Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
wazee hivi hili swala la posho mbili kwa wabunge limebeba uzito kuliko lile la richmonduli, EPA nk??? maana naona saa hizi attention inahamia pande nyingine. mimi naona waliendeleze kwanza la richmonduli , halafu lije la posho mbili.
Swala la Posho ni kosa, lakini haliwezi ondolewa kwa kosa jingine la PCCB kuwahoji Wabunge wakati yaonyesha wazi kabisa kwamba Waziri mkuu alisha wasilisha malalamiko yake Bungeni na hayakupewa kipaumbele na wahusika..
Sote tunakubaliana na makosa haya ya Wabunge na yapo mengi sana lakini hatuwezi vunja sheria kwa sababu ya kuwafurahisha baadhi ya watu. Kama swala hili lingekuwa muhimu, bunge lingezungumzia na kuweka sheria dhidi ya posho hizi, lakini maadam Sitta na katibu wake walighairi barua ya waziri mkuu, wakashindwa kuonya vitendo hivyo wazi isipokuwa kwa kupitia mlango wa nyuma..wanaotakiwa kuhojiwa ni Spika Sitta na katibu wake.
Sheria inasema wazi kabisa kwamba wabunge wetu wamepewa kinga na sheria jambo ambalo nashindwa kuelewa viongozi wetu huitumia tu pale wao wanapokuwa ktk mshikemshike..
Haiwezi kuhalalisha tabia hii kumhukumu Mwakyembe ambaye amekataa kuhojiwa kwa sababu ni utaratibu mbovu uliotumika.
Two mistakes can't it right!
Ewe mtoa mada nadhani una ubia na ufisadi. Unadandia mada. Hili tatizo halitaisha mapema. Hata kama mwakyembe sio safi, hao kina hosea umewazungumziaje? Tafuta kinga, usikimbilie kutibu
Nina ubia upi na ufisadi? Hii mada inamhusu Dkt Mwakyembe, ya Dkt Hoseah unaweza kuianzisha hata wewe, hakuna aliyekukataza! Nikianzisha ya Dkt Hoseah utauliza tena mbona sijaanzisha mada ya Dkt Slaa! One thread at a time pls!
TanzaniaDaima,Oktoba30,2009
SLAA AMSHANGAA MWAKYEMBE.Katika hatua mpya, Mbunge wa Karatu na mwasisi wa mapambano ya ufisadi ndani na nje ya Bunge, Dr Willibrod Slaa, amejitokeza na kueleza kusikitishwa na hatua ya mbunge wa Kyela , Dr Harrison Mwakyembe kukataa kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) kuhusu tabia hiyo ya wabunge kupokea posho mara mbilimbili.
- Asema iwapo ni mtu safi kwanini anaogopa Takukuru?
Hata kama kupokea posho mara mbili ingekuwa ni kuvunja sheria, kwa nini mtu yeyote aamini utendaji wa TAKUKURU iliyowahi kuibariki Richmondgate hasa wakati huu wa kuijadili Ripoti ya Richmond?
Dr. Slaa amekosea na uamuzi wa Dr. Mwakyembe ni sahihi na wa hiari yake na haupaswi kujadiliwa kwa vile TAKUKURU ilishajivua uhalali wa kupambana na rushwa.
Haya yale yale ya hisia pole sana mzee. but tutajitahidi kuvumiliana, mimi siku hizi nimekuwa na mango tree.wewe ndiye umeishiwa na hiyo mango tree yako.
tangu mwanzo tulisema mwakyembe haishi kutapatapa.amegombana na madiwani karibia wote kyela,kagombana na uongozi wa ccm wilaya,kagombana na mkuu wa mkoa,kagona na polisi kwa kumtetea dereva wake na sasa yuko pccb.huyo kweli ni kiongozi gani,mpenda ugomvi na mwenye majivuno kiasi hiki.yeye kitu anachoamini ndicho hicho.
Ukiangalia jimbon,hakuna kitu zaidi ya kukimbilia kwenye media na kusema anaonewa.safari atakwenda tu na sijui utafanya nini na mangotree yako
majibu:Two wrong can not make a right. Never. If PCCB was wrong on Richmond it does not mean that Mwakyembe should also do wrong to make it right! Ni kosa kukataa amri halali ya chombo cha dola kuhojiwa hata kama ni upuuzi. Hata kama Mwakyembe alipata ushujaa katika kufumua kashfa ya Richomnd haimfanyi kuwa juu ya sheria na baya zaidi kuliweka hadharani. Ni kwa nini aliweke hadharani ili iweje kama sio kutafuta cheap popularity? It think it is being low to be zealot supporter of Mwakyembe even when it is clear he has goofed. I think He is overstreched himself this time around.
1. Tangu Dkt Harrison George Mwakyembe ajigambe kwamba anapambana na ufisadi, hasa baada ya Ripoti ya Richmond mwenendo wake katika upambanaji huo bado haujaeleweka hasa katika kauli zake na matendo yake!
