Dr. Mwele Malecela aula WHO

Dr. Mwele Malecela aula WHO

Nani kamfitini? Ni kweli nchi ilikuwa na ZIKA? kama ni kweli hiyo zika imeishia wapi? Lazima tukubaliane alikosea tuuu.... kupata cheo kingine hakuprove kuwa hakukosea....
Kama mlikataa kuwepo sasa unaiuliza vipi? Ulofa ni mzigo, na Zika ipo tu.
Hakuna siku wajinga hugeuka wenye vipaji maalum, ila wajinga watabakia kuwa wajinga tuu hadi mwisho wa dahari.
 
Kipara labda ana mshinda Bashite tu nchini kwakutema yai ila wote ni wachovu japo wanakipenda kimombo sema chenyewe akiwapendi
 
Hivi anayeula Tanzania kila mara huwa ni Dr. Mwele Malecela tu peke yake? Najiuliza hivi kama isingekuwa huyu Mwanamama ' Kutotumbuliwa ' na Rais JPM tungekuwa tunamzungumzia hivi kila mara huku tukitumia ' teuzi ' zake anazozipata huko Nje kama fimbo ya Kumnanga / Kumsema Magufuli?

Tusilazimishe kwamba kila Mtaalam basi lazima awe anafaa katika Uongozi fulani na tujifunze pia kuheshimu Maamuzi ya Mtu juu ya Mtu fulani. Mbona hamshangai katika Mpira wa Miguu unakuta Mchezaji fulani ni mahiri / mzuri kabisa ila akija tu Kocha mpya na kutokana na mfumo wake ataonekana hafai na ama atamweka benchi au ataamua auzwe kwakuwa atakuwa hamuhitaji.

Sina shida na huyu Mwanamama Dr. Mwele Malecela kwani ni Msomi mzuri tu na si Msomi tu pekee bali pia hata Kichwani ( Upstairs ) bado ametukuka ila nachukizwa na tabia za Kiswahili / Kimajungu ambazo nimekuwa nikiziona hasa pale akipata tu ' Wadhifa ' fulani Watu wataupokea katika mwelekeo wa Kumsema Rais Dr. Magufuli kwamba ameacha Mtu muhimu.

Tubadilikeni tafadhali na siku zingine muwe mnatuwekea na Watanzania wengine ' walioula ' Kimataifa kwani wapo wengi tu ' otherwise ' tutakuwa tunaiendeleza ile ile tabia ' zoeleka ' ya Watanzania ' Wanaharakati ' ya Unafiki!
kwa mtazamo wako unaona waliomthamini kumpa heshma ya kumpa ukuu hawana akili ila JIWE lako ndo linaakili pale llipomtumbua.
UWE UNAJIONGEZA WAKATI MWENGINE.
Usijifanye mjuzi kilakitu unajua[emoji83] [emoji83] [emoji90] we

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Mshahara wake na marupurupu vinaweza kufika US$50,000 kwa mwezi?
 
Huu uzi unatufundisha mengi......binadamu hata kama watapenda ufanikiwe...Lakini hawatapenda uwazidi. do better but not better than them. Ukisoma huu uzi unaona kabisa kuna watu wameumia.

Ndugu zangu, ndo mambo tunaongea humu kila siku: dunia ina fursa nyingi sana. Kwa uzoefu wangu, nafasi kama hii ya Dr. Mwele, HAIHITAJI government clearance or support. Ni weledi na taaluma yako. Hii inadhihirisha kwamba huyu dada/mama ni very competent. Kwenye post kama hii applicants siyo chini ya 1000! Sasa mpaka kutoboa ujue kabisa huyu ni habari nyingine. kazi za UN SIYO ZA KUGAWANA U-DC na U-RC wa Taifa letu pendwa!

Again, nampongeza sana Dr. Mwele. Aende atuwakilishe vizuri. Na hopefully pale atakapoweza kuunga mkono juhudi za waTanzania wenzake wanaotafuta fursa WHO na kwingineko........ itakapowezekana awape support!

Huu ni ushindi wa Taifa letu. inabidi Waziri Ummy Mwalimu na Mahiga on behlf of the Government amwandikie hata barua ya kumpongeza kwa kuteuliwa kwa hii nafasi. kwa nafasi kama hii (I am sure ni D-2) NI CHACHE SANA! na Kuipata..ni changamoto kubwa.....Kwa hiyo Tanzania lazima tujivunie haya mafanikio. Kwa wanaojua wananielewa.

