We have seen it all by now. CCM party machinery at it's very best mesmerizing opponents and displaying the sheer power it holds over Tanzanian politics.
Kikubwa nilichokiona mimi binafsi ni jinsi gani Tanzania tunaendelea na zoezi la kuhamisha Mvinyo kutoka chupa moja hadi nyengine kila baada ya miaka kumi.
CCM ni mfano Hai wa taasisi Iliyowahi kuwa na Mvinyo Bora kuliko yote Afrika (Mfumo mzuri wa Uongozi wakati wa Mwalimu Nyerere), Na chupa yenye ubora na yenye kuvutia (Nyerere).
Baada ya miaka mingi ya kunywa mvinyo huu, wananchi wa TZ, waliukinai, wakaamua kutia maji ili kuulainisha ladha na kubadili chupa ya kuhifandia mvinyo ili kuufanya uvutie kwa wanywaji wa nje (mabepari na wawekezaji).
Kila baada ya miaka 10,mvinyo huu hubadilishwa chupa, na kuwekwa kwenye chupa mpya, huku wanywaji wakiambiwa kuwa mvinyo umeboreshwa kwa viwango vipya kabisa. Kiuhalisia kinachotokea ni kuwa mvinyo hubakia kuwa ule ule,uliotiwa maji, na unaoendelea kupoteza ladha.
Miaka kumi iliyopita, tuliletewa Chupa maridadi kweli kweli,tukiahidiwa kuwa, kwa kuwa chupa ni maridadi kimuonekano, basi hata mvinyo nao ni maridadi.sisi ni wepesi kuamini, tukaamini hivyo mara moja, haikuchukua muda mrefu kujua kuwa ingawa uliwekwa kwenye chupa maridadi, mvinyo huu ulikuwa bomu kweli kweli.labda bomu kuliko hat amvinyo tulionunua miaka ya kabla yake. manungu'iko yalivyoongezeka na mauzo ya mvinyo kupungua,wakazunguka nchi nzima kukusanya mvinyo wao wakiahidi miaka kumi ikitimia watahakikisha wanafanyia kazi maoni yetu na kutupatia mvinyo bora, kwani walishaanza kuona watu wameizoea hii chupa mpya.
Hivi punde muda wa kuleta mvinyo mpya umewadia, wapika mvinyo kama kawaida yao wamemaliza maonesho ya kunadi mvinyo wao kwa kuvumbua chpa mpya tena, huku wakiahidi kuwa chupa hii ni imara na bora kuliko chupa zilizopita.
Wengi wa wanunuzi wameshaanza kuingia "line" kununua mvinyo huu wa kufikirika baada tu ya kuona chupa,lakini daili zote zinaonesha kuwa mvinyo unaoletwa ndio ule ule tuliouziwa miaka kumi iliyopita. Hatujaona dalili zozote za kubadilisha mvinyo, hata mitambo inayotumika kuandaa mvinyo ni ileile, malighafi ni zile zile, na wapika mvinyo ni wale wale. Ila kwa imani yetu inayoendelea kutuangusha kila baada ya miaka 10 tumeendelea kukubali maneno yale yale kuwa mvinyo umeboreshwa,wakati hali haioneshi hivyo.
Pembeni ya CCM kuna taasisi kadhaa zilizoamua kuunda umoja wa UKAWA ili na wao wauze mvinyo wao kw awatanzania. Taasisi hizi mvinyo wao unasemekana kuwa mzuri,sema CHUPA zao hazina mvuto wa chupa za CCM. La kushangaza hawa mabwana ingawa hakuna ajuaye ladha ya mvinyo wao, zaidi ya kuupima kwa kutumia chupa uliyokuwemo, wameendelea kuleta mvinyo wao kwa kutumia chupa zile zile kila baada ya miaka kadhaa.Na hata sasa inasememkana wamekusanya chupa zao zoote za mvinyo zilizokataliwa huko nyuma ili kuchagua moja yenye afadhali, waje waiuze kwa wanywa mvinyo. Matumaini yao ni kuwa wakileta chupa moja iliyokataliwa labda itakuwa rahisi kuchaguliwa,kuliko wakileta chupa zote zilizokataliwa.
Umoja huu wamekuwa pia bize kuponda chupa za mvinyo kuliko kuponda mvinyo wenyewe, wakati wakifahamu wazi kuwa matatizo yanayolalamikiwa na wanywaji sio kwenye chupa bali kwenye mvinyo.
Chupa iliyovumbuliwa hivi karibuni imeshaanza kuundiwa mlolongo wa list kuonesha mapungufu yake,wakati wananchi wanahitaji kusikia mlolongo wa matatizo ya mvinyo utakaokusanya hiyo list.
CCM ni wajanja, wanajua chupa mpya matatizo yanajionesha baada ya muda sio kabla ya kununulika. Wapinzani wanaendelea kuamini kuwa matatizo ya chupa iliyopita yanaweza kuwekwa pamoja na chupa mpya.
Kwa kuwa Mvinyo wa CCM umeendelea kununulika kwa miaka nenda rudi, kila wakibadili Chupa, na Upinzani wameendelea kukaa kimya kuwaeleza wananchi kuwa wanauziwa mvinyo ule ule kwenye Chupa mpya, wananchi wameendelea kununua mvinyo wa zamani kwenye chupa wanazoletewa mpya kuliko kujaribu mvinyo usiojulikana ladha yake kwenye chupa walizozizoea kutoka upinzani.
Kwa kifupi chupa za upinzani zinafahamika, hazijawahi kushinda mvuto chupa za CCM, lakini wote tunakubali mvinyo wa CCM umeshajazwa maji kiasi cha kugeuka kuwa sawa na chai au juisi. Mvinyo wa upinzani hakuna anayeujua kwa kuwa unaendelewa kunadiwa vibaya,na kwa chupa zile zile.
Kilichotokea weekend hii ni CCM kuonesha chupa zake mpya za kuwekea mvinyo wao wa zamani, uliojaa maji na kukosa ladha.
Nikiwa kama mtazamaji wa haya maonesho napatwa na maswali mengi ya msingi nisiyo na majibu nayo.
- kwa nini watanzania wameendelea kuuchagua Mvinyo Uleule wa CCM, kila unapowekwa kwenye chupa mpya?
- kwa nini wapinzani wa CCM wameendelea kuleta mvinyo wao kwa chupa zilizokataliwa ama kwa kutokuwa na mvuto au kuhisiwa kukosa ubora kama chupa za CCM?
- Kwa nini watanzania wanaendelea kukubali kunywa mvinyo wanaoulalamikia kwa miaka zaidi ya 30?na kuushangilia kila ukiwekwa kwenye chupa mpya, na kurudi tena kuulalamikia kila wakgundua mvinyo ni ule ule?
- Kwa nini wapinzani wanashindwa kuwaonesha watanzania Tatizo ni Mvinyo na sio CHUPA?
cc:
Nguruvi3,
JokaKuu,
Pasco,
Mzee Mwanakijiji,
Zitto,
Tumaini Makene,
Zakumi,
Mkandara