Elimu bora ni ipi? Unaweza kuthibitisha kwamba wote waliopata sifuri hawajaelimika? Suala hapa ni kuangalia suala la mitihani na lengo la kuwajenga watoto kitaaluma. Kama huna walimu, wanafunzi wanababia katika kusoma tafuta mbinu za kuwatahini watoto kutokana na kile wanachokipata. Huwezi kuchukua mitihani ya uingereza na kuileta hapa kisa syllabus ni moja wakati mwanafunzi hajawahi kufundiswa hiyo syllabus. Sasa Baraza la Mitihani siyo tu kijiwe cha kutunga mitihani, bali linatakiwa lisaidiwe kuishauri Wizara namna muafaka ya kuwatahini watoto katika mfumo wetu wa utoaji elimu.
Mkuu Mkodoleaji, Hakuna syllabus ya Uingereza iliyotumika. Kumbuka kuwa Tanzania ni sehemu ya nchi nyingine duniani. Wametunga mitihani kulingana na syllabus inayopaswa kufundishwa Tanzania kwa muda wa miaka mnne. Lakini kama wameifuata watakuwa wametimiza wajibu wao kama Wakala wa Serikali. Sio kazi ya Baraza la Mitihani kwenda kuwauliza Wizara ya Elimu kuhusu walikoishia ili kutunga mitihani kulingana na walivyofundisha kwa lengo la kuwafichia aibu. Kama hakuna walimu, wanafunzi wanababia katika kusoma sio busara kutafuta mbinu za kuwatahini kutokana na kile wanachokipata, hiyo itakuwa ni kuua elimu; watalaam watakapatikana hawatakuwa na uwezo wa kushindana na watalaam kutoka nchi nyingine kwa sabau wamependelewa katika kupata elimu duni.
Last edited by a moderator: