Dr. Mwakyembe Vs. TAKUKURU


Kwani hawezi kuwa logged on bila ya kuwa mbele ya computer yake? Au kuwa logged on kwenye simu? What are you trying to prove here?

If you are trying to prove mbunge hashughulikii shughuli zake za bunge kwa wakati fulani utahitaji zaidi ya haya mambo ya mtandao, kwanza huna hata uhakika kwamba huyu anayeingia hapa kwa jina la Zitto ndiye Zitto mwenyewe, can you prove that?
 
Valid point, mkuu, I was trying to show how politically at risk mbunge can be, na mtu akiamua kumzushia ni jambo rahisi, au ku-fanya mountain out of a mole hill. Zitto (or whoever it is he claims to be) should not be self righteous akisema eti ye msafi blahblah, maana what you say is one thing lakini kuzushiwa na kuchafuliwa ni rahisi, na pia half baked truths are very dangerous and can easily be twisted to be true. (Also proving that Zito is who he is, ni rahisi, unacheki kompyuta au lapto yake you will find sufficient trail leading him here. So it is not as difficult as you think.... )
Nimetumia mfano huu wa ye kuonekana hashughuliki na masuala ya bunge as an example, seriously I wouldn't care less personally, but his enemies can use it against him as I pointed out earlier.
Ni ushauri kwake, pia awe mwangalifu anachoandika katika blogs hizi maana anaweza kujikuta anajiweka katika wakati mgumu.
 
Kyala,
Mwakyembe hajakaidi summons. Alipigiwa simu. Unless siku hizi simu ni summons.
 
Tukukuru wangeanza kumchunguza Rais Kikwete kwanza...!! Kama wakiona yupo safi wachunguze Mawaziri Kisha wabunge na wamalize kwa wananchi wa kawaidi..! Haka kamchezo kakuanzia katikati kanatoka wapi wakati Shaka na mnuko wa posho posho upo tokea kwa Rais ? Watuchambulie Rais analitwa mshahara kiasi gani na Posho anayopata kwa kila ziara afanyayo..na vile vile watueleze ni kwanini anafanya ziara mara kwa mara ,,kwasababu kama itagundulika anapata posho kwa safari za kitaifa na kimataifa na ikawa anajipangia safari hizo mara kwa mara basi nayo tutaiita rushwa..Kwani zipo safari ambazo zingeweza kufanywa na viongozi wa kawaida wa nchi na si rais.
 

Mmh, hapo umenena... posho hizi za rais mbona hazichunguzwi? This is now looking very entertaining, mi nilishasema Hosea kakosea maana he has opened u the Pandora's box. Hizi posho ni standard procedure katika serikali nzima na mihimili yote ya dola....nasubiri siku Takukuru wakianza kuchunguza askari polisi na askari jeshi kupokea posho mara mbili.....
 
Hivi vitu vya kitoto vina kera sana, Hapa hakuna hoja yoyote ya msingi kwa Tukukuru kuwahoji Wabunge kuhusiana na posho wapewazo kwa kutembelea mashirika na taasisi mbali mbali..tumeliona hili tokea Zamani.

Nimefanya kazi nimelipwa na kupokea posho za jinsi hii kwa muda mrefu na si jambo la siri kwa wafanyakazi wa serikali wana lielewa vizuri ,sasa kwanini wasituchunguze na sisi wote wenye kupokea posho za jinsi hiyo ?

Kama nilivyosema Tanzania hatuhitaji kuwa na chombo chenye uwezo wa kuchunguza watu wenye madaraka madogo au wasio na madaraka kabisa bali Tunahitaji chombo chenye uwezo wa kuwachunguza watu wote kuanzia kwa Rais wa nchi na kuweka wazi uchunguzi wao.

Hii nchi inachosha, Ni heri ingekuwa ya muungano na nchi ya Malawi na tukatawaliwa na viongozi wa Malawi kuliko viongozi tulio nao kwa sasa..!

