Dr Licky Abdallah ni level nyingine sio kwenye mpira tu hata kwenye mambo mengine mengi sana yuko well informed.
Kwanza mpira alikuwa anapenda tangu mtoto, yeye na ndugu zake pia.
Ni mtu anayependa kusoma sana na kujifunza.
Alianza hayo mambo zamani sana.
Miaka hiyo hata internet hakuna wala TV hazikuwa nyingi, mipira tulikuwa tunaangalia (mechi ambazo zilishachezwa )kwenye cassette.
Yeye alikuwa akitumiwa majarida kutoka nchi za nje na marafiki zake.
Kwa hivyo kwa lugha rahisi tunaweza kusema kuwa fani hiyo ilivyoanza nchini ilimkuta yeye tayari kishawiva siku nyingi
Kwa muda sasa ugonjwa wa KISUKARI unamsumbua ndio maana ameadimika,
ratiba za kwenye vipindi na ratiba za dawa na chakula zinapishana sana ndo maana anashindwa kabisa mara chache akijiweza anakwenda.
MWENYEZI amjaalie afya njema huyu mzee wetu pamoja na familia yake.
Wengine pia tuwape sifa zao wanajitahidi japo kwa sasa mambo mengi yapo kwenye mtandao na ndio sababu huwa inanisikitisha wakikosea kosea hata majina ya wachezaji na vitu vingine,
Kwa kipindi hiki wao hawapaswi kuwa wanakosea kosea vitu vidogo vidogo tena kila mara.
NA PIA KWA WAANDISHI AU WANAHABARI WENGINE PIA MAKOSA MADOGO MADOGO YANAEPUKIKA NA YANAPUNGUZIKA TUKIWA NA ADABU NA TUKAPENDA KAZI ZETU.
Mf Tundu Lissu ni RAISI Wa TLS sio TLC.