Dr. Khiago Kilonzo kikaangoni, kuenguliwa muda wowote!

Dr. Khiago Kilonzo kikaangoni, kuenguliwa muda wowote!

Kwanza nimpongeze mh Rais kwa ushindi wa taifa stars pale kwa Mkapa pili nimtakie Dr maisha mema anaporudi kufundisha chuo au majukumu yoyote atakayopangiwa
Kupata na kupoteza ndio maisha ya binadam hadi pale anapopoteza uhai na kupumzika
Anaenda kufundasha chuo au shule.
 
Muhuni ameanguka kwasababu ya kuendekeza mapenzi...kina Baltazar wapo wengi sana.
 
Vipi kuhusu maslahi? Anarudi kusubiri mshahara kwa mshahara kutoka kuwa bosi.
Japo sijui anacholipwa vs atakachoenda kulipwa ila kuna uwezekano ikawa ni tofauti ndogo, angesota kama hizo tuhuma zingempelekea kutoka nje ya mfumo wa ajira
 
View attachment 3156973

Wakuu, poleni kwa janga la Kariakoo. Mungu awarehemu waliotangulia, majeruhi wapate nafuu mapema na ambao bado wapo katika kifusi wapate kuokolewa wangali hai, Amen!

Kama mtakumbuka vyema, mwishoni mwa mwezi May niliwaletea habari kuhusiana na suala la Dr. Khiago kutumia nafasi yake kama Katibu Mtendaji wa bodi ya filamu nchini kufanya upendeleo katika ziara iliyoandaliwa na Ofisi ya Rais ambayo wasanii na wadau wa filamu nchini waliungana na Rais kuelekea Korea ya Kusini.

Niliwaelezea namna Dr. Khiago alivyotumia nafasi yake hiyo kumuengua msanii (Mwanamama) aliyependekezwa hapo kabla kisha kumuweka anayedaiwa kuwa 'mpango wa kando' wake. Kitendo hicho kilituumiza tuliokuwa wengi, hadi kupelekea mimi kupaza sauti hapa jamvini...

Hivyo basi, hilo na mengine mengi vimepelekea Dr. Khiago kukosa sifa ya kuendelea kuwa Katibu Mtendaji wa bodi ya filamu nchini.

Taarifa za uhakika nilizonazo ni kwamba tayari ameshaenguliwa katika nafasi hiyo, na Katibu Mkuu mpya atakuwa baina ya Tido Muhando, Dr. Kasiga kutoka Udom au mwingine ambaye nimeshindwa kulipata jina lake kwa uharaka.

Penzi kitovu cha uzembe... Dokta atarudi kufundisha chuo kikuu kutoka kuwa Bosi wa bodi ya filamu nchini!

Chanzo changu nyeti pamoja nami,

Nifah.

Pia soma
Hongera, ni uandishi mzuri sana, ndani yake una sauti ya mamlaka na kujiamini. Ni uandishi kama wa gwiji. Safi sana.

Ova
 
Hongera, ni uandishi mzuri sana, ndani yake una sauti ya mamlaka na kujiamini. Ni uandishi kama wa gwiji. Safi sana.

Ova
Gwiji ambaye ni wewe b… mimi bado najitafuta.
Asante sana.
 
Back
Top Bottom