Pelekaroho
JF-Expert Member
- Sep 15, 2010
- 1,601
- 375
Kwa sasa tulipofikia kama taifa tunahitaji rais mwanasayansi,tunahitaji rais mwanasayansi kwa sababu zifuatazo.
Kwanza Tanzania tunahitaji kukua kwa yanja ya kisayansi na ili kuendelea katika sekta za viwanda na teknolojia TUNAHITAJI MTUMFUATILIJI MWENYE TAALUMA YA KISAYANSI.
Pili dunia ya sasa ni ya sayansi na teknolojia hivyo tunahitaji rais mwenye hiyo taaluma ya kisayansi ili aweze kuhakikisha kuwa taaluma yake inakuwa katika viwango vya kimataifa na kusababisha maendeleo yanayo tokana na sayansi.
Tatu tangu nchi hii uimbwe haijawahi kuwa na rais mwanasayansi
Rais wa awmu ya kwanza alikuwa ni mwalimu
Rais wa awamu ya pili alikuwa ni mwalimu
Rais wa awamu ya tatu alikuwa ni mwahahabari
Rais wa awamu ya nne ni mchumi.
Rais wa awamu ya tano tunamtaka rais ambaye ni mwanasayansi, sasa ni zamu ya mwanasayansi
maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa Tanzania kwa viwango vya juu zaidi yataletwa na rais mwanasayansi na siyo muugizaji au mwana sanaa aliyo bobea katika taaluma fani yake.
Hizo zamu za urais anayepanga ni nani? Unadhani makundi hayo uliyoyataja pekee ndo yanatakiwa kutoa rais? Vipi kuhusu makundi mengine kama wanasheria, wahandisi, madakitari na makundi mengine mengi ambayo kwa sasa siwezi nikamaliza kwa kuyataja hapa lakini labda kundi jingine muhimu ni la watu wasio soma.
Kundi hilo la mwisho, yaani la watu wasiosoma, siyo kundi la kubeza kwa sababu hata katika jamii tunamoishi wapo watu ambao hawakusoma lakini wamefanikiwa saana kimaisha. Mfano mmoja wa haraka ni aliyekuwa rais wa Brazil, Da Silva, hakusoma lakini katika kipindi chake cha utawala ndipo Brazil ilifanya mapinduzi makubwa saana ya kiuchumi.
Uongozi ni karama, na wala kiongozi mzuri hatokani na elimu yake, bali uongozi ni kipaji kutoka kwa Mungu mwenyewe. Hatuhitaji mwanasayansi tunahitaji kiongozi.