Dr. Leaky Abdallah, Shafih Dauda, Edo kumwembe na Geofrey Leah nani mchambuzi bora wa soka?

Dr. Leaky Abdallah, Shafih Dauda, Edo kumwembe na Geofrey Leah nani mchambuzi bora wa soka?

Mkuu umekosa chakufanya? Unawezaje kumfananisha Leaky na vitu vya ajabu hvyo? Mpe heshima yake
 
Hii list ungemuweka na Mwalimu Kashasha ningekuelewa. Toa huyo Dauda siyo mchambuzi.
 
Kuna mchambuzi soka na matangazaji soka(kama sijakosea) kwangu Mimi

Watangazaji soka
1.Charles hilal
2.maulidi kitenge

Wachambuzi
1.Mwl kashasha wa TBC
2.Oscar Oscar wa efm
 
Dr Licky Abdallah ni level nyingine sio kwenye mpira tu hata kwenye mambo mengine mengi sana yuko well informed.

Kwanza mpira alikuwa anapenda tangu mtoto, yeye na ndugu zake pia.
Ni mtu anayependa kusoma sana na kujifunza.
Alianza hayo mambo zamani sana.

Miaka hiyo hata internet hakuna wala TV hazikuwa nyingi, mipira tulikuwa tunaangalia (mechi ambazo zilishachezwa )kwenye cassette.

Yeye alikuwa akitumiwa majarida kutoka nchi za nje na marafiki zake.

Kwa hivyo kwa lugha rahisi tunaweza kusema kuwa fani hiyo ilivyoanza nchini ilimkuta yeye tayari kishawiva siku nyingi

Kwa muda sasa ugonjwa wa KISUKARI unamsumbua ndio maana ameadimika,
ratiba za kwenye vipindi na ratiba za dawa na chakula zinapishana sana ndo maana anashindwa kabisa mara chache akijiweza anakwenda.

MWENYEZI amjaalie afya njema huyu mzee wetu pamoja na familia yake.

Wengine pia tuwape sifa zao wanajitahidi japo kwa sasa mambo mengi yapo kwenye mtandao na ndio sababu huwa inanisikitisha wakikosea kosea hata majina ya wachezaji na vitu vingine,
Kwa kipindi hiki wao hawapaswi kuwa wanakosea kosea vitu vidogo vidogo tena kila mara.

NA PIA KWA WAANDISHI AU WANAHABARI WENGINE PIA MAKOSA MADOGO MADOGO YANAEPUKIKA NA YANAPUNGUZIKA TUKIWA NA ADABU NA TUKAPENDA KAZI ZETU.

Mf Tundu Lissu ni RAISI Wa TLS sio TLC.
 
Yupo kijana anakuja kwa kasi anaitwa TIGANA LUKINJA yupo east africa
 
2+Shafi+na+Ashrey%252C+Nani.JPG
 
Binafsi Edo kidogo namuelewa na ndo mana sishangai kuajiliwa super sports kama mchambuz
 
Bongo hakuna mchambuzi kama mwl kashasha hao wengine hata mimi nawazidi
62321c8d6607b324c2538ee2d56c9351.jpg
 
Back
Top Bottom