Dr. Mwakyembe Vs. TAKUKURU

Dr. Mwakyembe Vs. TAKUKURU

wahenga walisema kuchamba kwingi mwishowe kuondoka na mavi
 
Tunashangazwa na mpambambanaji mkuu aliyejifanya kuwa kamwe hawezi kuhojiwa na PCCB kwa kuwa yeye anaelewa sheria na pia na Mwalimu wa sheria.yeye kwa akili yake alifikiria kuwa anamgomea EH kumbe anafunja sheria ya nchi.Sheria ni msemeno hajali kuwa aliyefunja sheria ni Dr. wa sheria kosa ni kosa tu.Huo ubabe wake alioutangazia Dunia uko wapi?Kama kweli tume yake imefanya haki katika kuchunguza RM kwa nini aogope kuundwa Tume Huru ya kuchunguza ukweli kuhusu sakata la RM? Anawataka wa TZ.tukubaliane na kila jambo analosema eti kwa sababu yeye Mwalimu wa sheria.Yeye achunguze, ahukumu na atoeasi adhabu.haki iko wapi?Watuhumiwa hawapewi nafasi ya kujitetea sijui ni sheria zipi anazositui Dr.Sheria.Wasi wasi mkubwa unadhihirika pale Dr. wa sheria anapopinga kwa nguvu zote kuundwa kwa tume huru ya kupitia upya mapendekezo hayo.Anaogopa nini kama kweli tume yake haikumwonea mtu.Rm ndio ulikuwa mtaji wake kwa hiyo aliogopa kuumbuliwa mbinu zake
 
Moelex, hapo unapowaelekeza ni maua tu, mizizi iko huku
watendaji wa mitaa
polisi post
vyuoni
tawala za mikoa
mahospitali
mpirani
gesti
kwenye kulipa bili za maji na umeme

halafu zikitoka huko ndio zinakua maana watu wanaanza kuona tangu wanazaliwa... kama tunataka kupiga vita rushwa sustainably, basi tuanzie pia sio juu pekeyake

Well said MTM, tuko pamoja katika hili, tusipoanzia huku hatuwezi kamwe kutibu haka kaugonjwa
 
Pamoja na kuwa Dr. Mwakyembe ni mwanasheria mzuri lakini hakufanya research ya kutosha kabla ya kukutana na waandishi wa habari kutoa tamko kuwa kamwe hawezi kuhojiwa na PCCB.
 
Tunashangazwa na mpambambanaji mkuu aliyejifanya kuwa kamwe hawezi kuhojiwa na PCCB kwa kuwa yeye anaelewa sheria na pia na Mwalimu wa sheria.yeye kwa akili yake alifikiria kuwa anamgomea EH kumbe anafunja sheria ya nchi.Sheria ni msemeno hajali kuwa aliyefunja sheria ni Dr. wa sheria kosa ni kosa tu.Huo ubabe wake alioutangazia Dunia uko wapi?Kama kweli tume yake imefanya haki katika kuchunguza RM kwa nini aogope kuundwa Tume Huru ya kuchunguza ukweli kuhusu sakata la RM? Anawataka wa TZ.tukubaliane na kila jambo analosema eti kwa sababu yeye Mwalimu wa sheria.Yeye achunguze, ahukumu na atoeasi adhabu.haki iko wapi?Watuhumiwa hawapewi nafasi ya kujitetea sijui ni sheria zipi anazositui Dr.Sheria.Wasi wasi mkubwa unadhihirika pale Dr. wa sheria anapopinga kwa nguvu zote kuundwa kwa tume huru ya kupitia upya mapendekezo hayo.Anaogopa nini kama kweli tume yake haikumwonea mtu.Rm ndio ulikuwa mtaji wake kwa hiyo aliogopa kuumbuliwa mbinu zake

Mada yako ni ipi?
ilete hiyo mada niliyoinukuu kwa rangi tuijadili! usidandie treni kwa mbele!
 
