Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aliyekutuma kuandika gazeti mwambie watanzania wameamua kuchagua Lowassa.
Ni jamii iliyochoka na kuchakaa; ni jamii iliyooza na kuchoma pua kwa harufu ya uvundo wa rushwa na kujaza nzi wakubwa wa rangi ya Kijani, Ni jamii yenye ufisadi na ukandamizaji; ni jamii isiyojua mbele wala nyuma, ni jamii iliyokosa dira. Bunge lipo kwa jina tu kwa sababu limewekwa kwapani na watawala; Madaraka ya Rais ni makubwa kwa kiwango cha kupora demokrasia: Utajiri wa nchi upo mikononi mwa kikundi kidogo cha wateule na watawala kilichowageuza wananchi wadunda kazi wasiofaidi jasho lao. Na pale maandamano ya wanawake, wanaume na vijana wenye njaa yanapopita karibu na Makazi ya Wenye nacho,Malodilofa husimama ghorofani, wakawatazama na kuuliza, kulikoni?. Na walipoambiwa kwamba yalikuwa ya malofa wenye njaa waliokosa mkate wa kila siku, wao walijibu: Kama ni hivyo, kwa nini wasile nyasi na mihogo?Vijana wanaangamia kwa kukosa maarifa mashuleni na wanaishia kubwia "unga" ambao ni biashara pendwa ya Malodilofa,vijana wasanii wenye vipaji mbalimbali wanageuka ombaomba na wakati wa Kampeni wanakuwa "lulu" kwa kutumika kujaza nyomi katika mikutano,wakulima wanazeeka kwa kazi ngumu mashambani na kukosa pembejeo za kisasa na mazao yao yanaishia kukopwa kwa bei ndogo ajabu,wavuvi wanachomewa nyavu zao walizonunua kwa wafanyabiashara wajanja wenye meno,wawindaji wa vitoweo wanaambiwa ni majangili huku tembo wakiuwawa kwa tama ya meno yao na twiga wakipandishwa ndege kwenda ulaya na Asia..Dah! wagonjwa wanakufa huku wamelala mzungu wanne sakafuni mahospitalini kwa kukosa madawa,wakina mama wanajifungulia vichochoroni kwa ubovu wa barabara, Na wanapoona malofa wanawapigia kelele kwa madai yao sahihi wanaamuru majeshi ya ndugu zao wanyonge wawapige mabomu ya machozi na kuwaua na kuwasababishia vilema vya maisha na kuwatesa waandishi wa habari zao za kilofa.Watawala wetu hivi leo wanatuhumiwa kumiliki mabilioni ya fedha wanayomiliki huku wakiyaita ni vijisenti, au fedha ya mboga, wakati kipato cha Watanzania walio wengi ni chini ya shilingi mia nane kwa siku. Wananchi wanapopiga kelele kugugumia bei kubwa ya kivuko wanaambiwa Wapige mbizi na pale ndege ya Rais na rada chakavu inaponunuliwa kwa pesa nyingi zenye asilimia kumi za wajanja wanaambiwa Ni heri wale nyasi Pamoja na mikakati mikubwa na yakutumia fedha na rasilimali nyingi za walala hoi kwa ajili ya kuvuruga "Mabadiliko" kwa kuwanunua wanasiasa uchwara na kuwakashfu kuwa ni wapumbavu,amlofa na mbumbumbu. Wakati umefika,chama kilichokuwa na dhamana ya haya yote kipumzishwe,ili kijitafakari,kitakapokuja kwa mara nyingine (MUNGU akikijaalia) kije kikiwa kamili....Kwa wakati huu,nathubutu kusema,Naichagua UKAWA,...sio kwa sababu za uimara wa CDM,CUF,NLD,NCCR MAGEUZI ama Uimara wa UKAWA la hasha!!Ila ni kwa sababu ya udhaifu wa CCM na ahadi ilizoshindwa kuzitekeleza kwa miaka 54 mfululizo.ALUTA Continua, Victoria Ascerta.... The Struggle Continues, Victory is Certain; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!! ≠HapaNimakwenziTu!!
