Mtu yeyote anayechukua posho mara mbili kwa kazi ile ile anafanya makosa bila kujali ni rais wa nchi, waziri, mbunge au diwani wa kata.
Tusitetee mtu hapa na badala yake tutetee sheria. Kama kwa kupambana na mtu mmoja serikali imefungulia mkondo wa maji, hilo ni jambo jema kwa taifa maana ni nafasi ya kuwaumbua wote wanaofanya hivyo.
Nashangaa kuna watu wanakuja hapa na kusema kuchukua posho mbili sio kosa, inaonyesha jinsi Watanzania tunavyoshindwa kuelewa na kuheshimu sheria na maadili.
Hata kama PCCB ni wabovu mno lakini kweli utawalaumu pale wanapoamua kumhoji mtu ambaye amefanya kosa?
Tunajua polisi ni wala rushwa, kweli utawalaumu siku wakiamua kukukamata kwasababu umekula rushwa?
Ukitenda kosa usitafute mchawi na badala yake mchawi ni wewe mwenyewe. Mtu yeyote anayepigania jambo fulani lazima ajiangalia kwenye kioo na kuona yeye mwenyewe ni msafi, vinginevyo wabaya wake watammaliza na hilo ni kila sehemu hapa duniani.