Hatimaye mpiganaji ameamua kutii Sheria ya Nchi ambayo ameshiriki mwenyewe kuitunga? Halafu siku hizi haongei sana kwa kuwa kitu kilichompatia umaarufu, Richmond, kimewekwa kapuni, kwa hiyo mtaji wa kisiasa ume-expire?
U are such a HATER tu wewe sasa hapo unataka kusema nini, hivi ulitaka kitu hii ishu inyamaziwe tuu kama wewe si kibaraka mchakavu wa hao walarushwa????!@#$%^&
 
je wewe kama wewe ulitaribu uthubutu alo utenda japo punje ya ulezi? Sifia panapostahili .ok mungu atakutoa huko gizini ulipo akulete kwenye mwanga ili upambanue cheupe na cheusi.
Bosi wa walinzi wa walarushwa (TAKUKURU) akiwa mchafu ahina maana ofisi imekufa na kwamba ukatae kwenda kuhojiwa..ni jukumu letu kupiga kelele hivi hivi ili boss aondoke na ofc iwe safi na ifanye kazi kwa makusudio yaliowekwa period!
 
hilim lijamaa liwe la kwanza kupelekwa mahakamani kwa nguvu ya Mungu alie hai kwa kuwa hili nalo ni jizi kama majizi mengine yote.
 
watu kwa kweli wana matatizo; tatizo halikuwa Mwakyembe kuhojiwa na TAKUKURU; tatizo lilikuwa huwezi kuwa subpoena wabunge wakiwa kwenye kikao ni kinyume na Katiba! Alipoingia AG mpya aliwatumia ujumbe kina TAKUKURU kuwa hawawezi kufanya hivyo na ndio HOsea akakimbia Dodoma maana kingemuungulia na ndio sababu wao kusitisha uchunguzi wao hadi kikao kilipoisha.

Nje ya kikao cha Bunge unaweza kumuita mbunge kumhoji kirahisi tu!

Mzee Mwanakijiji,

PCCB walivyotaka kumhoji Dr. Mwakyembe mara ya kwanza hakukuwa na kikao cha bunge na in fact yeye Dr. alikuwa jimboni kwake.

Nafikiri kukataa kwake kulikuwa ni kwasababu tofauti na hiyo uliyoiandika hapo juu.
 
watu kwa kweli wana matatizo; tatizo halikuwa Mwakyembe kuhojiwa na TAKUKURU; tatizo lilikuwa huwezi kuwa subpoena wabunge wakiwa kwenye kikao ni kinyume na Katiba! Alipoingia AG mpya aliwatumia ujumbe kina TAKUKURU kuwa hawawezi kufanya hivyo na ndio HOsea akakimbia Dodoma maana kingemuungulia na ndio sababu wao kusitisha uchunguzi wao hadi kikao kilipoisha.

Nje ya kikao cha Bunge unaweza kumuita mbunge kumhoji kirahisi tu!
.

Lakini Mwakyembe alipoitwa mara ya kwanza na kukataa kuhojiwa,Hakukuwa na kikao chochote cha Bunge kilichokuwa kikiendelea..Kama alivyofafanua yeye mwenyewe kuwa alikahidi kutokanna na kwamba hakuona sababu yeyote ya kuhojiwa.
 
.

Aliambiwa tangu mwanzo kuwa hakuna aliyejuu ya sheria?Yeye akaleta u richmond .Ohoo mbona mwenyewe pccb walinipa posho .ohoo.mimi mwanasheria niliye bobea.ohooo mbona waandishi wa habari wanakunywa chai yetu.Ujinga mtupu.Mnakula pesa za wananchi halafu mnajifanya waasafi.Pumbavu.acha sheria ichukue mkondo wake.
Samwel unashangaza JF yote, maana inaonekana wazi unachuki na hawa wabunge mahiri tena wa kwanza nchini kutoka chama cha mafisadi. Tulia kidogo ungoje watakayoyafanya na kufichua pale TAKUKURU watapomaliza kuwahoji au kuwatishia. Itaanza movement ya aina yake ambayo hizi posho zote zitabidi zianikwe ndipo na Ikulu itakapochafuliwa. Wabunge hapa wamejikuta wameingizwa mjini lazima wote wakubali. Maana walizidiwa ujanja pale walipopitisha mswada wa kuanzisha TAKUKURU lakini hawakujua kuwa wamemwongezea tena mkono mrefu Rasi, hawakuweza kuweka hata kipengele kuwa wao ndiyo wamchague kiongozi wa hiyo taasisi, sasa imewageuka mara ya pili. Ya kwanza ni pale walipojaribu kufukia ukweli wa mambo ya Richmond na sasa kuwahoji kwa nia ya kuwatisha. Wakisha hojiwa wakaja wamepoa wakaacha mapambano kitakuwa kimeeleweka. Na wasipolifanyia kazi swala zima la posho mbili mbili serikalini na nyingine za aina hiyo tutajua kuwa wameshapatiwa kile alichopata mbunge mtegemewa akaanza kutetea Richmond.
 
