Dr. Mwele Malecela aula WHO

Dr. Mwele Malecela aula WHO

Hivi huwa mnafaidika nini kushangilia mtu asiyekujua wala kukufahamu akipata ulaji ambao ni kwa ajili yake na familia yake?

Binafsi sijawahi kulielewa hili!
Unaowajua wanakuletea hela home. Au kama ni mtumishi wa umma amekupa maslahi yako? Jitambue usiwe kibendera lofa kweli
 
Bado unaishi kwa matukio?? Hiyo nafasi ndio itakujengea reli, itakujengea barabara, itakuletea dreamliner, itakununulia vivuko..ifike mahali mpunguze mihemko ya kisiasa..nipe mafanikio ya nchi asharose migiro alipokuwa deputy general UN..
Nchi haibadilishwi na mtu mmoja bali pale kunapokuwa na mazingirwa wezeshwi ya kumfanya kila mtu atumie uwezo wake, vipaji vyake na ujuzi wake katika kuchangia maendeleo ya nchi.

Wa kwetu anadhani ana akili kuliko wote, ana uwezo kuliko wote, ana vipaji kuliko wote. Kwa fikra hizo hawezi kuipeleka nchi popote. Ndiyo maana kukiwa na kitu kidogo kelele huwa nyingi sana ili kutafuta sifa binafsi.

Nchi haiwezi kubadilika kwa sababu ya dreamliner pekee au reli pekee au umeme pekee. Kuna mambo mchanganyiko yanayochangia nchi kuendelea.

Hakuna cha pekee kinachofanyika awamu hii tofauti na awamu nyingine. Awamu zilizopita walijenga shule, vyuo, vyuo vikuu, viwanda, hospitali, zahanati, barabara, madaraja, n.k.

Tofauti ya awamu hii na nyingine zote ni kuwa awamu hii inaongoza kwa kupiga kelele. Kitu kidogo kelele nyingi kupindukia. Likijengwa daraja la waende kwa miguu, itakavyotangazwa ni kama tumejenga daraja la kuvuka mto Nile. Ikijengwa barabara ya kilometer 4, itakavyotangazwa ni kama tumehrnga barabara ya kilometer 4,000. Ni awamu ya maneno mengi na kutafuta sifa.
 
Aibu kwa Jiwe!!
Shida kubwa kiongozi wetu anapenda watu wasio na akili, watu watakaomtukuza na kumwimbia nyimbo za sifa. Wenye akili hawataki maana wenye akili hawawezi kufanya kazi ya kumlamba vidole kama wafanyavyo akina Bashite.
 
This is something to get us in the #FridayFeeling: A huge congratulations to @mwelentuli⁩ for her appointment as the new NTDs Director at ⁦@WHO⁩. A great appointment by @DrTedros⁩.
View attachment 887879
Mwaka 2016 Uteuzi wa Dk. Mwele Malecela kama Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (National Institute for Medical Research – NIMR) ulitenguliwa na Rais John Magufuli, siku moja baada ya Dk. Mwele kusoma hadharani ripoti iliyoonesha kuwa kuna kina mama wamekutwa na dalili za virusi vya ZIKA nchini Tanzania.

Pamoja na yote hayo, Dk. Malecela anashikilia rekodi nyingi na kubwa sana. Kwa mfano, Dk. Mwele ndiye mwanamke wa kwanza duniani na mwafrika wa kwanza kuteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Kimataifa cha Taasisi za Afya Jamii (IANPHI) taasisi ambayo ni mwamvuli wa taasisi zote za kitaifa za afya kwenye mataifa yote duniani.

Dk. Malecela alijiunga NIMR mwaka 1987 baada ya kuhitimu shahada zake kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM), pia ana Shahada ya Uzamivu (PhD) kutoka Chuo Kikuu cha London Uingereza mwaka 1995.

Sekta ya Afya nchini Tanzania haitamsahau kwa mchango wake mkubwa kwenye kujenga misingi ya tafiti za afya na hasa usimamizi wake kwenye Mchakato wa Kuweka Vipaumbele vya Kitaifa vya Tafiti za Afya ambao ulianzishwa mwaka 1999 na baadaye kufanyiwa mapitio mwaka 2005.
Kuelewa uwezo wa mwenye akili ni lazima nawe uwe na akili.
 
Hivi huwa mnafaidika nini kushangilia mtu asiyekujua wala kukufahamu akipata ulaji ambao ni kwa ajili yake na familia yake?

Binafsi sijawahi kulielewa hili!
Huwezi kuelewa kama huna uwezo wa kuelewa.

Huyu Mama anatoa mchango mkubwa kwa afya ya Dunia, na kila nchi iliyopo kwenye Dunia.

Mwendawazimu hata akaambiwa kuna teknolojia mpya ya tiba imegundulika atasema inanisaidia nini mimi, kwa sababu tu siku hiyo ana afya njema.

Tabia ya wap.umbavu wote ni kuguswa na mambo ya wakati huo, hawana fikra juu ya kesho wala keshokutwa.
 
Dr. Malecela is patron and Founder of the IMANI Group, which is a support group of people living with HIV/AIDS.

=======

Kwa wazungumza Kiswahili:

Hongera sana, Dr Mwele....[/QUOTE]


Duh! Umenichekesha kweli hiyo kwa wazungumza Kiswahili.

Umenikumbusha hadithi moja. Ilkuwa meli inazama, Captain akawaambia abiria, wale wote wanaojuwq kuogelea.wakae mkono wa kulia na waliokuwa hawajui kuogelea mkono wa kushoto. Akagawa life jackets kwa wote. Kisha akawaambia wanaojuwa kuogelea wachupe majini. Baadae akawageukia wale waliobakia ambao hawajui kuogelea na kuwwambia, " good luck" na yeye akachupa majini.
 
mzee wa visasi, anatamani amfate na huko akamtumbue tena..
prof. mwandosya pole broo
ndio tabia za jiwe !
 
ninachojuwa ni kwamba Dr Mwele lazima amepata baraka za serekali kuweza kupata hizo nafasi. Msiwachonganishe watu wakuu
Usitudanganye. UN huna haja ya kupata baraka toka serikalini. You play your part and you apply if you pass the interview you get the post. UN Ina consult nchi anayokwenda kwa kukubaliwa kwake. Nchi atokayo haina la kusema. She is already with UN anyway it is just a move from one station to the other.
 
Back
Top Bottom