Dr. Mwakyembe Vs. TAKUKURU

Dr. Mwakyembe Vs. TAKUKURU

Ndugu zangu, ............................................. Suala hili ni zito sana. Ni kashfa ambayo inaweza kuwa ya historia na ni kashfa ambayo inaweza kubadili mfumo uliojikita ambao sisi wenye madaraka fulani fulani tunafaidika na uoza uliopo. Hili sio jambo la kuchezeachezea hata kidogo. Kumbukeni kashfa ya malipo ya aina hii ilimwangusha Spika wa Uingereza hivi majuzi..........

Zitto,
Tunafahamu mengi sana kuhusu tabia hii ya wabunge kupenda extras. Kamati za bunge ni nuisense.

Kama ni malalamiko juu ya tabia hiyo kwa kweli ofisi za serikali zinajieleza kwa mengi saana. Wabunge mulishakuwa sugu.

Kinachonishangaza juu ya hili ni PCCB kulitekeleza kama kulipa kisasi kwa kuwaita wabunge selectively na kuwaacha wale ambao ni mawaziri. Kuanzia 2006 naweza kusema ni Wabunge woote wamesha ramba double payments, Pinda inclusive. Hapo kwa binadamu kama mimi topic hugeuka na kuwa witch-hunting.

Hata kama sheria imefuatwa, kwa idadi ya wabunge lazima iwe random exercise na siyo selective implementation. Mbaya zaidi ni PCCB ya Hosea ambayo ina sifa za kutosema ukweli wa wazi. Mbaya zaidi PCCB pia ilichunguzwa na tume ya Bunge. Pia ni mbaya kwamba ni hatua inayochukuliwa wakati Bunge linaelekea kuanza vikao, ndani yake kukiwa na mambo ya Richmond ambayo PCCB ilikuwa accused kwa kuyaficha.

Do I need to be intelligent to express my doubts on the move?
 
Jamani Watanzania tusichanganye MADAWA- Hapa TAKUKURU inataka kutekeleza wajibu wake. Sheria na Kanuni za malipo ya Posho zinasema Mtumishi au Mtu au Taasisi haiwezi kulipwa zaidi ya mara moja kwa ajili ya suala hilo hilo. Sasa hawa Wabuneg wanalipwa Posho za kujikimu (Subsistance Allowance) na Ofisi za Bunge, Lakini wakienda kwenye Taasisi au Mashiriki ya Umma au Serikali za Mitaa wanalipwa tena posho za kujikumu (Subsistance Allowance) kwa shughuli hiyo hiyo ambayo Bunge imeshawalipa.

Hapa kuna posho za aina mbili ambazo tusizishanganye. Posho ya kujikimu (Subsistance Allowance) na posho ya Kikao (Sitting Allowance). Wao Wabunge walitakiwa kulipwa posho za Vikao (Sitting Allowance) kama wanatembelea Mashirika ya Umma na kukawepo na Vikao vya kupitia taarifa ya Mashirika au Taasisi hizo na siyo kulipwa posho ya Kujikimu.

Suala la kuhojiwa kwa Wabunge na TAKUKURU- Huu ndiyo urasimu ambao hata wabunge wenyewe wanaihoji Serikali kutowachukulia hatua watuhumiwa wa sakata la RICHMOND. Unajua kila unapotaka kufanya suala la maendeleo Tanzania unakuta kuna URASIMU MKUUUUUUBWWWWAAAAAA!!! ambao mpaka unapo kamilisha taratibu zake kunakuwa hakuna maana tena. mini nasema acha wahojiwe.

Mapadri wa Roma wanamsemo wao mzuri sana nami hua naupenda nami leo nawapeni unasema hivi:

"MBWA HUBWEKA SANA ANAPOONA CHAKULA CHA BWANA WAKE KINALIWA NA MTU MWINGINE. LAKINI MBWA HUYO HUYO ANAPOKULA CHAKULA HICHO CHA BWANA WAKE BILA RIDHAA YA BWANA WAKE - HUWA MKALI PALE ANAPOKATAZWA KUENDELEA KUKILA"