Punguzeni jazba jamani yeye aligoma bse kulikuwa na conflict of interest pale as it was time to discuss the richmond alafu uyo uyo mnaetaka kumtia adabu anataka kuwahoji.Huoni kuwa alikuwa anataka kushusha munkari wa kuidiscus richmond bungeni which to me naiita UNDUE INFLUENCE au greasing wabunge waache kukomaa na Hosea ktk sakata la richmonduli
 
Hatimaye mpiganaji ameamua kutii Sheria ya Nchi ambayo ameshiriki mwenyewe kuitunga? Halafu siku hizi haongei sana kwa kuwa kitu kilichompatia umaarufu, Richmond, kimewekwa kapuni, kwa hiyo mtaji wa kisiasa ume-expire?
Avatar yako na hiyo comment , they do not tally.
 
Taarifa nilizozipata kutoka nyumbani Tanzania zinaeleza kwamba makamanda wawili maarufu wa vita ya ufisadi, Dk. Harrison Mwakyembe na Fred Mpendazoe, wamehojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Takukuru juzi kuhusiana na suala la posho mbili za wabunge.

naomba kuwasilisha

Double payment ya hela za umma siyo rushwa, hayo ni masuala ya fedha na mtu anayepokea fedha mara au fedha bila kufanyia kazi adhabu zake zinajulikana na zipo wazi. PPCB wanashindwa kutekeleza majukumu yao na wanavamia wapiganaji baada kamati ya Mwakeyembe kependekeza Hosea atimuliwe. Wakitaka rushwa zinaumiza wananchi waende halmashauri, hospitali za umma, mikataba ya madini, watu wanaopanga bei kama EWURA (mafuta), BOT(exchange rate), nauli za ndege za ndani etc.
 
Samwel unashangaza JF yote, maana inaonekana wazi unachuki na hawa wabunge mahiri tena wa kwanza nchini kutoka chama cha mafisadi. Tulia kidogo ungoje watakayoyafanya na kufichua pale TAKUKURU watapomaliza kuwahoji au kuwatishia. Itaanza movement ya aina yake ambayo hizi posho zote zitabidi zianikwe ndipo na Ikulu itakapochafuliwa. Wabunge hapa wamejikuta wameingizwa mjini lazima wote wakubali. Maana walizidiwa ujanja pale walipopitisha mswada wa kuanzisha TAKUKURU lakini hawakujua kuwa wamemwongezea tena mkono mrefu Rasi, hawakuweza kuweka hata kipengele kuwa wao ndiyo wamchague kiongozi wa hiyo taasisi, sasa imewageuka mara ya pili. Ya kwanza ni pale walipojaribu kufukia ukweli wa mambo ya Richmond na sasa kuwahoji kwa nia ya kuwatisha. Wakisha hojiwa wakaja wamepoa wakaacha mapambano kitakuwa kimeeleweka. Na wasipolifanyia kazi swala zima la posho mbili mbili serikalini na nyingine za aina hiyo tutajua kuwa wameshapatiwa kile alichopata mbunge mtegemewa akaanza kutetea Richmond.

Mtu yeyote anayechukua posho mara mbili kwa kazi ile ile anafanya makosa bila kujali ni rais wa nchi, waziri, mbunge au diwani wa kata.

Tusitetee mtu hapa na badala yake tutetee sheria. Kama kwa kupambana na mtu mmoja serikali imefungulia mkondo wa maji, hilo ni jambo jema kwa taifa maana ni nafasi ya kuwaumbua wote wanaofanya hivyo.

Nashangaa kuna watu wanakuja hapa na kusema kuchukua posho mbili sio kosa, inaonyesha jinsi Watanzania tunavyoshindwa kuelewa na kuheshimu sheria na maadili.

Hata kama PCCB ni wabovu mno lakini kweli utawalaumu pale wanapoamua kumhoji mtu ambaye amefanya kosa?

Tunajua polisi ni wala rushwa, kweli utawalaumu siku wakiamua kukukamata kwasababu umekula rushwa?

