Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,972
majibu:
jambo moja umesahau ni haki yako kukataa kuhojiwa na chombo ambacho huna Imani nacho, inawezekanaje TAKUKURU ambayo kamati ya Mwakyembe imewanyoshea kidole kuja kumuhoji na kumtendea haki Harrison Mwakyembe(mb),
alichofanya ni sahihi, na ndio maana amemwambia Hosea akiwa tayari wakakutane mahakamani.
kumbuka Mengi aliwahi kumgomea Waziri Masha kua hawezi kutoa maelezo yake polisi akiweza atangulie mahakamani, ni haki yako Mtanzania mwenzangu kukataa kuhojiwa na vyombo unavyohisi havitakutendea haki.
Hakuna haki ya kukataa wito, that right doesn't exist at all! Mtuhumiwa ana haki ya kutotoa maelezo lakini sio kukataa wito! Kifungu cha 10 (2A) cha CPA, 1985 kinasema kwamba ni kosa la jinai kukataa wito wa chombo cha dola. Mengi alipewa na Masha siku saba za kutoa maelezo na sio kumpa WITO wa kufika ofisini, tusichanganye vitu viwili hapa (WITO vs KUHOJIWA)! Hebu jiulize mwenyewe, kama huna imani na mahakama kwa kuwa inaongozwa na Jaji Mkuu ambaye ni corrupt hutaenda ukipewa summons kwa kuwa huna imani na chombo hicho? Where then is the checks and balances that is supposed to exist in a democratic country? Kamati ya Mwakyembe nao si waliwahoji watu wakati wa kufuatilia suala la Richmond? Mbona hawakuambiwa kwa kuwa wao (akina Mwakyembe) wanapokea posho mara mbili kwa kazi moja (ambao ni wizi) hawana uwezo wa kuwahoji akina Msabaha na Karamagi ambao walikuwa ni mawaziri? Why can't you simply be reasonable?