeshe hizo dawa na awspe wananchi ndo akatamani Ardhi ipasuke aingie humo
 
Kuna mtu amesema na mnyiramba wa shelui!! Basi wanyiramba watakuwa na bahati wakatu huu!!
1- Kitilla mnyiramba
2- Mwiguru aka madelu mnyiramba
3 - Dorothy aka makelele mnyiramba
Ukiondoa wasukuma kwenye baraza la mawaziri, kabila linalifuata kwa kuwa na mawaziri wengi ni wanyiramba!!

Mawaziri wameteuliwa Kwa kuzingatia Mikoa yao! Kanda ya ziwa ina Mikoa mingapi? Kama ni zaidi ya mmoja basi tulia dawa ikuingie acha udaku! Au ulikimbia hesabu?

Queen Esther
 
Ahakikishe nchi inakuwa na university hospital na pia hospitali ya taifa muhimbili haileweki, haina idara nyingi kama moyo, mifupa, Bado inazitegemea Jakaya heart institute na MOI nini maana ya hospitali ya taifa?
 
Magufuli hajakosea kumleta Dr Gwajima...si far the changed attitude ya watumishi wa afya ni matunda ya mama huyu.
Jipe muda uione Afya ya Tanzania inavyoondokana na hisani ya watu waMarekani
 
Dr Gwajima anajitahidi kuboresha mfumo wa afya ili wapate wateja wengi kwenye Universal Health Carea Insurance. (Moja ya manifesto za Lissu na Chadema).

Tatizo lililopo ni mfumo mbovu wa utawala. Kama katiba inapindishwa, daktari anaefanya makosa akiwa ni ndugu wa rais atawajibishwa?
Usipomtaja Lisu menstruation inakoma eheehh???
 
Huenda huyu waziri wa Afya akawa wa ovyo zaidi kuliko wote waliopita. Yaani kaanza vibaya sana. Nitatoa sababu kadhaa hapa.

Wizara ya Afya ni wizara inayohitaji waziri mtulivu, msikivu na mshirikishaji. Hakuna sababu yoyote ya waziri wa afya kufanya kazi kwa mlengo wa kupambana na watumishi wa wizara wa Afya.

Hulka ya watumishi wa Afya wanapenda sana kiongozi anayeweza kuongea nao kwa lugha na mtindo wa kuheshimiana na kiuweledi kulingana na taaluma yao. Matatizo ya afya hapa Tanzania yamekuwepo, yapo na yataendelea kuwepo. Na hilo sio issue, issue ni namna ya kuweza kuyatatua.

Hizi blah blah za Dr.Gwajma kutembea na ilani ya CCM, kufoka mbele ya media au kuwalaumu watendaji wa chini wa wizara ya Afya hayatasaidia kitu. Ni kaburi tu analojichimbia tu.
 
Kama makelele yake yanasaidia kuboresha utendaji kazi, basi aedelee tu.
Tuchape kazi ndugu zangu. Maendeleo hayana vyama .
 
Haya wewe peke yako ndio mwenye akili za kuweza kumtetea mtu kama Lissu ambae ni kituko mbele ya dunia na watanzania walio wengi, isipokuwa kwako.
Lisu anakujaje hapa. Alama ya kwanza ya mjinga ni kutojua kinachojadiliwa. Hata mahospitalini, namna ya kumtambua kichaa, kama siyo agressive, ni kusikiliza majibu anayoyatoa baada ya kuulizwa.

Kwa mfano:
Daktari: Unatokea wapi?

Mgonjwa: Rais Magufuli ni mzuri sana

Assessment: 90% assurance, mgonjwa ni kichaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiichukulie TISS poa hizi propaganda za nationalism; raisi, waziri mkuu na Bashiru wanazoziongelea usidhani nikufurahisha umati hao watu wanataarifa.

Lissu is a snake, awezi ishi Tanzania anajua mawasiliano yake yataingiliwa. Inawezekana kabisa anaachiwa ili serikali ijifunze kupitia kwake motives za mataifa ya west kwa Tanzania.

Usione watu wapuuzi walipomuacha avunje kanuni za uchaguzi huku wakijua awezi shinda; na wao wana motives zao.
Hivi unawafahamu hao TISS? Wengi wao siyo wataalam bali ni wambeya. Wameigeuza kazi ambayo ni profession na kuifanya ni kazi anayoweza kufanya kila mtu. Wamekuwa watu wa kusikiliza majungu ya mitaani na kuyafikisha kwa wakuu wao kama taarifa za kiuchunguzi.

Kama wazungu wangekuwa wanamtumia Lisu, wasingeshindwa kuyalinda mawasilano yao na yeye Lisu yasidukuliwe. Mitambo yenyewe wanayotumia TCRA wametengeneza wao.

Savimba alikuwa anatumia sat phone maalum aliyopewa na wamarekani kwa zaidi ya miaka 20, hakuna aliyeweza kuyanasa mawasiliano yake. Siku Wamarekani walipomwambia aache mapambano, aende Luanda kwa mazungumzo, yeye akagoma, siku ya 3 mawasiliano yake yakanaswa na watu wa Serikali ya Angola, na siku hiyo hiyo akauawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi huyu mama, Dr. Dorothy Gwajima nimeanza kumfuatilia tangu ni Naibu katibu mkuu wizara ya afya. Ni mchapa kazi mzuri sana tumpe muda atufikishe pazuri kwenye sekta ya afya.

Ana kiu ya kuleta mabadiliko ya kweli. Kwenye mapungufu tushauri sio kukosoa na kubomoa na ujuaji sana.
 
Huenda huyu waziri wa Afya akawa wa ovyo zaidi kuliko wote waliopita. Yaani kaanza vibaya sana. Nitatoa sababu kadhaa hapa.

Wizara ya Afya ni wizara inayohitaji waziri mtulivu, msikivu na mshirikishaji. Hakuna sababu yoyote ya waziri wa afya kufanya kazi kwa mlengo wa kupambana na watumishi wa wizara wa Afya.

Hulka ya watumishi wa Afya wanapenda sana kiongozi anayeweza kuongea nao kwa lugha na mtindo wa kuheshimiana na kiuweledi kulingana na taaluma yao. Matatizo ya afya hapa Tanzania yamekuwepo, yapo na yataendelea kuwepo. Na hilo sio issue, issue ni namna ya kuweza kuyatatua.

Hizi blah blah za Dr.Gwajma kutembea na ilani ya CCM, kufoka mbele ya media au kuwalaumu watendaji wa chini wa wizara ya Afya hayatasaidia kitu. Ni kaburi tu analojichimbia tu.
Haa anajua kule ni tamisemi kwamba atawapelekesha huku na kule ili hali anajua pesa hajatoa ya shughuli husika mara fanya hiki mara kile
 
Back
Top Bottom