Elections 2015 Dr. John Pombe Magufuli achaguliwa kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM 2015

Elections 2015 Dr. John Pombe Magufuli achaguliwa kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM 2015

Hatimaye huyu Dr Magufuli maombi yake aliyoenda kuomba huko Nigeria yamejibiwa. Huyu mzee alionekana akiwa church huko kwa Joshua akipata maombi. Nchi sasa itarudi kukaa sawa. Yale makando kando ya mtangulizi wake yataondoka kwa kweli.
 
Mie nilidhani unataka kusema Rais Shoga, Toba. Kama Mwanamke, poa tu ila awe na akili zake kama Halima Mdee hivi.

Mambo ya kuwa na Rais Mwanamke kama yule Mama wa CCM Mbunge, anaitwa nani vile?

hapa tunaandaliwa siku moja tutakuwa na rais mwanamke tu na tunakaribia sana
 
We have seen it all by now. CCM party machinery at it's very best mesmerizing opponents and displaying the sheer power it holds over Tanzanian politics.

Kikubwa nilichokiona mimi binafsi ni jinsi gani Tanzania tunaendelea na zoezi la kuhamisha Mvinyo kutoka chupa moja hadi nyengine kila baada ya miaka kumi.

CCM ni mfano Hai wa taasisi Iliyowahi kuwa na Mvinyo Bora kuliko yote Afrika (Mfumo mzuri wa Uongozi wakati wa Mwalimu Nyerere), Na chupa yenye ubora na yenye kuvutia (Nyerere).

Baada ya miaka mingi ya kunywa mvinyo huu, wananchi wa TZ, waliukinai, wakaamua kutia maji ili kuulainisha ladha na kubadili chupa ya kuhifandia mvinyo ili kuufanya uvutie kwa wanywaji wa nje (mabepari na wawekezaji).

Kila baada ya miaka 10,mvinyo huu hubadilishwa chupa, na kuwekwa kwenye chupa mpya, huku wanywaji wakiambiwa kuwa mvinyo umeboreshwa kwa viwango vipya kabisa. Kiuhalisia kinachotokea ni kuwa mvinyo hubakia kuwa ule ule,uliotiwa maji, na unaoendelea kupoteza ladha.

Miaka kumi iliyopita, tuliletewa Chupa maridadi kweli kweli,tukiahidiwa kuwa, kwa kuwa chupa ni maridadi kimuonekano, basi hata mvinyo nao ni maridadi.sisi ni wepesi kuamini, tukaamini hivyo mara moja, haikuchukua muda mrefu kujua kuwa ingawa uliwekwa kwenye chupa maridadi, mvinyo huu ulikuwa bomu kweli kweli.labda bomu kuliko hat amvinyo tulionunua miaka ya kabla yake. manungu'iko yalivyoongezeka na mauzo ya mvinyo kupungua,wakazunguka nchi nzima kukusanya mvinyo wao wakiahidi miaka kumi ikitimia watahakikisha wanafanyia kazi maoni yetu na kutupatia mvinyo bora, kwani walishaanza kuona watu wameizoea hii chupa mpya.

Hivi punde muda wa kuleta mvinyo mpya umewadia, wapika mvinyo kama kawaida yao wamemaliza maonesho ya kunadi mvinyo wao kwa kuvumbua chpa mpya tena, huku wakiahidi kuwa chupa hii ni imara na bora kuliko chupa zilizopita.

Wengi wa wanunuzi wameshaanza kuingia "line" kununua mvinyo huu wa kufikirika baada tu ya kuona chupa,lakini daili zote zinaonesha kuwa mvinyo unaoletwa ndio ule ule tuliouziwa miaka kumi iliyopita. Hatujaona dalili zozote za kubadilisha mvinyo, hata mitambo inayotumika kuandaa mvinyo ni ileile, malighafi ni zile zile, na wapika mvinyo ni wale wale. Ila kwa imani yetu inayoendelea kutuangusha kila baada ya miaka 10 tumeendelea kukubali maneno yale yale kuwa mvinyo umeboreshwa,wakati hali haioneshi hivyo.


