Dr. Leaky Abdallah, Shafih Dauda, Edo kumwembe na Geofrey Leah nani mchambuzi bora wa soka?

Dr. Leaky Abdallah, Shafih Dauda, Edo kumwembe na Geofrey Leah nani mchambuzi bora wa soka?

Koment ya maana kuliko zote kwenye huu uzi. Leaky alikuja kipindi ambacho utafutaji wa taarifa na rekodi ulikuwa mgumu sana, kwa hiyo akaonekana yuko nondo jumlisha na kumbukumbu zake murua za matukio ya soka duniani.


Kina Edo wanaonekana wababaishaji kwa kuwa taarifa zote ziko mitandaoni na kila mtu anaweza kuzipata hivyo jamaa wanaonekana copy and paste.


Binafsi simkubali yoyote, hasa kwa kuwa wengi ni wajuaji, mtu anataka ajadili siasa za soka, mambo ya kiufundi, vituko vya mashabiki... Yaani waliomakinika kwenye ufundi pekee i.e wanaochambua kilichotokea kwenye ndimu ni kama akina Mwalimu Kashasha, Ally Mayay na bwana mmoja wa kuitwa Denis Kitambi kabla hajawa kocha wa kufukuzwa na timu aliyoipandisha daraja.
Babu Alex Kashasha yuko vema.
 
Leaky atabia kuwa best milele... kwanza mkongwe afu itikadi sio saaaana......

Achna na wachambuzi wa maelekezo na kuzoom zoom camera.....

Kidoogo yule othman kazi anayafaham haya mambo hajapewa uwanja tu
 
Dkt Leakey anajitahidi sana hasa history ya soka kumwembe anajitahidi sana kwa kuandika makala za soka
 
Habari wadau!

Nahitaji mawazo yenu kati ya hawa watu wanne niliowataja hapo, ni nani ambaye anajua kuchambua soka kwa ufasaha zaidi?

Shafih kila siku tunamsikia pamoja na Geofrey Leah, Dr Leaky Abdallah wengi tunamfahamu na hata Edo Kumwembe tunazisoma sana makala zake katika gazeti la Mwanaspoti.

Napata wakati mgumu kutambua. Msaada (kura) zenu wadau!
Wapi Charles Hillary???
Baada yake ndio anafuata dr. Leakey
 
Dr. Leaky kama peluigi colina.
Anajua kuchambua, kuoanisha, kufikirisha na kutambua.
Hatafuti sifa, ana uelewa mpana wa soka (haungiungi)

Ana misamiati maridhawa.

Akichambua soka utaangalia kabla ya mchezo, mchezo wenyewe mpaka watakapoaga studio.

Kipindi cha mapumziko kwako itakuwa burudani level ingine.
"yatakukera matangazo ya biashara tu"
 
Edo a.k.a kumwembe achana na huyu kiumbe wa kusin mwa tanzania
 
Back
Top Bottom