Dr. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji wa NECTA! "It's Time To Go!.

Nivea nakubaliana na wewe, angalia katika sababu zangu hiyo namba 1. inaendana na ulichosema
 
shule hazina walimu

shuke hazina madarasa ya kutosha

shule hazina maabara

shuke hazina vitabu

hakuna mitaala



 
I beg to differ, watoto siku hizi hawasomi kutwa kwenye facebook,youtube asa atasoma saa ngapi kama hajui kumanage muda wake vizuri lazima afeli tu hilo ulilosema watoto walionacho ndo wamefaulu si kweli , jitihada binafsi za mwanafunzi ndo zita determine matokeo Dr Ndalichako hahusiki na lolote wanafunzi wanambwelambwela tun hata hasomi kabisaa
 

Pasco kwa kizazi hiki ambacho wasomi hamkuwaandaa wazazi wao kukabiliana na Dr. Ndalichako hata upewe wewe kitengo hicho cha Dr. Ndalichako naamini mambo yatakuwa mabaya zaidi
 
Last edited by a moderator:
Mkuu bado nashindwa kulielewa hili Bandiko...
Ila binafsi nikiwa kama mmoja wa wanafunzi wa zamani, nimeyatazama matokeo haya kwa namna tofauti kidogo.
Moja kwa moja ni ngumu kutambua ni nini chanzo cha matokeo mabovu, lakini nadhani kuna mambo mawili matatu ambayo huenda ndio yakawa chanzo.
1. Aina ya utunzi wa mitihani umezingatia uelewa kuliko kukariri (Mwenye kuelimika ndiye ataye faulu).
2. Kuna uwezekano pia mitihani ilikuwa ni migumu (Wanafunzi walikomolewa). Ukijaribu kuangalia idadi ya wafaulu wa daraja la kwanza utaona ni wanatahiniwa wachache mno waliofaulu kwa kiwango hicho.
3. Wapo wanaodhani kuwa mfumo wa utandawazi na teknohama pengine umechangia kwa asilimia kubwa, ila binafsi naamini hiyo sio sababu haswa ya msingi. Jaribu kuangalia matokeo ya shule zilizofanya vizuri Kitaifa mathalani St. Fransic, Marian Girls n.k(Hizi shule wanafunzi wao huwa hawa-interact na outside world)...utagundua kuwa kwa wastani shule hizo zimefanikiwa kufaulisha wanafunzi kwa kiwango kikubwa, lakini sasa kiwango cha ufaulu kwa watahiniwa wa Daraja la Kwanza, ni wa wastani mno...si kama tulivyozoea miaka ya nyuma kuona ufaulu wa Division I zile za "single digit" zikiwa za kutosha.
 

Mkirua teh teh usinitoe macho. Hapo nimetoa baadhi ya sababu ambazo zinaweza kufanya watoto wafeli. Sasa kwa Baraza na Wizara kuangalia sababu moja au mbili tu hapo siyo sahihi. Kuhusu maandamano kuzuilika ndugu mimi siyo mtabiri.

Kuhusu vitabu ni kwamba kama Wizara inatoa vitabu vya msingi, ambavyo walimu na wanafunzi wanatumia muda kuvisoma unategemea pia hata maswali ya kuwatahini mengi yatatoka humo. Unaweza kuongeza machache kutoka sehemu nyingine ili kujenga utamaduni wa kujisomea zaidi ya vitabu vya Wizara. Sasa kwa kiwango gani mitihani iliyotungwa iliwiana na hilo, hicho ni kitu ambacho Baraza na Wizara walitakiwa waseme. Siyo sisi kuja kuspeculate hapa. Na wasiwasi wangu unakuja maana mitaala yenyewe bado inagombaniwa kuwa haijakaa sawa (rudia sakata la Mbatia bungeni)
 
Hivi jamani huyo Dr. Joyce Ndalichako, ndiyo mtungaji na msahihishaji wa hii mitihani? tusikurupuke na kuanza kuongea tu na kufurahisha midomo yetu.
 

siku hizi mtoto wa darasa la nne anamiliki Blackberry kali kuliko ya ticha anaangalia picha za ngono.
 
