Dr. Joyce Ndalichako, Katibu Mtendaji wa NECTA! "It's Time To Go!.


Lukolo nakubaliana na wewe kwa maelezo uliyoyatoa, lakini kitu kimoja ufahamu matokeo ya mitihani ni zao la Baraza la Mitihani. Matokeo yakiwa mabaya watu watalalamikia Baraza la Mitihani. Kwa nini basi inakuwa ni kwa sababu Baraza ndio linalochagua watungaji, baraza ndilo linachagua wasahihishaji na baraza ndilo linatoa mitihani. Sasa kama syllabus haikutekelezwa yote, mitihani ingetungwa kutokana na kile kilichotekelezwa. Huwezi kutunga nje ya kile kilichofundishwa na kuwaita watoto wamefeli, watu watasema umewafelisha.

Sasa kama ulivyosema kumvagaa Ndalichako peke yake kwa kweli siyo sahihi maana mfumo mzima wa elimu una matatizo na ndiyo maana hata mitaala haikutolewa bungeni. Hivyo kuna haja kabisa ya kuufumua mfumo mzima wa elimu ili kuhakikisha kuwa watoto wetu wanapata elimu iliyo bora
 

Kwa nini unaona kumpima mwanafunzi kwa mtihani wa mwisho sio sahihi katika kipindi hiki? Kwa nini sio zama zile ulizokuwa ukisoma wewe? Still NECTA wapo right.
 
Umeeleza kwa umakini mkubwa sana ila sijaona point inayomfanya Ndalichako aachie ngazi,, mitihani ikisahihishwa upya matusi yatakuwa majibu sahihi? au vesi za bongo fleva na wasiojibu je nao watapewa alama gani? hoja zako za hapo juu ndio zilikuwa sahihi kabisa, Kuhusu kurudiwa mitihani mwaka 1998 ilirudiwa kwa sababu wao walishindwa kudhibiti mitihani so ukavuja this time unataka urudiwe kwa sababu zipi?
 
mimi naanza kuwa na mashaka, kama wizara haina mitaala (fake??) hao NECTA wanatumia ipi kutunga mitihani?

Lakini pia hapa tunaona vitu tofauti kutokana na hoja hii, walivyowambia wananchi mwanzoni juu ya elimu watawala (viongozi) wakabuni wazo la St. 'School' na wakadhani ndio ujanja. Hata walivyoambiwa walijipa confidence tu wakisema "hao wengine watajijua" na hata wakaenda mbali zaidi na kutuletea shule za siasa (za kata). Sasa kinachotokea ni dalili za mwazo wa tatizo na wala sio tatizo kamili. Fikiria NECTA wakifanya hivyi, je wakisema East Africa Community (EAC) tu harmonize pia elimu jaribu kufikiria itakuwaje kwa wanafunzi wa Kitanzania!!!
Tulimuhasi Mwalimu Nyerere bila kufikiria njia mbadala kwa kudhani 'rukhusa' inge animate vision ya elimu ya nchi.

LAKINI:
hebu tafakari juu ya hii logo ya NECTA na uhalisia wa elimu ya dunia ya sasa ....angalia symbols kama jembe, koleo, kitabu then ufikirie elimu ilivyobadilika kidunia!

 
Au Pasco umeamua kumsulubisha Kawambwa indirectly? Jicho la tatu lanionesha hivyo. If that is what you meant I like your ingenious approach.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 

Hapa sijakuelewa.......maswali yaoke kwenye kitabu? Sio yatungwe na wataalamu wa NECTA?
 
Kwa nini unaona kumpima mwanafunzi kwa mtihani wa mwisho sio sahihi katika kipindi hiki? Kwa nini sio zama zile ulizokuwa ukisoma wewe? Still NECTA wapo right.
Mimi nilishalipinga hili siku nyingi kamanda, kudhihirishi hilo niliona ni upuuzi na niliacha kufanya mitihani na test za darasani ikiwepo mitihani ya mock nikisubiri hiyo necta yao kwa sababu niliona ni upuuzi kupotweza muda kutengeneza cont. assessment isiyo na kazi.
 
Jamani kwa mtazamo wangu hawa wenzangu ni "Janga la Kitaifa" sana, hivi jamani nani yuko salama? Ndalichako yuko chini ya Kawambwa ambao wote wanaripoti kwa Kikwete,sasa mama wa watu kafanyaje. Mtoa mada hebu anza kwa Kawambwa kwani huyu Shukuru hajui kwa nini wanafunzi wamefeli acha kutafuta mchawi, Mchawi ni wewe mwenyewe. wewe mwenyewe umechukua hatua gani ili kuwafundisha wenzio elimu ni mwanga. Wewe endelea kulalamikia mama Ndalichako mwenzio ni dokta huyo, acha wivu:nono:
 

Dancan,
Hiyo mapendekezo kwangu yalitokana na vitu viwili: 1. Kwamba kwa sababu walimu wengi hawana motisha inawezekana hawakusahihisha kwa makini. Hapa utaniuliza je umakini utaongezeka wakisahihisha mara ya pili, naamini kama wakipewa motisha wanaweza kusahihisha kwa makini (lakini hapa hata mimi naona bado pagumu). Na pia kusahihisha upya haina maana hakutakuwa na watakaofeli (kama hao wa bongo fleva).

