Elections 2015 Dr. John Pombe Magufuli anafaa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania

Elections 2015 Dr. John Pombe Magufuli anafaa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania

Hafai kwa sababu ya maamuzi yake ya kukurupuka yalolitia hasara taifa,fisadi kwa mujibu Wa report ya cag,kauza nyumba za taifa,mikataba mibavu ya barabara,barabara chin ya kiwango,ubabe ktk ndoa na siasa,anatetea mambo ya kijinga kama safari za rais,hasikiliz ushauri,amekaa ktk chama fisad
 
Kiongozi wakweli ni yule anayekuwa na Hofu ya mungu na kuweza kujali wanzake kwa kuwapa haki yao, Tanzania ni muda mrefu sana hatujapata kiongozi ambaye anaweza kujitoa kwa ajili ya watu wengine lakini kwa sasa tunamshukuru mungu kwa kutupa kiongozi mzuri Dk.Magufuli kwa kutupa matumaini ya kuirudisha hii nchi kwenye misingi ya Maendeleo bora na Haki kwa kila mtanzania, Vigogo Wanasiasa ambao wamelifanya ili Taifa kama Shamba la BIBI kuchuma wanavyotaka na kuwaancha wananchi wakikosa msaada na wazalengo.

Magufuli tunakushukuru kwa kutupa matumaini mapya na tumekuona kwenye wizara nyeti ya Ujenzi wa Hii nchi na umekuwa mwadilifu na mchapakazi bora kwa kweli wewe kama Rais ajae utaweza kurudisha hii nchi kwa Watanzanial.

Hongera sana TINGATINGA TUNAOMBA BAADA YA TAREHE 25 UKIWA RAIS HAKIKISHA VILE VIPAUMBELE VYAKO TUNAVIONA KWA KWELI KAMA ULIVYOTUFANYIA KWENYE UVUVI, TANROAD, NA BAADHI YA HUDUMA ULIZOZIPIGANIA.

Hapo ndipo sikuelewi sababu huyu ndiye aliyewambia wale maskini wa Kigamboni wasipokuwa na TZs200 wapige mbizi.Ndiye huyu huyu aliyewaambia wale watanzania wa Biharamulo kama wanatka LAMI wasambaze KINYESI chao ili kiwe lami.

Leo unaniambi huyu ndiye anayejali maisha ya watanzania kwa maneno yake haya MACHAFU kwetu sisi walalahoi tunasema hakika hafai kupewa hiyo sifa.
 
Kiongozi wakweli ni yule anayekuwa na Hofu ya mungu na kuweza kujali wanzake kwa kuwapa haki yao, Tanzania ni muda mrefu sana hatujapata kiongozi ambaye anaweza kujitoa kwa ajili ya watu wengine lakini kwa sasa tunamshukuru mungu kwa kutupa kiongozi mzuri Dk.Magufuli kwa kutupa matumaini ya kuirudisha hii nchi kwenye misingi ya Maendeleo bora na Haki kwa kila mtanzania, Vigogo Wanasiasa ambao wamelifanya ili Taifa kama Shamba la BIBI kuchuma wanavyotaka na kuwaancha wananchi wakikosa msaada na wazalengo.

Magufuli tunakushukuru kwa kutupa matumaini mapya na tumekuona kwenye wizara nyeti ya Ujenzi wa Hii nchi na umekuwa mwadilifu na mchapakazi bora kwa kweli wewe kama Rais ajae utaweza kurudisha hii nchi kwa Watanzanial.

Hongera sana TINGATINGA TUNAOMBA BAADA YA TAREHE 25 UKIWA RAIS HAKIKISHA VILE VIPAUMBELE VYAKO TUNAVIONA KWA KWELI KAMA ULIVYOTUFANYIA KWENYE UVUVI, TANROAD, NA BAADHI YA HUDUMA ULIZOZIPIGANIA.

Angekuwa Mzalendo angewambia wakazi wa kigamboni kama Hawana shilingi 200 ya kivuko wapige Mbizi?

