ndugu yangu sikubaliani na wewe. mwalimu anapotunga mtihani shuleni, lazima ajiulize kuwa syllabus imefundishwa hadi wapi. akitunga mtihani wa muhula wa kwanza, itakua ajabu akiweka topics ambazo hajazifundisha. zinafaa kufundishwa
muhula wa pili. huo ndiyo upimaji (evaluation)
ile formula ya kcaase kwa waliyo chukua ualimu wanaelewa umuhimu wake. kugawa maswali kwa 25. 50 na 25% kama nilivyo andika awali ni muhimu sana. kwa mwalimu bora, akipelekwa senegal kutunga mitihani, hawezi kukurupuka kutunga kabla ya kuzingatia vipengele vingi. baadhi yake ni kuuliza kama hapajatokea mafuriko au vita au janga lolote lililofanya syllabus zisifundishwe kwa ukamilifu, maabara zipo mashuleni, ufaulu wa mwaka uliopita ulikuwaje, nk......
ufaulu mzuri ni ule ambao umekaa kama bakuli lilofunikwa. pande za pembeni ziko chini na upande wa katikati uko juu. namaanisha kuwa wanaofaulu kwa division 1 wachache, wanaopata div 11 na 111 wengi, na wale wa iv na 0 wachache. mwaka huu wa iv na 0 ndiyo wengi! hii ni hatari. sababu zitafutwe naamini ni nyingi lakini lazima waliyotunga nao wana swali la kujibu. dkt. ngalichako ajiuzulu