Mgombea mteule wa CCM, Mh Magufuli ameonyesha uwezo wa hali ya juu kiutendaji akiwa waziri zaidi ya Mzee Lowasa katika kipindi chake akiwa waziri. Mh Magufuli ameonesha uthubutu katika majukumu yake ktka wizara alizopita. Wote hawa wawili wamelitumikia taifa hili katika nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Uwaziri. Kati ya hawa wawili mmoja ambaye ni Magufuli kote alikopita ameweka record ya kipekee kiasi cha kuwafanya wananchi wengi kutamani apewe majukumu makubwa zaidi.
Mh Makufuli, amekua tunu hata wizara nyingine alizokwenda nakumfanya ang'are zaidi tofauti na mzee Lowasa katika wizara zote alizopita hakuna jipya alilolifanya zaidi ya kuacha malalamiko ya kero mbalimbali. Mh Magufuli ndiye aliyeokoa upotevu wa magari ya miradi ya serikali ambayo watumishi wengi walikua wakijimilikisha magari hayo na kuyatumia vibaya kwakua yalikua na namba za kiraia na baadae akaanzisha program kuweka namba mpya za magari yote ya serikali, Mh Makufuli akiwa wizara ya ujenzi watanzania tumempongeza sana na kwa juhudi,uboreshaji wa miundo mbinu kama barabara za kisasa, hakika huyu ndio kiongozi tunaemhitaji kwa sasa.
Mh Magufuli alipambana na wavuvi haramu waliokua wanatumia mabomu na nyavu haramu ijapokua wengine wachache walimchukia lakini wanaichi wengi tumempongeza kwa kazi nzuri hata akiwa wizara ya mifugo
Magufuli mara nyingi ameonekana akiwa sites mbalimbali za ujenzi akisimamia shughuli zinazofanyika iwe usiku au mchana akishirikiana na sisi wanainchi.Hakika huyu ndiye kiongozi tunaehitaji kwa sasa.
Jimboni kwake Mh Magufuli kupo vizuri barabara za lami,shule,ujenzi vituo bora vya afya na amekuwa karibu sana na wanainchi wake ukilinganisha na babu yetu Lowasa kule Monduli. Babu katika kipindi chake wizarani ametumia fulsa hiyo kujilimbikizia mali,kufanya biashara haramu na mataifa ya Ulaya, alijikita katika kutengeneza makundi yasiyokuwa na tija kwetu sisi wanainchi na zaidi kutuongezea umasikini.Kama wazalendo tujiulize huyu babu anaedai kuchukia umasikini,katengeneza ajira ngapi kwa vijana wa Monduli?
Zaidi ya maigizo anayofanya makanisani na misikitini,atueleze ni bodaboda wangapi kawapa mitaji zaidi ya kuwaburuza hususani wale wasiojitambua,vijana wengi wa kimasai kawapa fursa kiasi gani zaidi ya kukimbilia Dar es Salaam?. Kwa miaka zaidi ya 20 akiwa kiongozi hajaonesha nia ya dhati ya kumkomboa kijana,ataweza vipi kwa sasa na uzee unaomkabili ukiachilia maradhi anayokabiliana nayo. Alipokua waziri Mkuu Wafuasi wake wamekua wakimpongeza sana kwamba anamaamuzi magumu ambayo kama ni shule za kata zimechangiwa na wanainchi chini ya ilani ya chama cha CCM,yeye alikuwa na jukumu la kusimamia zoezi hilo tu.
Jimboni kwake kwenyewe hakuna maendeleo yeyote yale maisha ni magumu sana kuliko majimbo mengine.
Zaidi ya kujilimbikizia mali hakuna jipya alilofanya mzee Lowasa pamoja na kupendwa na bodaboda wachache wasiojitambua maana ukiwauliza kwanini wanampenda w atakujibu basi tumempenda tu" Ahahahaaaa mwengine watakujibu kuwa wanataka mabadiliko sasa hebu jiulize mabadiliko gani atakayokuletea wakati Jimboni kwake kwenyewe ni njaa tu!!!