Mkodoleaji
JF-Expert Member
- Apr 27, 2008
- 458
- 138
Nivea nakubaliana na wewe, angalia katika sababu zangu hiyo namba 1. inaendana na ulichosema
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndugu Mkodoleaji, ukikodoa sawa sawa utaona maelezo yako hapo kwenye RED na mfano ulioutoa vinahitilafiana!! Unadhani mitihani ingetungwa nje ya Muhtasari hayo maandamano yangezuilika???
La hasha. Sidhani kama kuna swali lilitoka nje ya Muhtasari na kama kuna mwenye ushahidi aweke humu. Pili unanishangaza unapotaka eti mitihani itungwe toka kwenye kitabgu/vitabu fulani...Nadhani cha msingi ni kuzingatia mada zilizopo kwenye muhtasari na maarifa anayotakiwa kuwa nayo mtahiniwa wa level hiyo. issue sio kitabu!!
i beg to differ, watoto siku hizi hawasomi kutwa kwenye facebook,youtube asa atasoma saa ngapi kama hajui kumanage muda wake vizuri lazima afeli tu hilo ulilosema watoto walionacho ndo wamefaulu si kweli , jitihada binafsi za mwanafunzi ndo zita determine matokeo Dr Ndalichako hahusiki na lolote wanafunzi wanambwelambwela tun hata hasomi kabisaa
Hivi jamani huyo Dr. Joyce Ndalichako, ndiyo mtungaji na msahihishaji wa hii mitihani? tusikurupuke na kuanza kuongea tu na kufurahisha midomo yetu.
Kwa muda mrefu nimekuwa nikiheshimu sana uandishi wako, lakini katika hili naona umekurupuka. Unaufahamu utaratibu wa utungaji wa mtihani wa kidato cha nne? Katika maswali yaliyotungwa, kuna lolote lipo nje ya syllabus? Au unataka NECT ipite kila shule kuulizia walimu kama wamefikiri wapi kwenye kufundisha ili kila shule itungiwe mtihani wake? Kwenye mtihani wa taifa yanaulizwa hadi maswali ya form one, sasa ukisema eti yametungwa maswali magumu unamaanisha nini?Wanabodi,
Kwa maoni yangu, kitendo cha NECTA kutunga mtihani ambao siyo ili kuwakomoa "watu fulani " kulikopelekea wanafunzi kufeli vibaya ili kujustify hao kina "fulani" ni wajinga!, na kuyapeleka makaratasi halisi ya mtihani kuuanika uthibitisho wa jinsi hao kina fulani walivyo jibu utumbo yakiwemo matusi ili kupata public sympathy kujustify tatizo sio NECTA, sio mitihani wall sio usahihishaji bail ni wanafunzi ndio wajinga na vibonde, hakipaswi kuachwa bila kupingwa!.
Wengi waliangalia hili kwa jicho la juu juu juu tuu bila kujiuliza wajinga halisi ni kina nani na long impact ya ukomoaji huu wa NECTA utalifikisha wapi taifa letu in a long run baada ya matokeo hayo kujenga matabaka ya wenye nacho na wasionacho!.
Kwa sio jua Wengi wa waliofaulu ni watoto wa wenye nacho ambao wana uwezo wa kuwalipia watoto wao shule bora, na wengi wa waliofeli ni watoto wa wa wasionacho hivyo Mama Ndalichako kupitia NECTA anawanyanganya hata hicho kidogo walichonacho, unategemea mini after a long time ?!.
I think it's time up for Mama, Dr. Joyce Ndalichako to go!, not withstanding madhaifu mengine yote wenye mfumo wetu wa elimu.
Pasco.
