Wabongo tunakwamishana wenyewe kutokana na kuendekeza wivu usio na maendeleo.Kosa la Dr Shayo ni kuweka article yake kwa Michuzi,just like Mashaka did,kwa ajili ya matumizi ya Watanzania wenzie.Ma Know-all wetu,ambao sijui level zao za elimu zikoje (I'm always suspicious of people who tend to unnecessarily use difficult terms in attempt to convince their audiance kwamba shule imepanda).
Hivi nyie critics wetu ni lini mtakuja na article zenu zisizo na chembe ya makosa ya kisarufi au kifasihi na zenye kubeba ujumbe mzito kwa umma?Sana sana ujanja wenu ni hapahapa JF,na wala sio ujanja wa kuja ni vitu tofauti na hivyo mnavyovi-criticize,bali mashindano ya maneno magumu ya Kiingereza.
Missing link sio the Mashakas,Shayos,etc bali ni wenzetu mnaotumia muda mwingi kumjadili mtoa mada badala ya relevancy na substance ya mada husika.Hatujawahi kuambiwa kuwa watu wenye akili za kutosha hujadili mambo ilhali wale wenye akili pungufu hujadili watu?Missing link ni watu wanaosubiri wenzao waseme ili wao wakosoe ilhali wao wenyewe hawana jeuri ya kusema in the first place,pengine kwa hofu ya kukosolewa japo wao ni mahiri wa kukosoa.
Kwa mtu anayethamini elimu,na anayefahamu ugumu wa kupata madaraja flani ya kielimu (eg udaktari wa falsafa) inasikitisha kuona michango ya kitaaluma ikiishia kukosolewa sio kwa vile haijabeba ujumbe wa maana bali tuhuma kwamba ina madudu kwenye lugha.Na watoa tuhuma hawafanyi jitihada zozote za kuonyesha madudu yenyewe yako wapi.
Hivi hadi tumefika hapa,hayo madudu yaliyomo kwenye article ya Dr Shayo ni yapi hasa?
"Jealousy is simply and clearly the fear that you do not have value. Jealousy scans for evidence to prove the point - that others will be preferred and rewarded more than you. There is only one alternative - self-value. If you cannot love yourself, you will not believe that you are loved. You will always think it's a mistake or luck. Take your eyes off others and turn the scanner within. Find the seeds of your jealousy, clear the old voices and experiences. Put all the energy into building your personal and emotional security. Then you will be the one others envy, and you can remember the pain and reach out to them." - Jennifer James