God bless Tanzania.
Masanja umenena. Nakumbuka Askofu Mkuu Rugambwa alipoteuliwa na Pope Emeritus kuwa Balozi wa Vatican nchini Angola, Mheshimiwa Raisi JM Kikwete alimtumia salamu za pongezi. Hiki ni "kichwa" cha kitanzania na isitoshe ni zao la shule za kitanzania. Ndiyo mambo ya "kutembea kifua mbele". Naunga mkono hoja.
 
This is something to get us in the #FridayFeeling: A huge congratulations to @mwelentuli⁩ for her appointment as the new NTDs Director at ⁦@WHO⁩. A great appointment by @DrTedros⁩.
View attachment 887879
Mwaka 2016 Uteuzi wa Dk. Mwele Malecela kama Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (National Institute for Medical Research – NIMR) ulitenguliwa na Rais John Magufuli, siku moja baada ya Dk. Mwele kusoma hadharani ripoti iliyoonesha kuwa kuna kina mama wamekutwa na dalili za virusi vya ZIKA nchini Tanzania.

Pamoja na yote hayo, Dk. Malecela anashikilia rekodi nyingi na kubwa sana. Kwa mfano, Dk. Mwele ndiye mwanamke wa kwanza duniani na mwafrika wa kwanza kuteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Kimataifa cha Taasisi za Afya Jamii (IANPHI) taasisi ambayo ni mwamvuli wa taasisi zote za kitaifa za afya kwenye mataifa yote duniani.

Dk. Malecela alijiunga NIMR mwaka 1987 baada ya kuhitimu shahada zake kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM), pia ana Shahada ya Uzamivu (PhD) kutoka Chuo Kikuu cha London Uingereza mwaka 1995.

Sekta ya Afya nchini Tanzania haitamsahau kwa mchango wake mkubwa kwenye kujenga misingi ya tafiti za afya na hasa usimamizi wake kwenye Mchakato wa Kuweka Vipaumbele vya Kitaifa vya Tafiti za Afya ambao ulianzishwa mwaka 1999 na baadaye kufanyiwa mapitio mwaka 2005.
Baada ya kutumbuliwa,inaonesha alijifunza vingi
 
Nani kamfitini? Ni kweli nchi ilikuwa na ZIKA? kama ni kweli hiyo zika imeishia wapi? Lazima tukubaliane alikosea tuuu.... kupata cheo kingine hakuprove kuwa hakukosea....
tetea ujinga wa jiwe [emoji90] [emoji90] [emoji83] ...mbafff wee
 
Anayekosea anashushwa cheo au kufukuzwa kabisa. Unakosea unapandishwa cheo! What precedence? Yale ya kwenu ya vyeti feki kuchapa kazi unayapeleka WHO? Miaka mingapi kafanya kazi hapo NIMR! Kutoka chini kabisa kapanda hadi kuwa Mkurugenzi, bado unauliza viswali vya hovyo tu? Ulitaka ukutane na hiyo Zika Kariakoo? Kama inadhibitika ikadhibitiwa!
mwambie aende pale fery kivukoni atakutana na ZIKA 3 zinaishipale zinaombaomba
 
Your wrong kabisa.... Mwale kuwambombezi hakumfanyi kuwa mkamilifu lazima tukubali alikosea sana tena sana kutangaza tanzania kuna Zika ....jiulize zika yake iliishia wapi?
Tatizo ya Mwale she is not a medical doctor. Yeye ni mtu wa zoology. Hakustahili kuongoza a national medical research institute, being not a medical proffessional.
 
That is reality mkuu, alionewa kabisa
Alionewa kwa kupewa kuongoza taasisi ambayo hana utaalamu nayo. Hivyo akavurunda kwa kukiuka codes of ethical medical conducts. Ikawa hakuna namna nyingine JPM ya kumfanya isipokuwa kumtumbua!
 
kwa vile alisoma UK tena Chuo maarufu duniani CV yake Ni kubwa. Hizi nafasi za kazi hazipatikani kimchezo mchezo. Pongezi kwake
 
Kuelewa uwezo wa mwenye akili ni lazima nawe uwe na akili.
Sasa kosa lake nini huyo mama kutoa taarifa ya ukweli kuhusu ugonjwa kosa? Sasa bora mungu kamwona akafanye kazi. Ya utaalamu wake bila mashinikizo ya kijinga
 
Back
Top Bottom