Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 6,710
- 9,063
Aliyekua Mkurugenzi Mkuu wa NIMRI Bi.Mwele malecela ameposti katika akaunti yake ya twitter maneno haya. Nadhani huu ni mrejesho baada ya tamko la Mwenye nyumba kuwa Daktari Mwele malecela alikua anatumika na MABEBERU.
View attachment 1223939
View attachment 1223982
View attachment 1223983
=====
RAIS John Pombe Magufuli, amesema moja ya sababu kumtumbua aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za Kiafya NIMR, Mwele Malecela, ni kiongozi huyo kutoa taarifa ambazo hazikuwa sahihi kuhusiana na ugonjwa wa Zika.
Magufuli ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Songwe, wakati alipofika kwenye ziara ya kikazi na kufanikiwa kuzindua kiwanda cha kahawa kilichojengwa na wajasiriamali wa Tanzania, ambapo amesema moja ya mambo ambayo yalipelekea kumtoa kwenye nafasi hiyo Malecelea ni kutangaza ugonjwa.
“Maneno huwa hayaishi, kuna wakati walitangaza kuna ugonjwa wa Zika nchini Tanzania, alipotangaza hivyo wakati mimi najua haupo nilimfukuza saa 7:30 usiku, wala hakuna cha Zika iliyotokea. Baada ya wiki moja wakamteua akawa bosi wao, hii ilionyesha alitumwa kusema aliyoyasema; hizi ni mbinu za kibeberu,” amesema Rais Magufuli.
Dada Mwele Malecela ni binti wa Mzee John Samwel Malecela ambaye amewahi kuwa Waziri Mkuu wa nji hii lakini pia aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za Uwaziri katika Wizara tafauti tafauti enzi za Mwalimu na wakti wa Mzee Ruksa.
Jambo ninalofikria hapa ni vipi Bwana John Pombe Magufuli anaweza kuthubutu kumtukana, kumdhalilisha Dada Mwele kiasi hichi kisa ugonjwa wa ZIKA..?? Kumdhalilisha au kumtukana mtoto wa Mzee Malecela ni sawa na kudhalilisha na kumtukana Mzee huyo..!!Hivi Mzee Malecela anajisikiaje anapomwona Magufuli akiongea kwenye runinga au redio?
Mtu ulishamtumbua...lakini ana elimu yake ya Kimataifa na kaajiriwa huko kwa sifa alizonazo halafu Rais unaanza kuropoka eti MABEBERU ndio waliomtuma kusema Tanzania kuna ZIKA....!!! Hawa Mabeberu unaowasema ni Shirika la Afya Kimataifa (WHO-World Health Organization)linaloshughulikia maswala ya Kiafya dunia nzima...!!!
Swali la Kufikirisha : Hivi Rais Magufuli akishtakiwa Mahakamani na Shirika la Afya Duniani(WHO)kwa kulidhalilisha na akaambiwa alete USHAHIDI USIOTILIWA SHAKA ya kwamba Dr. Mwele Malecela alitumwa na WHO(Mabeberu-according to Magufuli)kutamka kwamba ZIKA ipo Tanzania na ndo maana wakampa kazi ataweza???