Wakati mwingine mtu unajiuliza ..Hivi kweli tunae Rais hapa Tanzania au tunae mtu ambae anatusanifu watanzania ?
 
mmh!! Tanzania kazi ipo, matatizo yamekua mengi mno. yanatia kizunguzungu! ccm ingekufa leo tukaanza upya kabisa ingekua afadhali.
 
mzee umeishiwa sera sasa umeanza kushabikia hata upuuzi. Kweli wajinga ndio waliwao kwa kupenda kula

Mkuu,
Niliandika kuhusu Mwakyembe. Kumbe imekukuna ehh!! Hahahaaa safi saana maana ujumbe umefika. Mwakyembe anafahamu kuwa ukitaka kuuwa nyoka, PONDA bichwa lile la Mamvi hadi life (Kisiasa). Yeye akapigapiga mbavu na kumwacha Lowassa akihema bado. Jamaa katibiwa na rafiki zake na sasa wamemrudia tena na anaanza kutetema kama kapigwa shock ya umeme. Mhhh, bikira huyo........

Alifanya makosa kutokumwaga mambo yote HADHARANI eti kwa sababu anaitunzia heshima serikali. Hivi hakumbuki jinsi Malecela na Sallim walivyopakwa? Si walichafuliwa hadi leo unawaonea huruma. Yeye alifikiri ndiyo watamhurumia? Alikuwa na dakika tano zake na akatumia tatu tu. Sasa wenzake wanakuja.
Wiki lijalo anadakika zake za mwisho kuzimalizia. Wasipolia na Richmonduli hadi waimalize, basi yeye ndiyo atazikwa kisiasa.

Hivi kwa nini yeye tu ana matatizo wakati wapinzani kama Zitto na Slaa ambao ni sumu kali ya CCM hadi leo wanapeta? Anafahamu kweli sheria huyu wakati kila siku ana matatizo na sheria? Hawezi kufuata mfano wa Dr mwenzake? Hata Zitto hana matatizo na sheria na hata yakitokea, wananchi wanakuwa nyuma yake. Sasa yeye kwa vyovyote vile kwa aliyoyafanya, ni sawa na UK. Alitakiwa kurudisha pesa na kujiuzulu.

Na mwisho nakukumbusha ukasome maelezo ya Zitto ambaye anasema wazi kuwa hili limeanza siku nyingi na si leo. Kama hakupewa HONGO basi ukweli ni kuwa ALIIBA serikalini maana alipewa posho mara mbili kwa kazi ileile. Ndiyo hawa wanafanya halmashauri za wilaya zife. Mashirika ya umma yafe nk. Ni VIBAKA tu. Kama Mwakyembe hakuchukua basi NAMUOMBA MSAMAHA. Ila kama alimega, basi na yeye akubali tu TAKURURU wamshughulikie.

Mwisho niseme, wasalimie kaka zako. Unafahamu nina maana gani......
 

Kasyabone,
Maneno ndiyo hayo. Siyo kukalia ushabiki wa kitoto. Mwakyembe na hao mafisadi wa Richmond wote ni timu moja. Haya mwambie na Bluray kuwa na yeye kaishiwa kwa kushabikia UJINGA. Mwaka huu hapendwi mtu hapa. Kama Mwakyembe akiwarudi PCCB na Richmond huko bungeni, ntamshabikia yeye. Asipofanya hivyo, na PCCB wakamsulubu yeye, ntawashabikia PCCB. All in all, vita vyao vya sasa, mshindi ni SISI WALALAHOI yaani Watanzania.
 
Nimesha shauri kwamba ngoma zote zinaweza kupigwa kwa mara moja . Kufanya mambo kwa tradition ni wizi mkubwa .Huwezi kuishi kwa posho kibao na watu wanakufa hata aspirini hawawezi kununua . Ngoma hizi zipigwe kwa mara moja .Wewe PCCB chunguza ulete majibu na uchukue hatua na Bungeni Richmond iendelee hadi tujue mwisho wake .Hakuna kurudi nyuma hapa .
 
The best Political strategy (weapon ya Upinzani) siku zote ni kushambulia utawala na utekelezaji wa sera za serikali iliyopo madarakani na sii kushambulia watu wanaosimama nanyi ktk sera au hoja hata kama chama chao kinahusika..
Kosa kubwa linalofanywa hapa ni kwamba watu wanashambulia watu kutafuta mchawi wakati wanasahau kabisa chimbuko la maradhi hayo kuwa hayatokani na Uchawi iusipokuwa ni virusi vya maradhi hayo..
Kazi kwenu kama hamkuelewa!
 