Tutamfukuza. Tutaleta anaeendana na Kawambwa.
Elimu itabaki pale pale mbaya.
Mitihani itaonekaka mtaani a month before
Huku wewe Pasco ukiwa among people who will solve the paper and sell to these kids.
Hawa watafanya vizuri mitihani na tutafurahi sote.
Lakini je huko mbele watakapoelekea hali itakuwaje?
Sio kama wazazi wanafurahia kuonekana wanacho kwa kupeleka watoto katika shule za binafsi. Wengi wao wanajinyima kwa sababu wanajua atleast kule watoto wao watapata elimu bora.
Sasa unataka huyu mama atunge mtihani ya la saba kwa form four?? Ikiwa serikali imeamua asiyejua kusoma na kuandika aelekee form one. Unataka nae huyu afaulu form four kwa mtihani wa aina gani??
 
Hivi jamani huyo Dr. Joyce Ndalichako, ndiyo mtungaji na msahihishaji wa hii mitihani? tusikurupuke na kuanza kuongea tu na kufurahisha midomo yetu.

Sasa nani bosi wa wanaotunga na wanaosahihisha?
 
Kwa muda mrefu nimekuwa nikiheshimu sana uandishi wako, lakini katika hili naona umekurupuka. Unaufahamu utaratibu wa utungaji wa mtihani wa kidato cha nne? Katika maswali yaliyotungwa, kuna lolote lipo nje ya syllabus? Au unataka NECT ipite kila shule kuulizia walimu kama wamefikiri wapi kwenye kufundisha ili kila shule itungiwe mtihani wake? Kwenye mtihani wa taifa yanaulizwa hadi maswali ya form one, sasa ukisema eti yametungwa maswali magumu unamaanisha nini?

Kuna maagent wa tatu wa curriculum processing; kuna curriculum developer, curriculum implementer na curriculum evaluator. Na siku zote huyu evaluator siku zote hafanyi chochote nje ya mapendekezo ya TIE na Walimu ambao ndiyo wanaimplement curriculum.
 
Mitihani inatungwa kwa kufuata mtaala pamoja na muhtasari wa somo husika na sio kitabu fulani ndugu. Halafu maswali inategemea na jinsi walivyouliza: Unaweza kuulizwa: 'account for; Give reasons for au explain' hayo yote yanahitaji jibu la namna moja. Pmoja na kufundishwa wanafunzi lazima wafundishwe namna ya kuelewa maswali na kuyajibu. Sasa mwalimu mwenye manung'uniko usitarajie afanye hivyo. Yaani hapa suala/sababu kuu ukosefu wa walimu tu. Mimi mwenyewe O-level nilisoma shule ambayo ndo tulikuwa intake ya kwanza, tulianza form one mwezi wa sita badala ya januari lakini walimu walikuwa nanatufundisha kwa kutimia nitisi zao au kutoka shule nyingine na nilifaulu vizuri. A-level nilikuwa intake ya pili mambo ni hivyo hivyo lakini tulifaulu.
 

Tulizoea kuwa zinafaulisha kwa sababu nyingi zilikuwa zikiiba mitihani. Siku hizi hiyo imefutwa.
 
