Elections 2015 Dr. John Pombe Magufuli achaguliwa kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM 2015

Elections 2015 Dr. John Pombe Magufuli achaguliwa kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM 2015

Magufuli mbona amewaruka wakina sophia simba na Adam kimbisa hajawasalimu pale high table
 
Dr. Magufuli kama atachaguliwa na waTanzania ana kazi kubwa mbele yake . Maombi yangu kwa kama Utachaguliwa na WaTanzania
1. Mabadiliko Makubwa katika Utumishi wa Umma
inabidi afanye mabadiliko makubwa ndani ya serikali kuhakikisha tunasonga mbele. Asipofanya hivyo nasikitika ataanguka vibaya na ataangukiwa na chama. Kumbuka uwezekano wa yeye kutawala na bunge lenye 50/50 ama hata unpinzania >50 hali kwake kama rais itakuwa ngumu hivyo apange watu wasafi na watendaji serikalini vinginevyo atabadilisha mawaziri na makatibu wakuu kuliko hata JK

2. Kurudisha umoja kwa waTanzania. Ungozi unaoondoka uliifanya nchi ni ya watu wachache na wanaoamini hivyo kwamba wao nchi yao. Ilifika mahali watu wamejenga iman kuwa uongozi uliopo na CCM kwa ujumla walizaliwa na Tanzania mikononi mwao hivyo kuifanya yao. Hii dhana ni potovu na yanayojiri nchini mwetu sasa ni uthibitisho kuwa waTanzania tumejitambua kuwa wote tuna milki sawa katika nchi hii. Ifahamike hakuna aliyezaliwa na Tanzania mkononi sisi sote bila kuchagua tumejikuta Tanzania na hivyo tunahaki sawa katika nchi hii hivyo nafasi za uongozi, ajira, biashara na nyingine zote zifuate haki, uwezo, usawa, uwiano nk. Upendeleo katika kutoa fursa ni ugonjwa mkubwa nchin Tanzania na kama ambavyo ndiyo sababu kubwa ya mauaji ya kimbari hatutaepuka kama serikali yako haitayarekebisha. WaTanzania wameshajua hayo na wataendelea kuangalia, kukemea na kufuatilia wakishindwa kubadilisha haya kwa kura watafanya mabaya.

3. Rejesha kujiamini kwa nchi kwa kuondoa Uwakala na ukuwadi kama mbinu kuu ya kipato- Ni ukweli usiopingika kuwa Utajiri wa WaTanzania wengi kwasasa unatokana na ukuwadi kwa wanansiasa na ndugu/jamaa rafiki zao na uwakala kwa watumishi wa umma. Ushabiki wa siasa na vyama unakua kwa kasi kwa kuwa imejidhihirisha nchini kwetu kuwa ili uwe na neema lazima uwe ema kuwadi ndani ya CCM na serikali ema wakala ndani ya serikali. Kama haupo katika makundi haya mawili basi na hutakula wewe na vizazi vyako. Hili si sihahihi na si hulka yetu. Tusijenge maadili ambayo si yetu na kuyahalilisha kwa vile tuu tumejenga jamii isiyotaka kufanya kazi bali kuneemeka kwa ukuwadi na uwakala. Ni ukweli usiopingika tunamipango na mifumo ya serikali mizuri sana lakini hatusogei kwa kasi kama tulivyotarajia kwasababu watumishi wa umma wamekuwa makuwadi na mawakala wa matajiri na wageni. Wao ni magolokipa ndiyo wanaoamua mradi upi uende kwa nani na kwa gharama gani na kwa njia gani. Pamoja na mishahara midogo hawataki kutoka na hata sisi tulio nje tunalilia kurudi serikalini. Mgeni yeyote anayekuja nchini na kuulizia fursa za kuwekeza watumishi wa umma wamekuwa mawakala wa matajiri na kuhakikisha ni pale tuu watakapopata chochote ndiyo mradi huo utatekelezeka. Dr Magufuli ridhaa yetu waTanzania ikupe nguvu usafishe uchafu huu. Ikiwezekena anza upya na watumishi wapya wa umma pitisha fagio chunguza wangapi wanautajiri wa kupita kipimo? bahati mbaya waTanzania tunaona uchafu na uozo kwa wanasiasa tuu lakini tumewaacha watumishi waumma hawa ndiyo adui mkubwa wa maendeleo ya watanzania. Tukiweza kurekebisha hapa tutatoka kama nchi. Usiwe kama rais JK ambaye amekuwa analalamikia watendaji wakati yeye ndiye amewaajiri wewe rudisha heshima kwa kuwwajibisha vinginevyo hakuna chama hata iwe upinzani itatekeleza ilani yake kama hakutakuwa na mabadiliko katika utumishi wa umma. Jenga hulka ya watu kuheshimu na kuogopa kwenda kwenye utumishi wa umma kwa kupafanya patakatifu na siyo pango la makwadi na mawakala.