Mkandara,

Vita vya PANZI ni furaha ya KUNGURU. Mwakyembe na Sitta wasipowawahi Richmond na kundi lao, basi Mafisadi watatawahi wao. Jumatano wiki lijalo wachezee shilingi kwenye tundu la Ch*o. Inatakiwa sasa hivi wachachamae hasa ili wawamalize mafisadi. Kikao kikiisha hawajafanya kitu, they are eaten alive.
 
  • Asema iwapo ni mtu safi kwanini anaogopa Takukuru?
  • Asisitiza malipo ya posho mbilimbili ni ni wizi na ufujaji
  • Spika Sitta aendelea kuwatetea wabunge wa kundi lake
  • Waziri Marmo awageukia Takukuru, awatetea wabunge
Na Mwandishi wetu
Tanzania Daima,
Oktoba 30,2009


Mzozo unaohusu wabunge kupokea posho mbili kutoka katika taasisi za serikali na mashirika ya Umma wakati wakifanya kazi za kamati za kudumu za Bunge, linazidi kuchukua sura mpya kila kukicha.

Katika hatua mpya, Mbunge wa Karatu na mwasisi wa mapambano ya ufisadi ndani na nje ya Bunge, Dr Willibrod Slaa, amejitokeza na kueleza kusikitishwa na hatua ya mbunge wa Kyela , Dr Harrison Mwakyembe kukataa kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) kuhusu tabia hiyo ya wabunge kupokea posho mara mbilimbili

akizungumza na TanzaniaDaima jana, Dr Slaa ambaye siku zote amekuwa mstari wa mbele kupinga hatua ya wabunge kujilimbikizia mamilioni ya fedha za posho na mishahara, alisema kuendelea malipo ya mara mbilimbili ya namna hiyo, kunachangia katika kudunisha maisha ya wananchi walala hoi.

Dr Slaa alisema fedha hizo ambazo mashirika na taasisi za Umma na zile za serikali hutoa kwa wabunge , zingeweza kutumia kwa shughuli za maana zaidi ambazo zingewasaidia wananchi kutatua matatizo yao samabamba yao sambamba na kupiga hatua ya maendeleo

"Huu utaratibu sikubaliani nao kabisa, posho hizi ni sawa na wizi pamoja na kuwanyonya walala hoi ambao kila kukicha umasikini unazidi kuwatafuna" alisema Dr Slaa ambae mkakati wa kupambambana na ufisadi aliouzindua akiwa na viongozi wengine wa vyama vya upinzani miaka miwili iliyopita, 'umetekwa nyara' umetekwa nyara na kikundi kidogo cha wabunge wa CCM, akiwemo Dr Mwakyembe.

Akitoa mfano alisema kuwa hata Makamu wa Rais , Dr Ally Mohamed Shein alipofanya ziara yaje katika wilaya ya Karatu hakulipwa posho na viongozi wa wilaya hiyo kwakuwa alishapewa fungu na ofisi yake.

Aliongeza kuwa, hata wabunge waliopo katika Kamati ya Kudumu ya Hesabu za serikali za mitaa ambayo yeye ni Mwenyekiti wake hawakupewa posho na wilaya hiyo.

Alibainisha kuwa, Kama Dr Mwakyembe anajiona kuwa mtu safi kwa namna ambavyo amekuwa akijinadi siku zote, ni kwanini aogope kuhojiwa na Takukuru ambayo ilishawahoji baadhi ya wabunge kuhusu kuchukua posho hizo mara mbili.

"Kama yeye ni msafi kwanini aogope au akatae kuhojiwa na Takukuru ambayo ilisha wahoji wabunge wengine? alihoji Dr Slaa

Wakati Slaa akiwakaanga wabunge wenzake wanaotetea posho hizo, kwa mara nyingine, Spika wa Bunge Samwel Sitta jana aliibuka tena na kuwatetea wabunge wanaotetea hoja hiyo akiwemo Mwakyembe.

Akizungumza bungeni jana, Sitta ambaye siku zote msimamo wake ni wa kumtetea Mwakyembe katika masuala mbalimbali, alisema malipo hayo wanayopewa wabunge si posho, bali ni tarkrima yenye lengo la kuwakirimu.

Spika Sitta alitoa ufafanuzi huo bungeni jana mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu ambapo alidai kuna vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikilikuza jambo hilo.

Alisema ni utaratibu wa kawaida mtu kukirimu au kukirimiwa, hivyo si vibaya kwa wabunge kupewa chai au fedha kwa kazi wanazozifanya hapa nchini.