Ukitenda kosa usitafute mchawi na badala yake mchawi ni wewe mwenyewe. Mtu yeyote anayepigania jambo fulani lazima ajiangalia kwenye kioo na kuona yeye mwenyewe ni msafi, vinginevyo wabaya wake watammaliza na hilo ni kila sehemu hapa duniani.
 
Afadhali amekubali maana angeendelea kubisha yangemkuta yaliyomkuta Sendeka wangempa kesi ya kukataa amri halai ya kuitwa kuhojiwa.

Bravo Mwakyembe umekwepa mtego wa mafisadi
 
Tunashangazwa na mpambambanaji mkuu aliyejifanya kuwa kamwe hawezi kuhojiwa na PCCB kwa kuwa yeye anaelewa sheria na pia na Mwalimu wa sheria.yeye kwa akili yake alifikiria kuwa anamgomea EH kumbe anafunja sheria ya nchi.

Maneno yako yanadhihirisha kwamba una chuki binafsi dhidi ya Mwakyembe tena chuki mbaya! Sidhani kuna sehemu yoyote ambayo Mwakyembe alisema kuwa KAMWE hawezi kuhojiwa na PCCB 'kamwe' ni neno zito! Kama angelikuwa anavunja sheria ya nchi basi angelifunguliwa mashitaka mahakamani na si kuitwa PCCB.

Sheria ni msemeno hajali kuwa aliyefunja sheria ni Dr. wa sheria kosa ni kosa tu.Huo ubabe wake alioutangazia Dunia uko wapi?Kama kweli tume yake imefanya haki katika kuchunguza RM kwa nini aogope kuundwa Tume Huru ya kuchunguza ukweli kuhusu sakata la RM? Anawataka wa TZ.tukubaliane na kila jambo analosema eti kwa sababu yeye Mwalimu wa sheria.Yeye achunguze, ahukumu na atoeasi adhabu.haki iko wapi?Watuhumiwa hawapewi nafasi ya kujitetea sijui ni sheria zipi anazositui Dr.Sheria.

Ubabe gani? Mwakyembe alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge iliyopewa jukumu la kuchunguza kashfa ya Richmond. Kwa maana nyingine yeye na kamati yake walipewa kazi na Bunge zima wakiwemo watuhumiwa (wengi wape) kuifanya kazi hiyo. Bunge likaipokea ripoti ile na kutoa mapendekezo ya nini Serikali ifanye kuhusu yale yaliyokuwa kwenye ripoti ile na Serikali iliipokea ripoti hiyo kwa 'unyenyekevu' na kuahidi kuyafanyia kazi mapendekezo. Ubabe wa Mwakyembe unatoka wapi? Labda useme ubabe wa Bunge. Kama Mwakyembe alifanya na kusema lolote kuhusu Richmond ni kwa baraka za Bunge lililomteua kuwa Mwenyekiti wa Kamati ile. Ulitaka akae kimya kama kondoo pale inapobidi aseme ama kujibu shutuma dhidi yake na Kamati aliyoiongoza?[QUOTE]

Wasi wasi mkubwa unadhihirika pale Dr. wa sheria anapopinga kwa nguvu zote kuundwa kwa tume huru ya kupitia upya mapendekezo hayo.Anaogopa nini kama kweli tume yake haikumwonea mtu.Rm ndio ulikuwa mtaji wake kwa hiyo aliogopa kuumbuliwa mbinu zake

Tume huru ya kupitia mapendekezo gani wakati mapendekezo yalishapokelewa na Serikali na yanafanyiwa kazi? Alichokisema 'boss' wako ni kutaka jopo la majaji ndilo lianze kushughulikia suala la Richmond upyaa akijua kwamba keshaharibu na kufunika ushahidi wote wa maana ambao tayari Kamati ya Bunge iliweza kuukusanya. Na kwa hulka yake atakuwa keshajua ni majaji gani walioupande wake atakaotaka wateuliwe. He is a 'king maker' you know! Lolote kwake linawezekana.
 
Ni aibu kufika hapa tulipo kama Taifa,tumeonyesha udhaifu mkubwa mno katika mfumo wetu mzima wa kutafuta viongozi.Nafikiri tuelekeze utaalamu wetu,nguvu zetu na akili zetu kujadili mabadiliko ya kimfumo yanayohitajika sasa badala ya kupoteza wakati kuwajadili watu.
 
Back
Top Bottom