Pembeni ya CCM kuna taasisi kadhaa zilizoamua kuunda umoja wa UKAWA ili na wao wauze mvinyo wao kw awatanzania. Taasisi hizi mvinyo wao unasemekana kuwa mzuri,sema CHUPA zao hazina mvuto wa chupa za CCM. La kushangaza hawa mabwana ingawa hakuna ajuaye ladha ya mvinyo wao, zaidi ya kuupima kwa kutumia chupa uliyokuwemo, wameendelea kuleta mvinyo wao kwa kutumia chupa zile zile kila baada ya miaka kadhaa.Na hata sasa inasememkana wamekusanya chupa zao zoote za mvinyo zilizokataliwa huko nyuma ili kuchagua moja yenye afadhali, waje waiuze kwa wanywa mvinyo. Matumaini yao ni kuwa wakileta chupa moja iliyokataliwa labda itakuwa rahisi kuchaguliwa,kuliko wakileta chupa zote zilizokataliwa.
Umoja huu wamekuwa pia bize kuponda chupa za mvinyo kuliko kuponda mvinyo wenyewe, wakati wakifahamu wazi kuwa matatizo yanayolalamikiwa na wanywaji sio kwenye chupa bali kwenye mvinyo.

Chupa iliyovumbuliwa hivi karibuni imeshaanza kuundiwa mlolongo wa list kuonesha mapungufu yake,wakati wananchi wanahitaji kusikia mlolongo wa matatizo ya mvinyo utakaokusanya hiyo list.

CCM ni wajanja, wanajua chupa mpya matatizo yanajionesha baada ya muda sio kabla ya kununulika. Wapinzani wanaendelea kuamini kuwa matatizo ya chupa iliyopita yanaweza kuwekwa pamoja na chupa mpya.

Kwa kuwa Mvinyo wa CCM umeendelea kununulika kwa miaka nenda rudi, kila wakibadili Chupa, na Upinzani wameendelea kukaa kimya kuwaeleza wananchi kuwa wanauziwa mvinyo ule ule kwenye Chupa mpya, wananchi wameendelea kununua mvinyo wa zamani kwenye chupa wanazoletewa mpya kuliko kujaribu mvinyo usiojulikana ladha yake kwenye chupa walizozizoea kutoka upinzani.

Kwa kifupi chupa za upinzani zinafahamika, hazijawahi kushinda mvuto chupa za CCM, lakini wote tunakubali mvinyo wa CCM umeshajazwa maji kiasi cha kugeuka kuwa sawa na chai au juisi. Mvinyo wa upinzani hakuna anayeujua kwa kuwa unaendelewa kunadiwa vibaya,na kwa chupa zile zile.

Kilichotokea weekend hii ni CCM kuonesha chupa zake mpya za kuwekea mvinyo wao wa zamani, uliojaa maji na kukosa ladha.

Nikiwa kama mtazamaji wa haya maonesho napatwa na maswali mengi ya msingi nisiyo na majibu nayo.

  1. kwa nini watanzania wameendelea kuuchagua Mvinyo Uleule wa CCM, kila unapowekwa kwenye chupa mpya?
  2. kwa nini wapinzani wa CCM wameendelea kuleta mvinyo wao kwa chupa zilizokataliwa ama kwa kutokuwa na mvuto au kuhisiwa kukosa ubora kama chupa za CCM?
  3. Kwa nini watanzania wanaendelea kukubali kunywa mvinyo wanaoulalamikia kwa miaka zaidi ya 30?na kuushangilia kila ukiwekwa kwenye chupa mpya, na kurudi tena kuulalamikia kila wakgundua mvinyo ni ule ule?
  4. Kwa nini wapinzani wanashindwa kuwaonesha watanzania Tatizo ni Mvinyo na sio CHUPA?


cc: Nguruvi3, JokaKuu, Pasco, Mzee Mwanakijiji, Zitto, Tumaini Makene, Zakumi, Mkandara
 
Last edited by a moderator:
MAWAZO YA KIKOLONI umasikini...
Umofia kwenu wana JF,

Mh Pombe alitumia madaraka yake vibaya na kujimilikisha viwanja nane vya Mbweni Beach JKT na kujenga ghorofa katika kila kiwanja na ghorofa jingine amemuweka nyumba ndogo. Huyu Pombe amepata wapi fedha za kujenga maghorofa nane (kila ghorofa kwenye kiwanja kimoja) simultaneously kuanzia mwanzo mpaka mwisho?

Tumekabidhi wizara kafanya haya ,Je akipewa urais si itakuwa balaa? Huyu mtu sio muadilifu kabisa, hafai kuongoza nchi hii.
 
Tatizo la mgombea wao ni UTULIVU.
Naingiwa na wasiwasi wakipiga bao la mkono maamuzi yake ya haraka haraka.

Ila aelewe kuwa leo kashangiliwa ila kuna 'SHIDA YA UKAWA' mbele.
 