2. Baada ya Ripoti ya Richmond alidai kwamba kuna mambo ambayo wao (wanakamati teule) waliyaacha (hawayakuyafanyia kazi) "ili kulinda heshima ya Serikali!" Hii Serikali ni ipi ambayo heshima yake ilitakiwa ilindwe maana Waziri Mkuu wa wakati huo, Edward Lowasa alitakiwa apime uzito mwenyewe, na kweli Lowasa alipima uzito na kuachia ngazi. Vile vile mawaziri Msabaha na Karamati waliachia ngazi. Sasa Serikali ipi ambayo Kamati Teule ilikuwa inailinda? Hapa tuliachwa vinywa wazi kuhusu dhamira hasa ya "wapambanaji" hao.
3. Kabla vumbi halijatua tukasikia kwamba Dkt Mwakyembe alijihusisha na umeme wa upepo na haku-declare interest wakati alipokuwa anaongoza Kamati Teule kuhusu Richmond. Japokuwa Mwakyembe alijitahidi kueleza sana kwamba alitakiwa a-declare "pecuniary interest" (financial interest) na sio vinginevyo kulingana na Kanuni za Bunge, katika suala nyeti kama hilo alitakiwa aliweke wazi ili kusionekane kuwa kuna mgongano wa maslahi! Hata hiyo aliyodai kuwa ni "pecuniary interest" ni subject to interpretation kiasi kwamba suala la umeme wa upepo linaweza kuwekwa kwenye mukhtadha huo!
4. Dkt Harrison George Mwakyembe aliitwa majuzi na TAKUKURU kwa ajili ya kueleza uhalali wa kupokea posho mara mbili akadai, tena kwa dharau kubwa kwamba, amekataa kwenda kwa sababu eti Dkt Edward Hosea, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, suala lake bado linachunguzwa na kwamba nia ya TAKUKURU ni kuwaziba midomo "wapambanaji." Hoja iliyopo ni kwamba, Je, kupokea posho mara mbili toka kwenye Serikali hiyo moja kwa kazi ile ile sio kosa? Katika maelezo ambayo Dkt Mwakyembe amekuwa anayatoa kwa waandishi wa habari ameeleza kwamba suala la kupokea posho zaidi ya mara moja kwa kazi ile ile limeanza muda mrefu! Huyu Mwalimu Mwanasheria akumbuke kwamba hatuongelei practice (mazoea) bali tunaongelea sheria na uhalali wa malipo hayo. Maelezo yake kwamba TAKUKURU nao waliwahi kuwalipa posho mara mbili hayana mshiko kwa sababu TAKUKURU ndio waliowaita kwenye Semina hizo na walistahili kuwalipa. Sasa kama waliapply posho kule Bungeni TAKUKURU wangejuaje kama wamelipwa Bungeni. Kwa nini Wabunge hawakuzikataa hizo posho?
5. Kuhusu Dkt Harrison George Mwakyembe kukataa kuhojiwa na TAKUKURU kwa madai ya kuwa na kinga na kwamba bunge ni muhimili kamili! Kama Bunge ni muhimili kamili, mbona Kamati Teule ya Bunge iliwahoji Utawala ambao pia ni muhimili kamili wa dola? Hivi mipaka ya kinga ya wabunge inaishia wapi? Mbona wakati akina Mramba walipohojiwa hatukusikia juu ya kinga za bunge na wabunge? Hii kinga inawahusu "wapambanaji" tu! Hebu tuangalie Ibara ya 100(1) na (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria na. 15 ya mwaka 1984 kuhusu kinga ya Bunge kama alivyodai Dkt Mwakyembe: "100 (1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge. (2) Bila kuathiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo."
Ukisoma between lines utaona kwamba kinga ya Bunge ni ndani ya Bunge wakati wa majadiliano na kinga hiyo inahusu uhuru wa kutoa mawazo tu! Sasa hapa mambo ya kulipwa posho zaidi ya mara moja yanaingiaje?
Kwa hiyo Dkt Mwakyembe asijifiche kwenye kivuli ambacho hakipo, atekeleze Kifungu cha 10 (1) (a) na (c) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, 2007, Na. 11/2007 kinachomtaka aitikie wito anapoitwa kuhojiwa! Akisubiri aje akamatwe kwa kukataa kuitikia wito asifikiri kwamba ndio karata ya kisiasa ya kupanda chati, asome alama za nyakati, haziko upande wake kwa sasa!
6. Kwa maelezo hayo machache hapo juu, bado sijaelewa upambanaji wa Dkt Mwakyembe na wenzake katika vita dhidi ya ufisadi ambayo inapiganwa bila kuwafahamu kwa majina mafisadi wenyewe!
Siasa za Bongo ni kichekesho kitupu. Hivi msafi ni nani? Yesu hakusema urongo kuwa "ukuhukumu utahukumiwa" "toa boriti kwenye jicho lako ndipo utoe kibanzi kwenye jicho la mwenzako".
Kwa taarifa hizi hata mimi napata mashaka na nia ya wapiganaji wa ufisadi kama ni kweli wanapiga kelele kwa kutupenda walala hoi na nchi yao ama kuna ajenda nyuma ya pazia.