Toa sababu ya kumchagua Lowassa., mimi natoa za kumchagua Magufuli.
Sababu za kumchagua MAGUFULI.
1. Magufuli ni mchapa kazi nadhani wizara ya ujenzi unaiona jinsi ilivyo kuwa mbele"
A: Ni kweli barabara zote alizojenga ziko chini ya kiwango na nyingi zilibomoka hata kabla ya kuzinduliwa na ameliingiza taifa hasara ya takribani billioni 900 ambazo ni riba au faini kwa kushindwa kuwalipa wakandarasi kwa wakati. saafi sana
2. ni mtu asie na kundi lolote na huwa anasimama yeye kama yeye katika kila linalo muhusu"
B: Binadamu is a social being, katika maisha yetu ya kawaida ni lazima tuchanganyike na kushirikiana, usiri na ubinafsi wa Magufuli ni tabia ya watu wahalifu wasiopenda watu wengine waujue undani wao; wanajipa social distance kupunguza uwezekano wa mtu kuhoji hili na lile! utamuanzaje hamuzoeani?! magufuli huyoo!
3. kielimu huwezi fananisha Magufuli na Lowassa sababu Magufuli ni mkemia lakini lowassa ni msanii maana degree yake ni ya sanaa''
C: Uliwahi kusikia wapi shahada ya kuwa Rais; a president is a manager, managers use brains not misuli na jazba! managers are born and groomed, unlike Nyaparas; kutumia Nguvu nyingi kuliko akili, matokeo yake ni kuliiingiza taifa kwenye hasara kama vile meli ya samaki wa Magufuli!
4. Anaposimama jukwaani anaeleza kitu kwa mifano hai na kwa kusisitiza na huwezi fananisha sera zake na mgombea wa ukawa ambae hawezi hata kueleza back ground ya maisha yake ndani ya siasa.
D: Political novices kama magufuli ambaye hajawahi hata kuwa mwenyekiti wa tawi la CCM popote; hata shina! ndio wanahitaji kujieleza na kujipigia tarumbeta kila mara na kila mahali; sio a political GIANT kama EL ambaye track record yake inajieleza yenyewe loud and clear; amejijengea "political constituency" yake kwa miaka mingi sana; haitaji kujipigia tarumbeta; No wonder EL is a man "political novices" love to hate!
5. Chama chake Magufuli alichotoka bado hakijafarakana hivyo ni jambo jepesi hata kuunda baraza la serikali mpya na haiwezi fananishwa na ukawa ambapo wanaotegemewa wamekikimbia chama na kubakiza watu wasio waelewa maana hata nyumba kumi hawawezi kuongoza hivyo utajikuta baraza linajazwa na akina mnyika wasio na kauli wala nidhamu hata wawapo bungeni.Hii inatukumbusha kuwa tukiwapa utawala ukawa basi serikali itapambwa na mafisadi waliokimbia ccm.
E: Hujui unachoandika, ni wa kudharau tu wewe! kumbe hukusikia kauli hizi:
"CCM tunapambana na CCM maslahi upande mmoja na UKAWA kwa upande mwingine"! Samia Suluhu mgombea mwenza Urais 2015 na Muuaji Mwenza wa katiba ya wananchi BMK 2014.
"Najua kuna watu wananiunga mkono mchana kwenye kampeni zangu lakini usiku wanapigia kampeni UKAWA" John Magufuli; mgombea wa CCM urais 2015 akiwa mkoani Kagera
"Nimeachana na Siasa na sitarajii kupanda tena jukwaani kumuunga mkono John Magufuli". Makongoro Nyerere; Msasani kwa Mwalimu September 2015
Nawewe toa sababu ya kumchagua Lowassa.