Nani anabisha kuwa deal ya kupata candidate aliye mtaka mkulu imekufa bila kutegemewa? Mkulu hakutegemea kuwa baadhi ya wanakamati wa CC watatoka nje na kueleza kutofuatwa kwa taratibu za kuwapata 5 bora. Ilikuwa ni kama imetoka kwa Mwenyezi Mungu yaani hao (DR. Nchimbi, Mhs Sofia Simba na Mhs Adam …..) walikua malaika wake!

Wana JF, hatuna budi kuwashukuru hawa jamaa hata kama walikuwa wako kwenye kambi ya EL. Maana bila hivyo huyo jamaa wa kusini alishatayarishwa! Imekula kote, yaani kwa Mkulu pamaoja na kwa EL.

Ha ha ha ha. Kweli kabisa, na mwishowe Architect mkuu wa hili ni Mkapa na wazee wenzake. Hatimae makundi hasimu yakatupiliwa mbali kabisa
 
Mhh yupi msafi sasa kumbukeni yeye pia wewe uliyeandika Huna kimada hurt slaa yule ni mke wake haha
 
Tatizo la mgombea wao ni UTULIVU.
Naingiwa na wasiwasi wakipiga bao la mkono maamuzi yake ya haraka haraka.

Ila aelewe kuwa leo kashangiliwa ila kuna 'SHIDA YA UKAWA' mbele.


Obviously Magufuli selection was a carefully controlled manipulation of an illusion of democracy and openness.In african Elections, everything can be done openly, but if vote counting is done in secret then you know what's up.

CCM knowing that their entire performance had to be carefully orchestrated without need for any deviation from the script shamefully decided to conduct counting away from prying eyes. Even more so, announce results overnight. What more proof of a setup and rigging would you need apart from that?

Two thing's do not add up. If Migiro got 280 votes in the previous round,how come she got 59 votes in a round that included even more voters?After she actually pleaded for votes?

If Amina got 284 votes, how come her votes went down in the next session?especially after she publicly pleaded for Lowassa people's votes?
My belief is that Magufuli votes were inflated to create a certain image. to blur off certain divisions,to fool people.

In a normal election The votes at the final session for the two ladies should not have been lower than the totals they got in the previous sessions. they should also have gotten a larger percentage of women votes.

What happened in Dodoma, is simple continuation of theatrics, well played by JK and CCM
 
Wengi wanaosema Ukawa ni hawa hawa wa mitandao ya kijamii..wale mababu zetu kule viijini ambao ni wengi kuliko akina sisi na hawana account hata moja kwenye hizi vitu mnafkiri wanasema nani labda?

Kuna mzee mmoja alinipigia simu toka kijijini akiniuliza kama nafuatilia huu mkutano wa CCM na kuniuliza;"Vipi, hao chichiemu wanenchagua dota Chilaa?" Hadi sasa nafikiria cha kumjibu!
 
Obviously Magufuli selection was a carefully controlled manipulation of an illusion of democracy and openness.In african Elections, everything can be done openly, but if vote counting is done in secret then you know what's up.

CCM knowing that their entire performance had to be carefully orchestrated without need for any deviation from the script shamefully decided to conduct counting away from prying eyes. Even more so, announce results overnight. What more proof of a setup and rigging would you need apart from that?

Two thing's do not add up. If Migiro got 280 votes in the previous round,how come she got 59 votes in a round that included even more voters?After she actually pleaded for votes?

If Amina got 284 votes, how come her votes went down in the next session?especially after she publicly pleaded for Lowassa people's votes?
My belief is that Magufuli votes were inflated to create a certain image. to blur off certain divisions,to fool people.

In a normal election The votes at the final session for the two ladies should not have been lower than the totals they got in the previous sessions. they should also have gotten a larger percentage of women votes.

What happened in Dodoma, is simple continuation of theatrics, well played by JK and CCM

your analysis is superb man. great
 
Kimweri,

..siasa za tz ni ngumu kuliko nchi nyingine.

..kwa mfano hakuna labor unions ambazo zingeweza kuichallenge Ccm.

..pic haiwezekani kucheza siasa za kikabila nchi huku tanganyika. Numbers just don't add up. Kenya unaweza kuanzisha cha ma cha kikabila na within a year ukashinda uchaguzi.

..vilevile ccm imeweza kuzuia kumeguka na wanachama na viongozi wake kuanzisha chama kip ya.