2. Pia kutokana na matatizo mengi ya wizara ya elimu, kuna uwezokano syllabus hazifundishwi kwa ukamilifu na mitihani ikitungwa kwa kuzingatia kuwa syllabus zilikamilika. Sasa kinachotakiwa kufanywa ni kutungwa mitihani mipya ambayo itawiana na syllabus ambazo zimekamilishwa. Huu ni ufumbuzi wa muda mfupi. Kwa ufumbuzi wa muda mrefu ni kuangalia matatizo yote yanayoikumba sekta ya elimu na kuyarekebisha. Sasa hili litaendana pamoja na kuwafumua viongozi ambao wamekaa lakini hawajayatatua haya matatizo ya elimu.
 
Jamani kwa mtazamo wangu hawa wenzangu ni "Janga la Kitaifa" sana, hivi jamani nani yuko salama? Ndalichako yuko chini ya Kawambwa ambao wote wanaripoti kwa Kikwete,sasa mama wa watu kafanyaje. Mtoa mada hebu anza kwa Kawambwa kwani huyu Shukuru hajui kwa nini wanafunzi wamefeli acha kutafuta mchawi, Mchawi ni wewe mwenyewe. wewe mwenyewe umechukua hatua gani ili kuwafundisha wenzio elimu ni mwanga. Wewe endelea kulalamikia mama Ndalichako mwenzio ni dokta huyo, acha wivu:nono:
 

Kikubwa sana hapo pia wanafunzi wanawekwa kinidhamu ya kishule kama miaka hiyo ya zamani uzuri na wewe ni mtu wa zamani lakini tazama leo maisha ya wanafunzi jinsi yalivyo hakuna utofauti na watoto wa mitaani maana hata kwenye kumbi za starehe unawakuta hakuna wa kuhoji wengine wanaishi na mabwana kabisa ukiachilia mbali na wanaoishi geto kwa ghalama za wanaume,wakati zamani kwenda mjini tu ilikuwa ishu lazima uwe na get pass otherwise huna shule na ndio hizo shule tajwa hapo juu bado wanendeleza mfumo huo. kuhusu ugumu wa mitihani inawezekana ila aliyesoma marks zinapungua kidogo kama ilivyotokea kwa hizo shule ulizotaja, wa A hawezi pata F
 
Ni fikra za kivivu sana kufikiria kuwa eti kufeli kwa wanafunzi hawa kunasababishwa na Necta, pia ni utapiafikra kufikiri kuwa eti sababu za wanafunzi hawa kufeli ni moja au mbili tu, kwangu mimi hoja ya mbatia ndo ulikuwa msingi mzuri wa kuanzia kujadili tatizo hili! lakini je ni serikali gani hii isiyotaka kuwajali walimu kama haitoshi haitaki kujadiliwa bungeni?
 
Kama sylabus imetolewa shule makini zimefundisha kama inavyotakiwa na baadhi ya shule isiyo na maabara kwa mfano haikufundishwa ipasavyo ndalichako aende kuuliza kila shule mmefundishwa nn ili atunge mtihani au atunge kutokana na sylabus inavyotaka? Wale walochora katuni wameongezea watu wa kufeli ndalichako afanyeje?
 
Ni kweli kaka ila naomba ujue kuwa .Kwa ghalama za usahihishaji hizo hutolewa na NECTA haihisiani na mshahara tena walimu wengi hufurahi wakipata hiyo nafasi maana ni hela ya ziada
Kuhusu silabausi unapozungumzia ubora mara huwa lazima ubora huo ufuatwe tukisema itungwe mitihani kwa mujiwa silabasi zilizokamilka tutakuwa tunajidanganya maana shule zote haziishii pamoja utakuta wengine wako nyuma wengine mbele nk but cha muhimu sababu zote ulizotoa hapo mwanzo zifuatwe ili kukamilisha hizo silabasi maana ndio standard ya elimu kwa inchi nyingi sasa leo ukisema tutunge kulingana na uzembe wetu wa kutomaliza silabasi tutakuwa tunajidanganya wenyewe na tutaaibika huko duniani maana cheti hicho hakitumiki Tanzania pekee
 
Sijawahi tegemea hata siku moja mkuu wangu pasco utaandika kitu usichokielewa kabisa? Sidhani kama unaijua kazi ya necta...kama ungeijua usingelaumu hata kidogo
 

Dancan,
Nakubaliana na wewe kabisa nguvu ziwekezwe katika kutoa elimu tushindane na watu wengine duniani. Hilo nimesema ni suluhisho la muda mrefu. Sasa suluhisho la muda mfupi ni lipi kama taifa? Maana tuna watoto laki mbili na ushee ambao wanaenda kuzagaa barabarani na kila mtu anakubali kuwa hili ni tatizo tufanyaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…