Dr. Magufuli utaweza kufanikiwa kurejesha heshima kwa utumishi wa umma kwa kuboresha mfumo wa uteuzi kuzingatioa taaluma, uwezo, maadili na uwiano kuhakikisha waTanzania wote wanauwezo wa kuingia utumishi wa umma. Ni ukweli usipoingika kuna baadhi ya waTanzania hawamo katika utumishi wa umma wala kwenye biashara wala kweny fursa nyingine. Tupende tusipende ukabila, udini, ukanda, uchama, urafiki; ni vigezo vinavyotumika sana katika ajira, kupata fursa za uchumi etc. Dr. Magufuli tuko makabila 123 na zaidi na sote ni waTanzania na ni haki sote kuwemo na kupata fursa. kwa vile ukoloni ulijenga matabaka kwa dini, kabila, na nafasi tuendelee kurekebisha haya kuhakikisha hakuna Mtanzania anabaki nyuma kwasababu ya historia. Pato la Taifa lisiendekeze mazao ya bishara yale ambayo tuliachiwa na wakoloi haya ndiyo yanayoendeleza kutugawa kwani wale ambao wakuwa na mazao ya bishara wataendelea kupata mgawo mdogo wa bajeti na hivyo kuendelea kurudi nyuma ama kubalki walipo.

D. Magafuli linda Tanzania endeleza kujenga Taifa la watu wenye uwezo na maadili kuweza kutoa ushindani ndani na nje ya nchi. Jenga Taifa lenye hofu ya Mungu na si hofu ya fedha. Wewe ni uzao wa uthibitsho kuwa palipo MUNGU Fedha haina nafasi. Kama fedha ingekuwa ni kila kitu, wewe usingeteuliwa kuwa Mgombea wa CCM.

Hakikisha unazungukwa na marafiki, ndugu, jamaa na wanasiasa wenye uwezo na maadili wengine achana nao mbinu zao zimepitwa na wakati waTanzania wanaendelea kukataa kugeuzwa kitovu cha fedha inaongea.

Rudisha amasa ya kufanya kazi kwa vijana na waTanzania kwa ujumla. Inasikitisha kuona kwamba vijana wengi waTanzania wanaona siasa ni shighili kubwa ya kiuchumi. Dr Magufuli jenga vivutio kwa vijana jutoa nguvu kutoka siasa na kuzielekeza kwenye uzalishaji. Kuwa na shughuli ya kipato na mchango wake kuleta ajira viwe vigezo vikubwa kwa vijana kuingia kwenye siasa ili vijana wetu wasipotee na kuwa wanasiasa wenye kuganga njaa kama ilivyo sasa.
 
Ukawa tupambane tu tupate wabunge wengi zaidi tulikamate bunge
 
1. John magufuli kura 2104 %87.1
2. Rose migilo kura 59 %2.4
3. Amina salumu kura 253%10.5
ZilizoPigwa 2422
Haribika 6
Halali 2416

Hivyo magufuli ndio mgombea urais

UKAWA ijipange otherwise they will stay
 
UKAWA walete mgombea mpya ili kushindana na huyu jamaa
 
1. John magufuli kura 2104 %87.1
2. Rose migilo kura 59 %2.4
3. Amina salumu kura 253%10.5
ZilizoPigwa 2422
Haribika 6
Halali 2416

Hivyo magufuli ndio mgombea urais

UKAWA ijipange otherwise they will stay

Hoho ngenge raraaaaaaaaa!
 
Back
Top Bottom