..Kwamba Ccm haikumeguka imesababisha Vyama vya upinzani vianzishwe na watu ambao si wanasiasa au wanasiasa ambao wamechuja au wako past their prime. Kwa mfano Mtei, Makani, na wenzao walioasisi Cdm hawakuwa wanasiasa. Pita prof.lipumba wa cuf siyo mwanasiasa ndiyo mañana unaona uchaguzi mkuu ukiisha anarudi kwenye taaluma yake badala ya kujenga chama.

..kwasababu ya kukosekana kwa watu ambao wana WITO wa kweli wa siasa ktk vya upinzani kumepelekea vyama hivyo kudumaa kwa muda Mrefu.

..Cdm wamebahatika kwa na kiongozi kama Dr.Slaa ambaye ameweza kuchukua jukumu la kazi ngumu ya kujenga chama ktk mazingira magumu ya hapa nyumbani. Huyu mzee naweza kusema ni mmoja wa wanasiasa wa aina yake kupata kutokea tanzania. Kama huamini jiulize Kama kuna mwanasiasa yeyote yule wa rika lake angeweza kujenga chama kama alivyofanya Dr.Slaa.

..kuhusu uchaguzi wa mwaka huu ndiyo mara ya kwanza vyama vya upinzani vina nafasi ya kushinda.
 
Last edited by a moderator:
Uchakachuaji a.k.a goli la mkono! Hili ndilo tatizo kubwa. Mkipeleka mvinyo mpya kule ghalani keshoye utakuta wamechakachua na kuweka ule wa zamani! Sijui kama UKAWA wamejiamdaaje safari hii!
 
JK chali.......

Anatupimia kwa kijiko? Ataumia!

Hureeeeeee TeamLowassa!

Chezea mamvi weye! Kanikomesheaje kigeugeu wake na ka mic kake? Alidhani mamvi ni wa shambaeee? Mamvi nae wa mjini bana hajaijua shida toka kuzaliwa kwake etiiii.Chuo kikuu anamiliki gari na alikua akienda nayo chuoni. Mwanamme morani atateleza ila kuanguka chini nadra. Aliteleza ila huko huko kawekeza pia.
 
  1. kwa nini watanzania wameendelea kuuchagua Mvinyo Uleule wa CCM, kila unapowekwa kwenye chupa mpya?




  1. kwa nini wapinzani wa CCM wameendelea kuleta mvinyo wao kwa chupa zilizokataliwa ama kwa kutokuwa na mvuto au kuhisiwa kukosa ubora kama chupa za CCM?
  2. Kwa nini watanzania wanaendelea kukubali kunywa mvinyo wanaoulalamikia kwa miaka zaidi ya 30?na kuushangilia kila ukiwekwa kwenye chupa mpya, na kurudi tena kuulalamikia kila wakgundua mvinyo ni ule ule?
  3. Kwa nini wapinzani wanashindwa kuwaonesha watanzania Tatizo ni Mvinyo na sio CHUPA?

Kwa sababu ya ujinga tu. Otherwise how else would you explain it? Watu wana maisha magumu, kero chungu nzima, na kila aina ya adha ambazo zimekua na kushamiri chini ya uongozi wa chama hicho hicho tokea tupate uhuru lakini hata siku moja hawafikirii kubadili walau na kujaribu huko kwingine kuona kuna nini.

Na CCM wameshalijua hilo [na wala hauhitaji kuwa genius kulibaini hilo] na wameshaugeuza huo ujinnga kuwa ndo mtaji wao wa kisiasa.

Inasikitisha sana kuona watu ambao unadhani labda wamefanikiwa kufuta ujinga kwa kiasi fulani wakiingia mkenge na kuhemka kisa tu eti Magufuli ndo atakuwa rais.

Kwamba kwa sababu huwa anatamka takwimu za madaraja na sijui mabarabara yale [ambazo hata huwa hazithibitishwi na yeyote yule kama zina ukweli au la] basi eti jamaa ni jembe, ni kichwa, na kila aina ya sifa za kipuuzi puuzi.

Na katika uchaguzi wowote ule ambao mwamuzi/ msimamizi wake ni makada wa CCM [tume ya uchaguzi] wapinzani wasahau kabisa kuiondoa CCM madarakani.

Kwa sababu nimeshashawishika kuamini kwamba njia pekee ya kuiondoa CCM madarakani ni kupitia maasi ya umma kama ilivyotokea kule Misri na Tunisia. Lakini najua kabisa hilo hapa kwetu ni ndoto za alinacha.
 
Back
Top Bottom