Mitihani inatungwa kwa kufuata mtaala pamoja na muhtasari wa somo husika na sio kitabu fulani ndugu. Halafu maswali inategemea na jinsi walivyouliza: Unaweza kuulizwa: 'account for; Give reasons for au explain' hayo yote yanahitaji jibu la namna moja. Pmoja na kufundishwa wanafunzi lazima wafundishwe namna ya kuelewa maswali na kuyajibu. Sasa mwalimu mwenye manung'uniko usitarajie afanye hivyo. Yaani hapa suala/sababu kuu ukosefu wa walimu tu. Mimi mwenyewe O-level nilisoma shule ambayo ndo tulikuwa intake ya kwanza, tulianza form one mwezi wa sita badala ya januari lakini walimu walikuwa nanatufundisha kwa kutimia nitisi zao au kutoka shule nyingine na nilifaulu vizuri. A-level nilikuwa intake ya pili mambo ni hivyo hivyo lakini tulifaulu.Pasco umeongea point ambayo watu wengi hawataki kuiona.
Kwangu Mimi suala si Dr Ndalichako tu, ila hata Waziri Kawambwa na viongozi waandamizi have to go. Hatukatai kuwa kuna watoto ambao hawasomi, hilo tunalijua maaana wote tumesoma sekondari. Sasa sababu za kufeli haiwezi kuwa moja tu ya uzembe wa wanafunzi.
Sababu zinaweza kuwa zifuatazo:
1. Uzembe wa wanafunzi
2. Mfumo mbovu wa elimu
2.1. Kutokuwa na mitaala ya kueleweka
2.2. Kuwa na shule bila walimu
2.3. Kutokufanya ukaguzi wa kutosha
2.4. Kutokuwa na motisha kwa walimu
2.5. Kutoboresha shule za kata n.k.
3. Utendaji mbovu wa Baraza la Mitihani
3.1. Kutunga mitihani ambayo haiendani na mihutasari waliyopewa walimu kufundisha na wanafunzi kusoma (nakumbuka wakati nasoma Sekondari, nilisoma Book-Keeping na kulikuwa na kitabu kinaitwa Book Keeing for Tanzania Secondary Schools kama sikosei ambacho kilikuwa kinatolewa na Wizara ya Elimu, lakini hata siku moja hutapata swali kutoka ndani ya hicho kitabu. Maswali karibu yote yalikuwa yanatoka kwenye Frank Wood-Business Accounting ambacho wakati huo kukipata ilikuwa mbinde)
3.2. Kutokuwa makini katika usahihishaji
4. Kutowajibika kwa nchi (Uzembe wa Viongozi) (viongozi hawajui kuwa wanatakiwa kulijenga taifa hili kwa kupitia elimu). Nakumbuka kuna bwana mdogo ambaye alishindwa kuendelea na shule akiwa Form Three kutokana na uwezo mdogo. Baada ya miaka kadhaa ya kujishughulisha na biashara akapata fedha akataka kurudi shule ili aendelee. Ile shule aliyokwenda ili ajiendeleze kama Private Candidate akaambiwa alete barua toka ile shule aliyokuwa anasoma. Ile shule aliyokuwa anasoma wakampa barua, kwenda kwenye shule mpya wakamwambia aje na matokeo ya Form Two akawajibu kuwa mwaka wao mitihani ya Form Two ilikuwa imefutwa, ili ilikuja kurudishwa baadaye. Wakamwambia nenda baraza la mitihani ukachukue barua kuthibitisha hilo. Kwenda baraza la mitihani wakasema huweza kwenda form three mpaka ufanye mitihani ya Form Two upya. Huyo bwana mdogo akaamua kuachana na masuala ya shule aendelee na maisha yake mengine. Nimetoa huu mfano kuonyesha jinsi viongozi wasivyoona jinsi wanavyojenga taifa la wajinga kwa kutowajibika kwao. Sasa hao watoto 240,000 wanakwenda wapi? Kama siyo kuanza kufuga majambazi na machangu.
Pasco watu wengi, hawataona ulichosema, lakini hawa viongozi lazima waje na maelezo ya kutosha kuhusu sababu hizi zote. Vinginevyo they have to go.
Pia waangalie cha kufanya. Kwangu mimi kuna mambo mawili tu:
1. Mitihani isahihishwe upya
2. Mitihani itungwe upya na wanafunzi wafanye tena. Hili si mara ya kwanza maana mitihani ya Mwaka 1998 (kama sikosei) ilirudiwa mwaka 1999 baada ya kuona kuwa kuna udanganyifu mkubwa.