Kama ufisadi ni kutumia Tshs. 10,000/- za wanakijiji na kunapelekea Afisa Mtendaji wa Kijiji ahojiwe na kufuikishwa Mahakamani, inakuwaje suala la Wabunge kuchukua Posho mara 2 na wanapotakiwa kuhojiwa INAKUWA SUALA LA OOOO!!!!, UNAJUA!!!. Jamani ACHENI UMBUMBUMBU fungeni macho na msiwe BENDERA KUFUATA UPEPO.
hili suala kwani ni rushwa au double payment, kama ni double payment sio suala la takukuru bali polisi, cag na la kiutawala zaidi.
tanzania suala la mambo ya allowance lipo kwenye taasisi karibu zote, ndio maana mwakyembe amesema mbona wenyewe takukuru waliwalipa wabunge walipo hudhuria semina hapo dar? waandishi wa habari wengi hulipwa makazini mwao na wanapofika kwenye semina or press conference hulipwa tena na waandaji, issue za rushwa zipo nyingi tu tena fedha nyingi tu ambazo takukuru hawazifuatili, eg juzi juzi tu hapa bunge lilifuta 15bn ambazo zilikuwa zina tokea katika audit report kwa matumizi yaliokosa viambatanisho nk.
hili la allowance ni la kulitolea ufafanuzi na kama kuna hitaji kuchukuliwa hatua ni kwa wahusika kurudisha hizo fedha.
 
huyu Mwakyembe hana lolote he is just another breed of fisadiz...sipotezi hata muda kumsikiliza
 
Mheshimiwa,

Timing ya kuwahoji hawa wabunge wakiwa wanajiandaa kwenda bungeni kwenye sakata la richmod nadhani ndo limeleta shida. Pia kuhoji kwa kutumia simu hapo sijui sheria inasemaje. Pia Utumishi watoe mwongozo wa serikali nzima kuhusu haya mambo ya allowance kwani Kuanzia Mawaziri, Makatibu wakuu, wakurugenzi n.k hii kitu inawakumba siyo wabunge peke yao.

vita ni vita huwezi chagua vije lini ..so hapa kilichofanyika ni kuwa frustrate completely kuelekea kikao cha 17 cha Bunge la Speed and Standards..hahaaaaaa
 
Kwa mtazamo wangu naona huu mjadala umeletwa ili kuwadivert watu kutoka kwenye masuala ambayo Bunge lilipaswa kupokea taarifa yake sasa. List za waliopewa posho bungeni na kwenye vikao sehemu nyingine inajulikana, wanawahoji ili nini, kama sheria inasema wazi posho ni moja tu? Nadhani tuanze kuwawajibisha kwanza wale waliolipa hizo posho huku wakijua hao wabunge wamelipwa walikotoka. Watasema wabunge wanashinikiza, hakuna sheria inayowalinda kuhusu hilo, tatizo mashirika mengi ya umma wanatumia hizo nafasi kuwanyamazisha wabunge kwa kuwalipa hizo posho ili wasiwabane, na pia ni loophole ya kufanikisha wizi wao. Huo uchunguzi kwa nini usifanyike kwenye nyaraka walizonazo? au hawana kumbukumbu kama kawaida yao?
Ikulu gani imeamuru uchunguzi ufanyike wakati Kagoda imeshikwa na kigugumizi kuichunguza? I doubt!
 
nini tafsiri ya rushwa? ni pale mpokeaji anapoomba hiyo rushwa ili iwe kichocheo cha maamuzi yake, kwa faida ya mtoaji, au mtoaji anapotoa rushwa kwa mpokeaji kwa ajili ya mchochea mpokeaji atoe uamuzi kwa faida ya mtoaji.
pili sheria inasema wote ni wakosaji yaani mtoa na mpokeaji, kizuizi ni ikiwa kuna aliye toa taarifa kwa mamlaka husika kwamba fulani kaniomba au fulani anataKA kunipa rushwa.
sasa kwenye hili suala je kulikuwa na nia ya kuinfluence maamuzi? na je hayo maamuzi yalikuwa infavour of mtoaji?
je mtaoji wameulizwa hili kwa maana ya kuhojiwa na takukuru, sababu za kutoa hiyo rushwa? au ilikuwa ni takrima ambayo ilikuwa na nia ya ku-influence uamuzi wa wabunge lakini haikuwa hivyo?
 
Mawaziri wana wataalamu wa kuwashauri katika mambo ya kazi zao. Nadhani wanaitwa aidha Personal au Private Assistants. Sijui kama wabunge nao wanautaratibu huu.

Kutokana na kukurupuka kwao na kutoa statements ambazo zinaonyesha wazi kuwa ni kinyume na sheria za nchi, naona kuna umuhimu wa ofisi ya Bunge kuhakikisha kuwa wanaajiri wasaidizi hao kwani fedha wanazolipwa kama mishahara na marupurupu ni nyingi.

Ninapendekeza hayo kwa sababu naona wabunge wameanza kupoteza muelekeo kutokana na kauli wanazozitowa. Wana miss interprate sheria kiajabu kabisa.

