Dr. Mwakyembe Vs. TAKUKURU

Mkuu hakuna utetezi sana hapa bali utanielewa vizuri zaidi pale mwisho. Maana haya mswala ya posho mbili yameenea sana Serikalini. Ninaimani hakuna atakayepona katika hili si ofisi ya raisi si ofisi ya waziri mkuu. Uchunguzi wa kina ukifanyika double payments zipo za aina nyingi sana! Ni nani atakayekwenda kuchunguza Ofisi ya Waziri Mkuu?, Ikulu? Ni Hosea?? Ndiyo maana watapigana kufa na kupona kisiingie chama kingine kushika usukani wa Serikali. Na kama itatokea tukiwa hai nakuomba ukumbuke hii thread wakati madudu yatakapokuwa yanafumuka.
 
.

Mkuu.mbona unaongea pumba.Ninaishangaza JF?Wewe ni kiongozi wa JF?.Umejuaje kama kila mwana Jf anashangaa?.upeo wako mdogo mzee rudia tena kusoma post zangu.
 
.

Mkuu wangu Mpenda tz.
Heshima mbele.Unashangaza sana mzee wangu.kama posho mbili zimeenea serikalini kwa hiyo dawa ni kuzihalalisha?hehehe.Kwa mtaji huu kweli tutafika?
 
Afadhali amekubali maana angeendelea kubisha yangemkuta yaliyomkuta Sendeka wangempa kesi ya kukataa amri halai ya kuitwa kuhojiwa.

Bravo Mwakyembe umekwepa mtego wa mafisadi
.

Afadhali yaliyomkuta Sendeka.Yaliyomkuta marehemu Kolimba je?
 
Mwakyembe alikataa kuhojiwa na TAKUKURU as a matter of principle kwamba wao walipendekeza kwenye tume yao kuwa Kiongozi wa Takukuru aadhibiwe kwa kupindisha ukweli; sasa kabla ya serikali kutekeleza agizo hilo la bunge wakaja na spin ya kutaka kuwathibiti wabunge kwa kupokea posho mbili mbili!! Sasa kama Mwakyembe amekubali kuhojiwa kabla ya Serikali kutimiza maagizo ya bunge maana yake hakuwaanaamini hoja iliyomsukuma awali kukataa kuhojiwa kabla ya mkuu wa Takukuru kuwajibishwa! Sasa hiyo ni weakness ambayo hapo baadae itamgharimu kwani hawa Takukuru lazima watamtafutia sababu ya kumtia hatiani na kudilute uadilifu ulioomyeshwa na kamati yake; na hilo ndio lengo lA SERIKALI!! He should have stuck to his guns!!
 
Mbunge wa Kyela Dkt Harisson G Mwakyembe alipokataa kuhojiwa na TAKUKURU kuhusu mambo ya posho mbili vyombo vya habari viliandika sana na wengine walimwona kama ni shujaa kwa kitendo hicho cha kukataa! Nilitegemea kwamba baada ya kujisalimisha TAKUKURU au kukamatwa kwa Mwakyembe na TAKUKURU basi vyombo vya habari vingeandika, unless taarifa iliyoandikwa humu JF ilikuwa haina ukweli wowote! Kama ina ukweli basi vyombo vya habari esp magazeti yaleyale yaliyoandika habari za kukataa kuhojiwa yangeandika! Wapambe wa Mwakyembe wanaweza kudai kwamba kuandikwa kwa habari za kuhojiwa kuna maslahi gani kwa nchi? Swali langu kwao ni kwamba kuandika habari za kukataa kuhojiwa kwa Mwakyembe, kitendo cha kuvunja Sheria ya nchi, kuna maslahi gani kwa taifa?
 
Under fair ground they suppose to report the same as they did on the first issue.
 
Jamani,

Kuhojiwa kwa Dk. Mwakyembe kumetangazwa na gazeti la Mtanzania na kichwa cha habari kikubwa kuwa "Mwakyembe ahojiwa", toleo Na. 4960 la Ijumaa Des. 11, 2009. Kwa mujibu wa habari hiyo, Mbunge huyo wa Kyela amehojiwa baada ya kuwekewa bayana hatari itakayomkuta mbele kama atakataa kuhojiwa, kwamba angekamatwa na maofisa wa TAKUKURU na wangemuhoji na kumfungulia shitaka jipya la kukaidi wito halali wa TAKUKURU. Chanzo cha habari hizo kinasema TAKUKURU walikuwa wanatekeleza maelekezo ya Spika aliyetaka Wabunge wahojiwe kwa aibu ya kuchukua posho mara mbili mbili kiwizi! Alisalimu amri akahojiwa. Subirini, labda ataitisha Mkutano wa Waandishi wa habari kuelezea, kama alivyofanya awali wakati anakaidi kuhojiwa!

Bwassa
 
sasa imethibitika na kubainika kua iliandikwa Buchanan ulitaka kutudanganya ?
 
Kwa hiyo kukataa kwake kulikuwa tu geresha! Presha kidogo tu kabend! Ha ha ha ha ha! Ndio kamanda wa vita against ufisadi - my ass
 
Kwa hiyo kukataa kwake kulikuwa tu geresha! Presha kidogo tu kabend! Ha ha ha ha ha! Ndio kamanda wa vita against ufisadi - my ass

Hee!
Tumefikia huko kweli?
Did you mean it?
 
Takukuru ikamuhoji pia na mzee wa kagoda na mzee wa kiwira bana,inahoji udaga inaacha jodari😱
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…