Sitta alisema anashangazwa na vyombo vya habari kuendelea kung'ang'ania kuandika jambo hilo wakati kuna masuala ya msingi kwa taifa ambayo huwa hayaandikwi.

"Hivi hakuna vitu vingine vya kuandika? kila siku ni posho za wabunge pamoja na kuwahojiwa na Takukuru, mbona hatuoni masuala ya msingi kama 'kilimo kwanza' kupewa kipaumbele?" alihoji Sitta ambaye yeye mwenyewe amekuwa mstari wa mbele kuendeleza masuala kadhaa yaliyopitwa na wakati.

Akitoa kauli hiyo, Spika Sitta alilitaja gazeti moja la kila wiki alilodai kuwa ni la hovyo hovyo, kuwa limekuwa likifanya kazi ya kumchafua.

Alisema hivi sasa wabunge wanatukanwa bila sababu za msingi na vyombo vya habari ambavyo vinalenga kuharibu utendaji wa Bunge pamoja na kuwapaka matope baadhi ya wabunge.

"Fedha hizi za tarima hata waandishi wa habari mmekuwa mkipewa na zipo nje ya posho zenu mnazopewa na Ofisi zenu. Mbona hilo hamlisemi?" alisema na kuhoji Spika Sitta akirejea hoja iliyotolewa juzi na Mwakyembe wakati akitetea msimamo wake wa kupokea posho mbilimbili na kukataa kuhojiwa na Takukuru.

Sitta aliendelea kwa kusema, mtu yeyote anayetamani na kudhani kuwa wabunge kwa kuwa madarakani, naye anapaswa kujitosa kugombea kugombea mwakani, kwani majimbo yatakuwa wazi.

Naye waziri wa nchi katika Ofisi ya waziri mkuu, sera na uratibu wa Bunge, Phillip Marmo ametofautiana na Takukuru ambayo iliwahoji baadhi ya wabunge kwa madai ya kupokea posho zaidi ya mara moja wanapokuwa kwenye majukumu yao.

Waziri Marmo ambaye alikuwa akizungumza na televisheni ya Taifa(TBC1) juzi usiku, alieleza wazi kuwa , hakuna kipengele chochote cha sheria au kanuni zilizotolewa na serikali zinazozuia wabunge wasilipwe posho zaidi ya moja wakati wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao.

" Hapa hatujaona kosa lolote lililofanyika kwakuwa si Bunge wala serikali walioketi kutunga sheria au kuweka utaratibu unaozuia wabunge wasilipwe posho zaidi ya mara mbili, sio kosa hapa, hakuna utaratibu unaopinga ndio maana hilo limefanyika" alisema marmo kwenye mahojiano hayo.

Wakati Marmo akitoa kauli hiyo, TanzaniaDaima inao ushahidi wa maandishi wa barua iliyoandikwa na waziri mkuu , Mizengo Pinda, Mei26m mwaka huu ikienda kwa Spika wa bunge , ikimtaka kushughulikia tatizo la wabunge kupokea posho mara mbilimbili

Pinda katika barua yake hiyo ambayo ameisaini mwenyewe na nakala kupelekwa kwa Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu kiongozi, Philemon Luhanjo, anaeleza kupokea malalamiko dhidi ya wabunge kutoka katika taasisi kadhaa za serikali


Habari hii imeandaliwa na Rahel Chizoza, Saul Gillard Dodoma na Christopher Nyenyembe Dar.
 
Hili suala la posho mia mia limebainisha ni nani wako kwa ajili ya masilahi yao binafsi na kina nani wapo kwa ajili ya masilahi ya taifa. Hata wakijaribu kupindisha lugha, ukweli unabaki pale pale KULIPWA POSHO KWA SHUGHULI AMBAYO MWAJIRI WAKO KESHAKULIPA NI WIZI MTUPU.
 