Hivi ni kinga gani aliyonayo Mbunge anayevunja sheria kwa kufanya kosa la jinai? Pili ni sheria gani inayompa kinga Mbunge kukataa wito wa chombo cha dola? Mwisho wa yote watakataa hata wito wa Mahakama eti kwa sababu wao ni Mhimili kamili. Hoja za namna hii zinaonyesha wazi kuwa wanahitaji msaada wa wataalamu.

Wabunge kama watunga sheria, ni muhimu wawe mstari wa mbele kuitii sheria hizo wanazozitunga ama sivyo itakuwa nchi inaendeshwa kwa misingi ya fujo tu.
 
Hawa Takukuru wasituletee mazingaombwe.Hatupingani nao na swala zima la kuwahoji
hao wabunge lakini kwa nini wanashindwa kuwashughulikia mafisadi ambao wananchi wanalia ni mwaka wa nne sasa wanarukia swala la posho kwa wabunge? Waanze na mafisadi, wabunge si wapo watashughulikiwa tu!. Wasitufanye sisi wajinga.. Tunajua janja yao. Takukuru acheni usanii. Mnataka kugusa pale pale panapowagusa ninyi. Toa boriti kwenye jicho lako ndipo utaona kibanzi kwenye jicho la mwenzako.
 
nini tafsiri ya rushwa? ni pale mpokeaji anapoomba hiyo rushwa ili iwe kichocheo cha maamuzi yake, kwa faida ya mtoaji, au mtoaji anapotoa rushwa kwa mpokeaji kwa ajili ya mchochea mpokeaji atoe uamuzi kwa faida ya mtoaji.
pili sheria inasema wote ni wakosaji yaani mtoa na mpokeaji, kizuizi ni ikiwa kuna aliye toa taarifa kwa mamlaka husika kwamba fulani kaniomba au fulani anataKA kunipa rushwa.
sasa kwenye hili suala je kulikuwa na nia ya kuinfluence maamuzi? na je hayo maamuzi yalikuwa infavour of mtoaji?
je mtaoji wameulizwa hili kwa maana ya kuhojiwa na takukuru, sababu za kutoa hiyo rushwa? au ilikuwa ni takrima ambayo ilikuwa na nia ya ku-influence uamuzi wa wabunge lakini haikuwa hivyo?

Si ndio maana Takukuru wanataka wawahoji wahusika ili wapate majibu ya maswali yote hayo? Watajuaje kama hawakuwahoji wabunge waliopokea ili wajue waliomba hizo fedha kwa madhumuni gani?

Wakitosheka kuwa ilikuwa si rushwa bali "kuwalainisha tu wasiingi ndani zadi katika uchunguzi wao" basi wataachiwa.
 
Nipe jibu kwanini Mheshimiwa anakataa kwenda kutoa maelezo ya kuisaidia Takukuru..

Do your home work ameanisha sababu za kutokwenda na akawaambia wakutane mahakamani....need more?
 
MIMI NAAMINI TANZANIA DAIMA INAYOMILIKIWA NA MBOWE HAIAMINI KATIKA SIASA ZA CCM NA MGAMBO WA UFISADI...KWA STORI KAMA HIZI, GAZETI HILI LINATHIBITISHA HOJA YA CHADEMA KWAMBA CCM NI WALEWALE.....HAWA MGAMBO WA UFISADI NI WASANII TU KAMA ALIVOFANYA USANII JK KWA MBWEMBWE ZA ARI, NGUVU NA KASI MPYA!...KAMA MNATAKA MAGAZETI YA KUTETEA MGAMBO WA UFISADI SOMENI MAGAZETI YANAYOMILIKIWA NA KAMANDA WAO-REGINARD MENGI...SIO MAGAZETI YA MBOWE....SOMENI NIPASHE, KULIKONI, THIS DAY,..nk ambayo ni mali ya bwana mengi...sio kazi ya mbowe kulinda mgambo wa ufisadi...
 
Do your home work ameanisha sababu za kutokwenda na akawaambia wakutane mahakamani....need more?

Homework nimekwisha fanya. Ni kosa la jinai kukataa wito wa chombo cha dola kama Polisi, Mahakama na PCCB. Sababu alizozitoa hazina mashiko kisheria na ndio maana wenzake wote wakaenda.

Huyu jamaa yako, kama mtunga sheria na mwana sheria, anaonyesha mfano mbaya mbele ya jamii kwa kuvidharau vyombo vya dola. You get me now sir?
 
Back
Top Bottom