Jamani watanzania wenzangu tusiwe Wapumbavu kiasi hicho, cha kushabikia Mambo Ambayo yatakugharimu kwa miaka 5.

Kama unataka kupigishwa Mbizi ya Maisha Basi Mchague Magufuli, lakini kama unahitaji Mabadiliko ya kweli na utendaji usio kuwa wa mazoea, chagua Lowassa.

Jamani badilikeni tuliaidiwa Maisha bora kwa kila mtanzania. Yapo wapi zaidi ya Maisha mabaya kwa kila mtanzania?

Kura yako Maisha yako ndugu zangu, tumelaghaiwa kwa miaka 50 utajiri wa nchi hii unamilikiwa na kikundi cha watu wachache huku watanzania wakifa maospital kwa kukosa madawa!

Hata Mungu Atatushangaa tukiichagua tena ccm!
 
Uadilifu ni kitu muhimu sana na kimeonekana dhahiri pasi shaka kwa Hon. JPM katika maamuzi yake murua ya uuzwaji wa nyumba za serikali, ubomoaji wa jengo la TANROAD, kituo cha kuuza mfuta cha kule Mwanza na dhamila ya kubomoa jengo la TANESCO, kukamatwa meli na wavuvi wa samaki kwenye bahari ya kina kirefu na ushuhuda wa CAG report kuhusu mabilioni yasiyoonekana wizara ya ujenzi. hakika kwa yote hayo ndiyo utumishi uliotukuka kwa maoni ya upande wa pili.
 
Magufuli hana mpinzani kwa kuwa sifa zote za Kuwa kiongozi wa nchi hii anazo na watanzania wengi wako nyuma yake,hapa kazi tu,mtaelewa tu kuwa huyo ni chaguo la Mungu na mtashindana naye lakini hamtamshinda john pombe Magufuli
 
Nitampa kula dr magufuri
 
Attachments

  • 1443778790676.jpg
    1443778790676.jpg
    54.5 KB · Views: 56
Education profile ,background yake ya uongozi katika sector mbalimbali zinaonyesha kuwa anafaa kuwa raisi...compare to other competitors
 
Magufuli hafai .kua rais na cm Yale hatuwataki.namanafiki yakutupwa
 
Vijana msikubali kutumiwa vibaya na baadhi ya wanasiasa kwa maslahi ya watu wachache huku hao wanaowatumia wanasonga mbele kimaendeleo na vijana wanazidi kurudi nyuma.

Kijana, mchague Dr. John Pombe Magufuli anatambua umuhimu wa vijana ambao ni kundi kubwa la nguvu kazi nchini. Anauwezo mkubwa wa kuisimamia ilani anayoitangaza kwenye kampeni za urais kwa kuhakikisha Halmashauri zote nchini zinaendelea kutenga, kurasimisha, kupima na kuyawekea miundombinu maeneo maalumu ya vijana kwa ajili ya shughuli za uzalishaji mali ktk sekta mbalimbali hususan kilimo, ufugaji, madini, viwanda vidogo vidogo, uvuvi, mwasiliano na biashara.
 
Nawasifu Watanzania kwa kuwa na uelewa mpana wa kuweza kung'amua mambo na kuacha kufuata mkumbo. Dr. Magufuli kitakachomfanya kuwa Rais bora hata kuliko baadhi ya waliomtangulia ni MZALENDO, MCHAPAKAZI, MWADILIFU, MTENDAJI NA SI MTU WA POROJO. Magufuli anachoahidi kukifanya anakifanya tena kwa ufanisi. Rekodi yake ya utendaji ni nzuri na ya kutukuka hivyo ana kila sababu ya kuingia Ikulu na kuwa kiongozi na si mtawala. Magufuli hana makundi kwa hiyo atafanya kazi bila kumwangalia mtu usoni. Pia hana waliombebna kumpeleka Ikulu, atapelekwa na wananchi. Lakini tukija kwa Lowassa ni kinyume cha haya. Ila kazi anachapa lakini kwa lengo la manufaa yake mwenyewe. hivyo Lowasa hatufai ng'o!
 
Back
Top Bottom