Mgombea mteule wa CCM, Mh Magufuli ameonyesha uwezo wa hali ya juu kiutendaji akiwa waziri zaidi ya Mzee Lowasa katika kipindi chake akiwa waziri. Mh Magufuli ameonesha uthubutu katika majukumu yake ktka wizara alizopita. Wote hawa wawili wamelitumikia taifa hili katika nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Uwaziri. Kati ya hawa wawili mmoja ambaye ni Magufuli kote alikopita ameweka record ya kipekee kiasi cha kuwafanya wananchi wengi kutamani apewe majukumu makubwa zaidi.
Mh Makufuli, amekua tunu hata wizara nyingine alizokwenda nakumfanya ang'are zaidi tofauti na mzee Lowasa katika wizara zote alizopita hakuna jipya alilolifanya zaidi ya kuacha malalamiko ya kero mbalimbali. Mh Magufuli ndiye aliyeokoa upotevu wa magari ya miradi ya serikali ambayo watumishi wengi walikua wakijimilikisha magari hayo na kuyatumia vibaya kwakua yalikua na namba za kiraia na baadae akaanzisha program kuweka namba mpya za magari yote ya serikali, Mh Makufuli akiwa wizara ya ujenzi watanzania tumempongeza sana na kwa juhudi,uboreshaji wa miundo mbinu kama barabara za kisasa, hakika huyu ndio kiongozi tunaemhitaji kwa sasa.
Mh Magufuli alipambana na wavuvi haramu waliokua wanatumia mabomu na nyavu haramu ijapokua wengine wachache walimchukia lakini wanaichi wengi tumempongeza kwa kazi nzuri hata akiwa wizara ya mifugo
Magufuli mara nyingi ameonekana akiwa sites mbalimbali za ujenzi akisimamia shughuli zinazofanyika iwe usiku au mchana akishirikiana na sisi wanainchi.Hakika huyu ndiye kiongozi tunaehitaji kwa sasa.
Jimboni kwake Mh Magufuli kupo vizuri barabara za lami,shule,ujenzi vituo bora vya afya na amekuwa karibu sana na wanainchi wake ukilinganisha na babu yetu Lowasa kule Monduli. Babu katika kipindi chake wizarani ametumia fulsa hiyo kujilimbikizia mali,kufanya biashara haramu na mataifa ya Ulaya, alijikita katika kutengeneza makundi yasiyokuwa na tija kwetu sisi wanainchi na zaidi kutuongezea umasikini.Kama wazalendo tujiulize huyu babu anaedai kuchukia umasikini,katengeneza ajira ngapi kwa vijana wa Monduli?
Zaidi ya maigizo anayofanya makanisani na misikitini,atueleze ni bodaboda wangapi kawapa mitaji zaidi ya kuwaburuza hususani wale wasiojitambua,vijana wengi wa kimasai kawapa fursa kiasi gani zaidi ya kukimbilia Dar es Salaam?. Kwa miaka zaidi ya 20 akiwa kiongozi hajaonesha nia ya dhati ya kumkomboa kijana,ataweza vipi kwa sasa na uzee unaomkabili ukiachilia maradhi anayokabiliana nayo. Alipokua waziri Mkuu Wafuasi wake wamekua wakimpongeza sana kwamba anamaamuzi magumu ambayo kama ni shule za kata zimechangiwa na wanainchi chini ya ilani ya chama cha CCM,yeye alikuwa na jukumu la kusimamia zoezi hilo tu.
Jimboni kwake kwenyewe hakuna maendeleo yeyote yale maisha ni magumu sana kuliko majimbo mengine.
Zaidi ya kujilimbikizia mali hakuna jipya alilofanya mzee Lowasa pamoja na kupendwa na bodaboda wachache wasiojitambua maana ukiwauliza kwanini wanampenda w atakujibu basi tumempenda tu" Ahahahaaaa mwengine watakujibu kuwa wanataka mabadiliko sasa hebu jiulize mabadiliko gani atakayokuletea wakati Jimboni kwake kwenyewe ni njaa tu!!!

Watanzania tunaimani kubwa na Magufuli na sio hao mafisadi