Dr. Mwele Malecela: Asiyekuumba, kukuumbua hawezi

Dr. Mwele Malecela: Asiyekuumba, kukuumbua hawezi

Hicho kifua hana. Yeye ni kufyatuka tu!
Binafsi naamini Raisi naye anapenda kuanzisha Mijadala isiyo na tija.

Kwani ni lazima kusema kila Jambo linalomfurahisha au kumkera Sana?

Suala la Dk. Mwele lilishapita na hakutakiwa kulizungumzia tena kwa kuliunganisha na taasisi za kimataifa ambazo kesho na kesho kutwa tutahitaji msaada wao pale ambapo magonjwa ya mlipuko yatakapo tokea.

Jana nimeona BBC NEWS habari kubwa ilikuwa ni Raisi kumpongeza Ofisa aliye charaza wanafunzi viboko.

Huu nao pia ni mjadala mkubwa ambao ameuanzisha na hauna tija. Chanzo cha mjadala huu ni hotuba yake aliyoitoa Jana.

Mh. Raisi ajitahidi kuwa na kifua cha kuifadhi mambo hata kama yanamfurahisha au kumsikitisha.
 
Angemjibu kwa Mithali 26:4 ingependeza zaidi.
Aliyekua Mkurugenzi Mkuu wa NIMRI Bi.Mwele malecela ameposti katika akaunti yake ya twitter maneno haya. Nadhani huu ni mrejesho baada ya tamko la Mwenye nyumba kuwa Daktari Mwele malecela alikua anatumika na MABEBERU.


View attachment 1223939
View attachment 1223982
View attachment 1223983

=====

RAIS John Pombe Magufuli, amesema moja ya sababu kumtumbua aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za Kiafya NIMR, Mwele Malecela, ni kiongozi huyo kutoa taarifa ambazo hazikuwa sahihi kuhusiana na ugonjwa wa Zika.

Magufuli ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Songwe, wakati alipofika kwenye ziara ya kikazi na kufanikiwa kuzindua kiwanda cha kahawa kilichojengwa na wajasiriamali wa Tanzania, ambapo amesema moja ya mambo ambayo yalipelekea kumtoa kwenye nafasi hiyo Malecelea ni kutangaza ugonjwa.

“Maneno huwa hayaishi, kuna wakati walitangaza kuna ugonjwa wa Zika nchini Tanzania, alipotangaza hivyo wakati mimi najua haupo nilimfukuza saa 7:30 usiku, wala hakuna cha Zika iliyotokea. Baada ya wiki moja wakamteua akawa bosi wao, hii ilionyesha alitumwa kusema aliyoyasema; hizi ni mbinu za kibeberu,” amesema Rais Magufuli.
 
Mzee alitaka kuona Dr. akihangaika mitaani mwisho apigiwe magoti kama kina Mwigulu, January na Kinana instead nyota ya Dr. inazidi kung'ara.
Kuna ma-mtu yana roho za shetwani ingawa kwa nje ni ma-binadamu! Shetani linateseka sana moyoni!
 
Mzee alitaka kuona Dr. akihangaika mitaani mwisho apigiwe magoti kama kina Mwigulu, January na Kinana instead nyota ya Dr. inazidi kung'ara.

Na Ile Kauli yake ya kibaguzi ya 'bahati mbaya Ni mgogo'.....

Kama wagogo wakimpigia kura nitawashangaa Sana...
 
..Dr.Mwele Ntuli Malecela katupa kombora lingine.

..amemnukuu mwandishi George Orwell ktk maneno haya," ...the further the society drifts from the truth, the more it will hate those that speak it..."
its true, the "stone" has tried to brand her as an enemy of the nation while its vice versa
 
Back
Top Bottom