this time Waislamu hawajafelishwa kama mwaka jana ? manake mmh
 
Daima watunga mitaala huwa wanatoa vitabu vya aina mbili; vitabu vya kiada na vya ziada (text books and reference books). Mtunga mitihani anachojali wakati wa kutunga mtihani ni concept iliyopo kwenye syllabus, kama kwenye syllabus watoto wanajifunza osmosis, mtunzi wa mtihani atatafuta sweli linalohusiana na concept ya osmosis kulingana na level ya mtoto. Hatatunga swali la form six akalileta kwa form four. Na uzuri ni kwamba utunzi wa maswali ya mitihani haufanywi na mtu mmoja. Random sample ya walimu kutoka mashuleni plus representative wa TIE huwa wanaparticipate. So mtu kukaa chini na kuanza kumrushia mawe Ndalichako, ni kutafuta visingizio visivyo na maana. Ukweli ni kwamba curriculum implementation haikuwenda sawa, walimu wapo kwenye Mgomo. Pasco asitake kukwepa ukweli. awaambie wakubwa wake kwamba walimu wapo kwenye mgomo, serikali itafute namna nzuri ya kusikiliza matatizo ya walimu.
 
Last edited by a moderator:

Sasa kwa nini Wizara hutoa vitabu na kuvipa alama ya ithibati. Na pia kwa nini Wizara hutofautisha kati ya vitabu vya Kiada na Ziada? Ni kwamba wengi tumesoma kama ulivyosoma wewe. Kwa kupitia juhudi zetu na za walimu wetu tukafaulu. Hapo nakubaliana na wewe kabisa.

Lakini hali tuliyosoma sisi haikuwa hali nzuri pia. Kwa hiyo hata wale waliofeli wakati wetu haina maana wote ni wajinga kama ambavyo Wizara na Baraza wanataka watu waamini. Na kitu kingine nani wa kututoa katika hali tuliyosoma mimi na wewe kama siyo hawa watu wa Wizara na Baraza la Mitihani?

Hivyo basi kuwalalamikia hatuwaonei tunataka wafanye kazi hali iwe nzuri na anayefaulu kweli awe ni mtu mwenye uwezo wa kufaulu na anayefeli awe ni mtu asiye na uwezo wa kufaulu (siyo mtu anafeli kwa sababu ya vitu vingine nje ya uwezo wake)
 
Hiv huyu pasco ana elimu gani?yawezekana huyu ni mwanafunz wa kipndi kile cha kapuya,mtihan wa 98 uliovuja. Yawezekana ulipata divisn 1 kumbe kichwan wewe ni garasa. Kwanin kawambwa asijiudhuru?shule zina vitabu tofauti vya kufundishia,wakt huo necta wanaambiwa tunga mtihan kulingana na topic a,b,cd. Unataka ndali afanye nini?ulitaka hao laki 2.5 wapewe div 3 ili ufauru upemepanda wakati ni watoto makopo?
 
Kwa ufupi hakuna mitihani migumu kama sylabus ilifuatwa. Nakumbuka miaka ya nyuma tulikuwa tunafanya mitihani inayotoka Cambridge na Oxford na tulifaulu. Cha msingi ni Muhtasari wa kufundishia kama ulifuatwa. Kinachoonekana hapo Bongo sasa ni siasa za kudharau baadhi ya watu hasa watendaji. walimu wakidai milioni 12 zinaonekana nyingi ,lakini mbunge akilipwa milioni 7 ni kidogo. Huyo mbunge anafanya nini,zaidi ya kulala na kutukanana tu? hasa wa chama twawala. Ajiuzulu waziri na mkuu wake ikiwezekana.
 
Sasa nani bosi wa wanaotunga na wanaosahihisha?

Kuwa bosi ndiyo nini? basi bosi wa Ndalichako ni nani? au bosi wa mawaziri ni nani? mbona tuna uozo mtupu na hatuna cha kufanya? cha muhimu walimu waboleshewe MISHAHARA, vitendea kazi viwepo, wazazi wajitume kufwatilia maendeleo ya watoto wao, watoto wasimiliki simu mashuleni, tuboreshe shule zilizopo na siyo kukimbilia kuanzisha mpya. kuanzisha na kuboresha maabara, Wanafunzi watandikwa inapobidi. Shule nyingi zenye nidhamu hufaulisha vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…