Nifah
JF-Expert Member
- Feb 12, 2014
- 34,020
- 79,098
Wakuu, poleni kwa janga la Kariakoo. Mungu awarehemu waliotangulia, majeruhi wapate nafuu mapema na ambao bado wapo katika kifusi wapate kuokolewa wangali hai, Amen!
Kama mtakumbuka vyema, mwishoni mwa mwezi May niliwaletea habari kuhusiana na suala la Dr. Khiago kutumia nafasi yake kama Katibu Mtendaji wa bodi ya filamu nchini kufanya upendeleo katika ziara iliyoandaliwa na Ofisi ya Rais ambayo wasanii na wadau wa filamu nchini waliungana na Rais kuelekea Korea ya Kusini.
Niliwaelezea namna Dr. Khiago alivyotumia nafasi yake hiyo kumuengua msanii (Mwanamama) aliyependekezwa hapo kabla kisha kumuweka anayedaiwa kuwa 'mpango wa kando' wake. Kitendo hicho kilituumiza tuliokuwa wengi, hadi kupelekea mimi kupaza sauti hapa jamvini...
Hivyo basi, hilo na mengine mengi vimepelekea Dr. Khiago kukosa sifa ya kuendelea kuwa Katibu Mtendaji wa bodi ya filamu nchini.
Taarifa za uhakika nilizonazo ni kwamba tayari ameshaenguliwa katika nafasi hiyo, na Katibu Mkuu mpya atakuwa baina ya Tido Muhando, Dr. Kasiga kutoka Udom au mwingine ambaye nimeshindwa kulipata jina lake kwa uharaka.
Penzi kitovu cha uzembe... Dokta atarudi kufundisha chuo kikuu kutoka kuwa Bosi wa bodi ya filamu nchini!
Chanzo changu nyeti pamoja nami,
Nifah.
Pia soma
Zengwe lagubika ziara ya Rais na wasanii; waratibu wadaiwa kufanya mchezo mchafu
Mkono mtupu haulambwi! Naam, ndivyo ninavyoweza kulielezea hili. Wikiendi iliyopita Rais alijumuika kwenye uzinduzi wa albam ya msanii wa kizazi kipya Harmonize akiwa kama mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa wengine ambao ni viongozi na wadau wa tasnia ya burudani. Katika uzinduzi huo Rais...