Sawa kabisa, Dr Mwakyembe hana haja ya kuchezewa kwa kupigiwa tu simu akaanza kuogopa kana kwamba ni samasi, ni vizuri kama hatua zikachukuliwa kwa Hosea ili ionekane hakuna hila.
Je ni kwanini hawa takukuru wawachague wabunge kwa misingi ya itikadi na msimamo wao? Mbaya zaidi inatamkwa kuwa ni maagizo toka juu, vipi? Hii siyo cheche za kimbari hasa ukiangalia milolongo yote kwa uhusika wa Richmond tangu izaliwe na inakokwenda? Au ni wazo tu la Hosea kwa vile alishalitumia kuwatishia wabunge wakati fulani?
Ningeomba takukuru wamhoji makamu wa Rais aliyelala hoteli moja huko karatu bila kulipa na kutegemea ilipwe na DC au Mkurugenzi, posho yake alipeleka wapi siku hiyo?
Inashangaza zaidi awamu hii wana hoja dhaifu katika kutafuta sababu ya kuwabana wabaya wao. Lamwai alibanwa kwa vile ile awamu ilikuwa na nguvu zaidi
Mwakyembe jipe moyo usiwe goigoi hawana lolote
 
wazee hivi hili swala la posho mbili kwa wabunge limebeba uzito kuliko lile la richmonduli, EPA nk??? maana naona saa hizi attention inahamia pande nyingine. mimi naona waliendeleze kwanza la richmonduli , halafu lije la posho mbili.
 

- Unless kuna maelezo mengine, lakini kama ni haya tu, Mwakyembe yuko sawa sawa na sheria, amekataa kuhojiwa kwa simu kwa sababu sheria haisemi hivyo na cha muhimu amesema wazi tena publicly, hakujifanya amesafiri, hakujifanya mgonjwa, hivi ndivyo inavyotakiwa kwa kiongozi kama yeye, sasa Takukuru watuambie jinsi Mwakyembe alivyovunja sheria kwa kukataa kuhojiwa kwenye simu.

- Leo nimezungumza na kiongozi mmoja mzito sana wa serikali, akaniambia mengi sana kuhusiana na hii ishu, kwa kifupi alisema Takukuru wako wrong kwa sababu hakuna sheria inayowazuia wabunge kupata posho mbili kwa kazi moja, isipokuwa lawenforcement wakitaka kukupata na hatia wanaweza kulazimisha anything,

- Akasema katika miaka yake mingi sana serikalini ni a fact kwamba ni tabia ya maofisa karibu wote wa serikali kucheza faulo za ki-administration katika posho, kwa hiyo kama Takukuru kweli wamepania kulimaliza hili tatizo basi wangeanzia na ofisi ya rais na kushuka chini, akasema yeye ajuavyo ni kwamba bila posho huwezi fanya semina yoyote duniani maofisa au viongozi wakakubali kuhudhuria, na pia akasema kwamba kwa kawaida ni kazi ya katibu mkuu wa wizara kufuatilia suala la posho za maofisa, na anapogundua kwamba kuna faulo, anachofanya ni kumjulisha anayehusika na kumkata mshahara wake mpaka hela zote zirudishwe, au kumlazimisha aazirudishe haraka sana kama anazo.

- Na kwamba kama kweli huko bungeni kuna faulo imechezwa na wabunge on posho, alisema for now dawa ilikuwa ni kuwalazimisha wazirudishe kwa kuwakata malipo yao bila mijadala ya Takukuru na uchunguzi wa bunge, na ndivyo exactly tunachosema kama imevunjwa sheria, basi wahusika watupwe Segerea mara moja, lakini kama iliyovunjwa ni siasa, basi wasitusumbue na kelele za bure!

- Maana sijawahi kusikia jambazi au mhalifu yoyote yule duniani akihojiwa kwa simu, I meana hata Banana Republic wana standards japo kidogo lakini not this low!

Respect.


FMEs!
 
NIKATIKA KAZI-"wazee hivi hili swala la posho mbili kwa wabunge limebeba uzito kuliko lile la richmonduli, EPA nk??? maana naona saa hizi attention inahamia pande nyingine. mimi naona waliendeleze kwanza la richmonduli , halafu lije la posho mbili."

Watu mnakosea sana. huu mjadala wa posho mbili ni sawa na TAKUKURU kuamsha hasira za wabunge...nakwambia wabunge wakibanwa hadi wakaumbuka, utaona siku ya jumatano wakati wa mjadala wa Richmond. kila mbunge atakuwa anataka kuosha ili kurejesha imani. na wataishughulikia TAKUKURU kwelikweli... we acha Hosea aendelee kuwachokonoa mpaka jumatano...sisi wananchi tunafurahia. acha serikali na bunge wapalulane...ugomvi wa nzige ni furaha ya kunguru!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…