Samahani wadau nimeandika sana.
hapo umenena, haiwezekani hata shule tulizoea kufaulisha zkafeli, kwani watu weng kwa sasa wanalaum migomo ya walim lakn tujiulize swali la pili je hata shule za binafsi kulikuwa na mgomo?? Je ni kwel wanafunzi na walim hawana akili? Je tugeuzie macho upande wa pili kumekuwa na mambo yanayofanyika kimchezomchezo, angalia suala la mikopo kwa watu wanaochukua taaluma ya ualim, je ni kila mtu awe mwalimu? Hapa ina maana baadhi ya watu kutokana na watu kuwa na maisha magum anaenda kukidhi mahitaji, fatilia kwa umakini utaona baadhi ya watu wanabadilisha fani katikat ya safar ama anabadl mda akpata hela na kwenda anapotaka. Hili ni janga la kitaifa, tena si mchezo
Daima watunga mitaala huwa wanatoa vitabu vya aina mbili; vitabu vya kiada na vya ziada (text books and reference books). Mtunga mitihani anachojali wakati wa kutunga mtihani ni concept iliyopo kwenye syllabus, kama kwenye syllabus watoto wanajifunza osmosis, mtunzi wa mtihani atatafuta sweli linalohusiana na concept ya osmosis kulingana na level ya mtoto. Hatatunga swali la form six akalileta kwa form four. Na uzuri ni kwamba utunzi wa maswali ya mitihani haufanywi na mtu mmoja. Random sample ya walimu kutoka mashuleni plus representative wa TIE huwa wanaparticipate. So mtu kukaa chini na kuanza kumrushia mawe Ndalichako, ni kutafuta visingizio visivyo na maana. Ukweli ni kwamba curriculum implementation haikuwenda sawa, walimu wapo kwenye Mgomo. Pasco asitake kukwepa ukweli. awaambie wakubwa wake kwamba walimu wapo kwenye mgomo, serikali itafute namna nzuri ya kusikiliza matatizo ya walimu.Mkirua teh teh usinitoe macho. Hapo nimetoa baadhi ya sababu ambazo zinaweza kufanya watoto wafeli. Sasa kwa Baraza na Wizara kuangalia sababu moja au mbili tu hapo siyo sahihi. Kuhusu maandamano kuzuilika ndugu mimi siyo mtabiri.
Kuhusu vitabu ni kwamba kama Wizara inatoa vitabu vya msingi, ambavyo walimu na wanafunzi wanatumia muda kuvisoma unategemea pia hata maswali ya kuwatahini mengi yatatoka humo. Unaweza kuongeza machache kutoka sehemu nyingine ili kujenga utamaduni wa kujisomea zaidi ya vitabu vya Wizara. Sasa kwa kiwango gani mitihani iliyotungwa iliwiana na hilo, hicho ni kitu ambacho Baraza na Wizara walitakiwa waseme. Siyo sisi kuja kuspeculate hapa. Na wasiwasi wangu unakuja maana mitaala yenyewe bado inagombaniwa kuwa haijakaa sawa (rudia sakata la Mbatia bungeni)
Mitihani inatungwa kwa kufuata mtaala pamoja na muhtasari wa somo husika na sio kitabu fulani ndugu. Halafu maswali inategemea na jinsi walivyouliza: Unaweza kuulizwa: 'account for; Give reasons for au explain' hayo yote yanahitaji jibu la namna moja. Pmoja na kufundishwa wanafunzi lazima wafundishwe namna ya kuelewa maswali na kuyajibu. Sasa mwalimu mwenye manung'uniko usitarajie afanye hivyo. Yaani hapa suala/sababu kuu ukosefu wa walimu tu. Mimi mwenyewe O-level nilisoma shule ambayo ndo tulikuwa intake ya kwanza, tulianza form one mwezi wa sita badala ya januari lakini walimu walikuwa nanatufundisha kwa kutimia nitisi zao au kutoka shule nyingine na nilifaulu vizuri. A-level nilikuwa intake ya pili mambo ni hivyo hivyo lakini tulifaulu.
Sasa nani bosi wa wanaotunga na wanaosahihisha?